Pages

Saturday, April 23, 2011

AFA KWA UMEME






mfanyabiashara Bashiru Sebastian (33) amekufa baada ya kunaswa na umeme juzi saa 2:30 usiku katika eneo la Temeke Sudan, Dar es Salaam.

Akielezea ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema Bashiru na mwenzake Yasin Shaban (35) walipokuwa wakitokea msikitini juzi, walikuta nguzo ya umeme ya msongo wa megawati 32 imekatika na waya ukining’inia.

Amesema, wakati wakipita karibu na nguzo hiyo, Bashiru alinaswa na kufa papo hapo na Shaban alipojaribu kumnasua mwenzake alipata mshtuko kwenye mguu wa kulia na mkono wa kulia na amelazwa katika Hospitali ya Temeke.

No comments:

Post a Comment