Pages

Saturday, January 29, 2011

YANGA vs DEDEBIT HAKUNA MBABE

 Mechi kati ya Yanga na Dedebit sports ikiendelea
 Mashabiki waliojitokeza katila Mpambano huo

 Kipa wa Yanga akipata huduma ya kwanza baada ya kuumia

 Mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Mpira wilaya Temeke Said Akida

 Dedebit wakishangilia goli la nne
 Filimbi ya mwisho kupulizwa

 Kocha Msaidizi wa Yanga Salvatory Edward

Mashabili wakitoka nje baada ya mchezo kwisha hadi mwisho Yanga 4 - Dedebit 4

Tuesday, January 25, 2011

ABOBAINI YA AMINI AKIDA

Marehemu  Amin Akida
Familia ya Akida wa Temeke inapenda kutoa shukrani kwa wote walioweza kuwa pamoja toka mwanzo wa msiba mpaka Arobaini ya ndugu yao mpendwa.Hawana cha kuwalipa zaidi ya kumuomba Mola awazidishie Imani na Upendo na kuwatilia wepesi kwa Yote mnayofanya.
SHUKRANI ZA DHATI 

 kisomo cha kumrehemu kikiendelea

 Baadhi ya watu waliohudhuria katika kisomo

 Saidy Akida kaka wa marehemu akijaribu kuweka sawa mambo
 wahudhuriaji wakijiandaa kupata sadaka


 Wakinamama nao wakipata sadaka

wasimamizi wakuu wa shughuli wakiwa katika picha ya pamoja

Sunday, January 23, 2011

MASHINDANO YA RBA UWANJA WA NDANI WA TAIFA

 Michael na Aman Temba wakijiandaa

 Kiraka Aman Temba akipasha mwili moto
 Furaha

 Kisoky Juma akifanya maandalizi kabla ya mchezo


 CHANG BOYZ

 Mohammed Mbwana msimamizi wa mazoezi
 ABC guard

 Shabiki No.1 



Washabiki wa ABC wakishangilia baada ya mechi kwisha
                                         Game imeisha na Changombe Boys 58 na ABC 76

Monday, January 17, 2011

TOBOA TOBO aka KITOBO

 Toboa Tobo akiendelea kuonyesha ufundi wake
 Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo

 hapa kuna kitu alikifukua ndio kikawa kinachomwa moto amesema ni chuma ulete watu wa nyumba hiyo walikuwa wakiweka pesa zao hazikai

 kitu alichokikamata ndio hicho alichosema ni chuma ulete

ANAITWA Husein Zayumba Toboa Tobo aka Kitobo ni mganga wa jadi Mitaa ya Temeke, Eneo la Tandika huyu jamaa sera zake sawa na manyaunyau anachinja paka na ile damu ya paka anakunywa navyosikia kazi yake kubwa wanavyosema ni kutoa misukule, kuvumbua wachawi na nini sijui nilikutana nae mitaa ya Temeke Wailes mtaa wa mkumba aliitwa kutoa msukule lakini mpaka naondoka hakuna kilichoendelea na anasema yy ndio aliyemfundisha manyaunyau ila yeye tu hafahamiki kwa wenye imani nae haya Bingwa huyo wa kuvumbua wachawi

Saturday, January 8, 2011

CHANG`OMBE BOYS WAJIANDAA NA RBA (CHANG BOYZ)

 Timu ya Mpira wa kikapu ya chan`ombe wakiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na ligi ya RBA kwenye viwanja vya TCC club Chang`ombe


 Furaha chang boyz
 Barnabas na Maiko
 Bigggggg Martin


INGAWA Chang'ombe Boys ni timu iliyoundwa na vijana waliokuwa mashabiki na wapenzi wakubwa wa mpira wa kikapu mjini Dar es Salaam, lakini sasa ina wataalamu wa kutosha kama Adam Jegame, Mohamed Mbwana, Furaha,Maiko nk .

Kuundwa kwa timu hiyo kulitokana na mkusanyiko wa vijana mbalimbali kutoka katika mitaa ya wilaya ya Temeke mwaka 1980 na kuweka kambi yao kwenye klabu ya Sigara, Chang'ombe ambako hadi leo wanapatikana.

Wao pekee, ingewawia vigumu kuisimamisha Chang'ombe Boys, hivyo walihitaji msaada kutoka kwa watu au kampuni zilizokuwa na uwezo hata Mamlaka ya Bandari Tanzania
(THA), ikawa ya kwanza kujitokeza kuisaidia.

Lakini kutokana na uwezo mdogo, Chang'ombe kusimama imara, ilichechemea kwa muongo mmoja kuweza kupata mafanikio.

Mwaka 1990 ndipo timu hiyo ilipofanikiwa kupanda hadi Daraja la Kwanza na kupata tiketi ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika michuano ya kuwania klabu bingwa
ya Tanzania.

Hata hivyo, Chang'ombe Boyz, ilishindwa kutamba katika michuano hiyo kutokana na uchanga wake.

Ikiwa chini ya kocha wake, marehemu Raymond Ndanshau, Chang'ombe Boyz ilijitutumua na kufanikiwa kushiriki katika michuano ya Super Cup kwa mara ya kwanza mwaka 1997, baada ya kupitishwa kwa uamuzi wa kuongeza timu kutoka nne hadi sita. Timu nyingine iliyoongeza pamoja na Chang'ombe Boyz ilikuwa ni Oilers.

Mwaka uliofuata timu hiyo ilifanikiwa kuingia tena katika michuano hiyo baada ya kushika nafasi ya tano. Mwaka 1999 ilishindwa kupata tiketi ya kushiriki michuano hiyo, lakini tokea hapo imekuwa mshiriki wa kudumu.

Vijana hao wa Chang'ombe wameendeleza jadi yao ya kuwa na mapenzi ya dhati katika mchezo huo, kwani pamoja na kutotwaa taji lolote kubwa wamekuwa wakijiimarisha na kutoa ushindani mkubwa dhidi ya timu kubwa.

Chang'ombe Boys msimu huu nayo imeweza kunyanyua wachezaji , ili kuimarisha kikosi chake.

Kama ni Mwana Temeke na Mpenzi Wa Mpira Kikapu ipe Nguvu Chang`ombe Boyz waweze kufanya vizuri katka ligi hii

Jumapili ya tarehe 9/01/2011 chang`ombe Boyz vs Chui uwanja wa ndani wa Taifa mechi inaanza saa 5.00 Asubuhi

Saturday, January 1, 2011

MECHI YA KUAGA MWAKA 2010 TEMEKE VETERAN vs TEMEKE SQUAD

 Kocha wa Kagera Sugar Mlage Kabange alikuwepo
 David Beatus mwenye kofia na shilton
Kanakamfumu na Peter Mkwera
 Temeke Veteran Wakiwa katika Picha ya pamoja
 Picha ya Pamoja Temeke Veteran na Temeke Squad
 Mish Digital Production Said Bungara mwenye flana nyeupe

katika mechi hiyo ya kuaga mwaka 2010 na kukaribisha mwaka 2011 Temeke veteran iliweza kuwafunga Temeke Squad kwa jumla ya goli 3-2 mechi iliyochezwa katika uwanja wa tmk squad mechi hiyo dhumuni ilikuwa ni kijaribu kuwahamasisha vijana katika kuupenda mpira na kuwapa changamoto mbalimbali zinazotokea katika mpira wa sasa