Pages

Wednesday, June 4, 2014

MAJANGA DEREVA NA UTINGO WAJIIBIA MALI WALIZOKUWA WAKISAFIRISHA

                                                                                           

Kamanda  wa polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi kushoto akisalimiana na mwakilishi wa kampuni ya Dandu ambao lori lao limeteketezwa kwa moto.

(Francisblog)(FS)

Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa akionyesha mitumba  iliyohifadhiwa katika nyumba  moja Nyololo baada ya kufaulishwa na dereva na utingo wake kisha lori kuchoma moto.(Francisblog)(FS)

Mitumba  hiyo ikionekana kwa nje baada ya kujaa ndani ya nyumba hiyo kupita kiasi 

Safari ya kwenda  kubaini mali ya wizi iliyofanywa na kamanda wa polisi Iringa
 
RPC Iringa Ramadhan Mungi akiangalia  mitumba  iliyohifadhiwa porini baada ya  kuporwa 



Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akitoka  kushuhudia mabelo ya mitumba yaliyofichwa  porini kijiji cha Maguhani Mufindi 

kamanda wa  polisi Iringa Ramadhan Mungi akimwonyesha mmiliki wa nyumba iliyohifadhi  mali  hizo za wizi kulia na dereva wa gari hilo mbele lenye namba  T 185 CJM ambalo  ndilo lilikuwa likisomba mali  hizo za wizi kutoka katika  lori lililochomwa moto
 
Watuhumiwa wa  wizi wa mali  zilizokuwa  zikisafirishwa na lori la kampuni ya Dandu
 
Hili ndilo lori  lililokuwa na mali  hizo  chini kukiwa na ubichi wa mafuta  ya taa yaliyomwagwa ili  kulilipua lori hilo bila mafanikio

mwonekano wa lori hilo kwa ndani baada ya mali zote  kuhamishwa kwa  lengo la kuziiba 

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akionyesha  lori hilo mali ya kampuni ya Dandu ambalo limechomwa moto na dereva na utingo wake baada ya  kufaulisha mali zote kwa lengo la kuiba
 
Picha: Fransic blog 
 

No comments:

Post a Comment