Pages

Monday, April 11, 2011

APIGWA MOTO BAADA YA KURUKA UKUTA





Pius Micky wa blogu ya Spoti Starehe anafahamisha kupitia blogu yake na ukurasa wa Facebook kuwa, kijana mmoja kwa jina Lilah Hussen (pichani) amechomwa na moto mwili mzima na walinzi wa Hotel ya South Beach wakishirikiana na Meneja mmiliki wa Hotel hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Shipata.

Wakiongea na kamera ya Spoti Starehe, ndugu wa majeruhi huyu wamesema kuwa ndugu yao alifika ufukweni hapo ambapo kila mwisho mwa wiki panakuwa na muziki kwa ajili ya kujiburudisha na alipoingia ndipo alipokamatwa na walinzi kwa kutokuwa na alama maalumu ambayo huvaliwa mkononi kwa waliolipa kiingilio (kiingilio ni Tsh. 7000/- kwa mtu) ndipo walipompeleka kwa Meneja wa Hoteli hiyo na aliamrisha kijana huyo avishwe mpira na kuchomwa moto.

Bwana Lila ambaye kwa sasa emehamishiwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili amesema yeye ni mfanyabiashara ndogo ndogo na mkazi wa Kigamboni na kuwa alikwenda hapo baada ya kuvutiwa na muziki pasipo kujua hayo yangemkuta.

Ndugu wa majeruhi huyu wamefungua kesi katika kituo cha Polisi Kigamboni lakini kwa masikitiko wanasema bado si uongozi wala walinzi wameshakamatwa.

Ufukwe wa South Beach unajizolea umaarufu kwa michezo ya ufukweni lakini wananchi wa kawaida ambao wanaishi eneo hili wamekuwa wakilalamikia ada kubwa ya kiingilio ufukweni hapo ikiwa ni Tsh. 7000/- ada ya kuingia tu bila kinywaji.

credit : Pius Micky/Spoti Starehe blog

1 comment:

  1. that guy nasikia tayari keshakufa na hakuna taarifa hatua yoyote nasikia iliyochukuliwa R.I.P bro

    ReplyDelete