Pages

Wednesday, June 4, 2014

WAUE-YA MH. TEMBA NA CHEGE YAKAMILIKA

 Baadhi ya vipande vya videovitakavyokuwepo katika nyimbo hiyo



Wanamuziki wa kizazi kipya wanaotoka kundi la TMK Wanaume Family, Chegge na Mhe Temba wanatarajia kuachia hewani wimbo wao mpya uitwao 'Waue' waliowashirikisha 'membaz' wa Mkubwa wa Wanawe.
Wasanii walioshirikishwa  ni Maromboso na YP ambao nao wanatokea 'ukoo' wa TMK Wanaume Family na Mkubwa na Wanae.
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe na Meneja wa wasanii hao, Said Fella 'Mkubwa' alisema  kuwa, wimbo huo utaachiwa 'audio' na video  muda wowote kuanzia sasa kwa kuwa kila kitu kipo tayari.
Mkubwa, alisema wimbo huo umerekodiwa katika studio zao za Mkubwa na Wanae chini na mtayarishaji, Shirko na video imefanywa na Adam Juma kupitia kampuni yake ya Visual Lab.
"Wasanii Temba na Chegge wamekamilisha kurekodi 'audio' na video ya wimbo wao uitwao 'Waue' walioimba na Maromboso na YP, na tunapanga kuachia kazi hiyo mda wowote," alisema.
Chegge na Mhe Temba wamekuwa wakitoa kazi za pamoja mbali na zile za binafsi za kila mmoja nje ya nyimbo za kundi lao la TMK Wanaume Family.

No comments:

Post a Comment