Pages

Tuesday, April 12, 2011

jahazi wawafunga usher family

WANAMUZIKI wa bendi ya taarab ya jahazi modern taarabu, leo wamewafunga waandaaji wa shughuli za burudani maarufu kwa jina la usher family ya Temeke, katika mchezo wa mpira wa miguu kwa goli moja kwa nunge lililofungwa na kiongozi wa bendi hiyo Mzee Yusuph, mchezo huo uliofanyika katika viwanja vya Luxury pub na kuhudhuliwa na umati wa watu.
Mchezaji Kiboko arambee maarufu kwa jina la HB JAX, itabidi ajutie makosa aliyokuwa akiyafanya katika kipindi cha kwanza dakika ya 27 na kipindi cha pili dakika ya 81 baada ya kupoteza nafasi za wazi alizokuwa akizipata kupitia wingi ya kushoto Dady brown mopao.
hadi dakika tisini zinamalizika jahazi walitoka kifua mbele kwa goli moja kwa nunge
wakati huohuo
Mashindano ya khanga sebene yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Usher family  na kampuni ya Aset Entertiment yaliyokuwa yanawashirikisha wanawake kumi katika kucheza sebene huku wakiwa wamevaa vazi la khanga, yamefikia hatua ya fainali na inatarajia kufanyika siku ya jumapili tarehe 17/04 katika ukumbi wa TCC Chang'ombe jijini Dar es alaam
hadi kufikia hatua hiyo ni wanadada watano ndio waliongia hatua hiyo ya fainali ambapo mshindi wa kwanza anatarajia kuchukua kitita cha Sh 200,000. mshindi wa pili 150,000. na mshindi wa tatu ataibuka na kitita cha 100,000.
mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu ZANTEL na mkurugenzi wa high way park Hussein Macheni.

No comments:

Post a Comment