Pages

Saturday, January 8, 2011

CHANG`OMBE BOYS WAJIANDAA NA RBA (CHANG BOYZ)

 Timu ya Mpira wa kikapu ya chan`ombe wakiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na ligi ya RBA kwenye viwanja vya TCC club Chang`ombe


 Furaha chang boyz
 Barnabas na Maiko
 Bigggggg Martin


INGAWA Chang'ombe Boys ni timu iliyoundwa na vijana waliokuwa mashabiki na wapenzi wakubwa wa mpira wa kikapu mjini Dar es Salaam, lakini sasa ina wataalamu wa kutosha kama Adam Jegame, Mohamed Mbwana, Furaha,Maiko nk .

Kuundwa kwa timu hiyo kulitokana na mkusanyiko wa vijana mbalimbali kutoka katika mitaa ya wilaya ya Temeke mwaka 1980 na kuweka kambi yao kwenye klabu ya Sigara, Chang'ombe ambako hadi leo wanapatikana.

Wao pekee, ingewawia vigumu kuisimamisha Chang'ombe Boys, hivyo walihitaji msaada kutoka kwa watu au kampuni zilizokuwa na uwezo hata Mamlaka ya Bandari Tanzania
(THA), ikawa ya kwanza kujitokeza kuisaidia.

Lakini kutokana na uwezo mdogo, Chang'ombe kusimama imara, ilichechemea kwa muongo mmoja kuweza kupata mafanikio.

Mwaka 1990 ndipo timu hiyo ilipofanikiwa kupanda hadi Daraja la Kwanza na kupata tiketi ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika michuano ya kuwania klabu bingwa
ya Tanzania.

Hata hivyo, Chang'ombe Boyz, ilishindwa kutamba katika michuano hiyo kutokana na uchanga wake.

Ikiwa chini ya kocha wake, marehemu Raymond Ndanshau, Chang'ombe Boyz ilijitutumua na kufanikiwa kushiriki katika michuano ya Super Cup kwa mara ya kwanza mwaka 1997, baada ya kupitishwa kwa uamuzi wa kuongeza timu kutoka nne hadi sita. Timu nyingine iliyoongeza pamoja na Chang'ombe Boyz ilikuwa ni Oilers.

Mwaka uliofuata timu hiyo ilifanikiwa kuingia tena katika michuano hiyo baada ya kushika nafasi ya tano. Mwaka 1999 ilishindwa kupata tiketi ya kushiriki michuano hiyo, lakini tokea hapo imekuwa mshiriki wa kudumu.

Vijana hao wa Chang'ombe wameendeleza jadi yao ya kuwa na mapenzi ya dhati katika mchezo huo, kwani pamoja na kutotwaa taji lolote kubwa wamekuwa wakijiimarisha na kutoa ushindani mkubwa dhidi ya timu kubwa.

Chang'ombe Boys msimu huu nayo imeweza kunyanyua wachezaji , ili kuimarisha kikosi chake.

Kama ni Mwana Temeke na Mpenzi Wa Mpira Kikapu ipe Nguvu Chang`ombe Boyz waweze kufanya vizuri katka ligi hii

Jumapili ya tarehe 9/01/2011 chang`ombe Boyz vs Chui uwanja wa ndani wa Taifa mechi inaanza saa 5.00 Asubuhi

No comments:

Post a Comment