Pages

Saturday, April 9, 2011

HITMA YA FIVE STAR



Kwanza kabisa ningependa kukufahamisha  kuwa imeundwa kamati ya kusimamia kisomo cha wasanii wa Five Star Modern Taarab waliofariki katika ajali iliyotokea Jumatatu 21/03/2011 Mkoani Morogoro.

Kamati hiyo itakuwa chini ya Mwenyekiti Mh. Abbas Mtemvu (Mbunge wa Temeke), Makamu Mwenyekiti: Sheikh Omar Alhadi ( Naibu Imamu msikiti wa kichangani), Katibu: Saidi Mdoe (Mkurugenzi Screen Masters) Mweka hazina ni Ashraf Ahmed (Mkurugenzi wa fedha East African Melody)

Kamati hii ina jumla ya wajumbe 14 wakiwemo Idd Azan (Mbunge wa Kinondoni) Mh. Azan Zungu(Mbunge wa Ilala na wengineo wengi.

Kamati hii kwa kushirikiana na uongozi wa Five Star umeamua kufanya hitma kubwa yenye sura ya kitaifa siku ya Jumapili 17/04/2011 katika ukumbi wa PTA sabasaba.

Ili kufanikisha shughuli hii ukiwa kama mdau wa sanaa hapa nchini, kamati inaomba mchango wako wa hali na mali

Tunaomba uwasilishe mchango wako kwa mweka hazina (Ashraf Ahmed 0713232747) au kwa katibu Saidi Mdoe( 0713 606109) kabla ya terehe 10/04/2011 na utapatiwa stakabadhi ya kuthibitisha mchango wako kupokelewa.

Said Mdoe
Katibu

4 comments:

  1. tunashukuru kwa kutupa taarifa, ila mbona kamati yenyewe imeundwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi tu huku tukiwa na wabunge vyama vya upinzani Mf. halima Mdee, Kawe, Mnyika Ubongo je! kweli itakuwa na sura ya kitaifa ilivyoanishwa humu au mnasemaje washika dau me naona zengwe tu siasa zinatawala kila upande nilitegemea ungepigwa mseto kila mtu awepo lakini mmm aya tuombe uzima

    ReplyDelete
  2. mambo hayo sinaga faida nayo wanajijua wenyewe
    kama kitaifa kichama shauri yao mipasho tu kila sehemu

    ReplyDelete
  3. Napata tabu na hiyo kauli ya Hitma yenye sura ya kitaifa, hapo nafikiri wangetafuta neno jingine la kutumia labda wangesema kumbukumbu au Tamasha la kuwakumbuka. lakini kusema Hitma ya kitaifa ina maana viongozi wa madhehebu ya dini tofauti watakuwepo pia kuwaombea kama inavyokuwa siku ya mashujaa?
    sana sana Khitma za muundo huo zinakuwa za kibishoo na kujionyesha tu, ukichukulia hicho kisomo na hiyo kalamu ni kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi mungu awasamehe madhambi ya marehemu na kuwapa pepo, sasa kwa namna hiyo inakuwa tabu sana.

    Nyinyi wabunge, majimboni mwenu kuna matatizo mengi ya kushughulikia lakini mnayafumbia macho, haya mambo yasiyo na msingi ndio mnayashikia bango ili kujitafutia ujiko acheni hizo.
    hicho mnachokifanya ni RIHA na Mwenyezi Mungu hampendi mtu mwenye kufanya riha.

    ReplyDelete
  4. Huo ni mtaji kwa CCM wameishiwa sera.

    ReplyDelete