Pages

Thursday, November 20, 2014

IPTL YAFIKIA PATAMU


Na Ojuku Abraham

MOTO wa ripoti ya upotevu wa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo imekabidhiwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe unatarajiwa kuwaka Novemba 27, mwaka huu, siku ambayo itasomwa na kujadiliwa bungeni baada ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na vigogo wengine kadhaa kuhojiwa.
Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilichotwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 300 katika hali isiyofahamika na wabunge wanataka ripoti hiyo iliyokabidhiwa kwa Kamati na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za…
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Na Ojuku Abraham
MOTO wa ripoti ya upotevu wa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo imekabidhiwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe unatarajiwa kuwaka Novemba 27, mwaka huu, siku ambayo itasomwa na kujadiliwa bungeni baada ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na vigogo wengine kadhaa kuhojiwa.
Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilichotwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 300 katika hali isiyofahamika na wabunge wanataka ripoti hiyo iliyokabidhiwa kwa Kamati na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, iwahoji wahusika wote kabla ya kuileta bungeni kwa mjadala.
Serikali kupitia kwa mwanasheria mkuu wake, Jaji Fredrick Werema na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, sambamba na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi wamekuwa wakisisitiza kuwa fedha hizo zilitolewa kwa kuzingatia hukumu ya Mahakama Kuu na kwamba haikuwa ya umma isipokuwa ni ya kampuni hiyo ya kufua umeme ya PAP.
“Katika hili, wabunge nao wamegawanyika, wapo wanaotetea madudu haya na wengine hawataki kabisa mchezo. Pale mwanzo ilionekana kama ni ajenda ya wapinzani, lakini kadiri siku zinavyokwenda, hata wabunge ndani ya chama tawala nao wanaonekana hawataki mchezo. Watu wamepania sana na huenda kukawa na mshikemshike mkubwa siku hiyo,” alisema mbunge mmoja wa CCM aliyekataa jina lake kutajwa.
“Inapofikia wakati wa kushughulikia wizi mkubwa kama huu, hatuna budi kuweka masilahi ya taifa mbele, hatuwezi kukubali fedha nyingi kama hizi zinaibwa wakati wananchi wanashindwa kupata mahitaji yao ya msingi kwa sababu ya ukosefu wa fedha, tunataka wote waliohusika katika jambo hili wawajibishwe na hatua zaidi za kisheria zichukuliwe,” alisema.
Kwa mara ya kwanza, skendo hiyo ya fedha iliibuliwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, akisema ana uthibitisho kwamba fedha hizo zilikwapuliwa na wajanja wachache, baada ya kuitafsiri kimakosa hukumu ya Mahakama Kuu chini ya Jaji John Utamwa, kwani hakuna popote ilipotaja Akaunti ya Escrow, akidai ingawa katika kikao kati ya Tanesco, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini walisema fedha zote za akaunti hiyo zipewe Kampuni ya PAP.
Vigogo wa serikali wanaotajwa kuhusika katika kashfa hiyo ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wake Eliakim Maswi, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu, Beno Ndullu, Mwanasheria Mkuu Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba.

No comments:

Post a Comment