Pages

Monday, March 9, 2015

Watu saba wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukata kiganja cha Albino

 Jeshi la polisi mkoani rukwa linawashikilia watu saba hadi sasa, kwa tuhuma za kuhusika na kitendo cha kikatili cha kukata kiganja cha mkono wa kulia, cha mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Baraka Cosmas Lusambo mwenye umri wa miaka sita, katika kitongoji cha kikonde kata ya kipeta wilaya ya sumbawanga vijijini, ambapo pia katika tukio hilo wamemjeruhi mtoto huyo mkono wa kushoto.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa rukwa kamishna msaidizi wa polisi Leons Rwegasira, amesema wamefanikiwa kuwakamata watu hao kufuatia msako mkali, mara tu baada ya kutokea tukio hilo kwenye kitongoji hicho cha kikonde, ambacho kinakuwa na wakazi wakati wa msimu wa kilimo na kiangazi watu wanahama tena, katika familia yenye watoto wengine watatu wenye ulemavu wa ngozi. 
 
ACP.Rwegasira pia amesema kwenye msako huo mkali, wamefanikiwa kuwakamata watu wanane wanaojihusisha na uganga wa jadi na upigaji wa ramli chonganishi, ambacho ni chanzo kikubwa cha kusababisha vifo na kujeruhiwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikina. 
 
Mtoto baraka na mama yake mzazi wamelazwa kwenye hospitali ya rufaa ya jijini mbeya, wakitibiwa majeraha waliyoyapata wakati wa purukushani za kumshambuliwa mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment