Pages

Thursday, October 10, 2013

ASASI ZA KIJAMII ZA TEMEKE ZAASWA

Waandishi wa ripoti kutoka asasi zinazofanya kazi ya kupambana na vvu manispaa ya temeke wakiwa katika mkutano wa robo ya tatu ya mwaka huu
Afisa maendeleo ya jamii wa manispaa ya temeke ndugu John Bwana amezitaka asasi zinazojihusisha na mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi katika jamii ndani ya manispaa ya Temeke kuwasilisha ripoti zao za kila robo katika mwaka katika vyombo husika serikalini.
Akizungumza na waandishi wa ripoti wa asasi zaidi ya sitini katika ukumbi wa mikutano wa shule ya msingi wailesi waiofika katika mkutano huo wa robo ya tatu katika mwaka huu wa 2013 ndugu Bwana alisema " njia nzuri ya kujenga mahusiano na mawasiliano mazuri baina ya asasi na serikali ni ni kwa njia ya asasi kulazimika kuwasilisha ripoti za kazi zao serikalini kwani ripoti hizo zitaisaidia serikali kujua asasi gani inafanya kazi, kwa ukubwa upi na ina changamoto zipi zinazoikabili na isitoshe sisi serikali tunaweza kuandaa mipango yetu ya kiutekelezaji kulingana na taarifa tunazoletewa na inatusaidia pia kutambua ukubwa wa tatizo au kupungua kwa tatizo pia itatusaidia kutambua asasi za kiuzipa kipaumbele kwa kushirikiana nazo".
Wakati huohuo asasi hizo katika kuchangia majadiliano kwenye mkutano huo zimeeleza mafanikio katika kupambana na hali ya maambukizi ya vvu, kwani wameweza kuwafikia watu wengi katika jamii kwa kuwapatia elimu ya kutokupata maambukizi ya vvu kwa kutoendelea kufanya ngono zembe na kwa wale wanaofanya biashara ya kuuza miili yao wamepatiwa elimu ya ujasiliamali na kuanzishiwa huduma ya vikoba ili waweze kujiajili kwa ajira iliyosalama kwa afya zao.
Katika ripoti zote zilizowasilishwa na asasi ripoti ya asasi inayojulikana kwa jina la STAY AWARE NETORK (SANA) yenye makao makuu yake sinza na inajihusisha na uzuiaji wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kundi lililosahaulika la watu wanaofanya mapenzi wenye jinsi moja inayofanana ndio iliyoleta msisimko mkubwa kwa wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
Asasi hiyo ilikumbusha jamii kuwa wwakati jamii inaweka vipaumbele vya mapambano ya vvu inawasahau kundi ilo ambalo lipo kwenye jamii na limegawanyika katika sehemu tatu kundi la kwanza ni la wanaume wanaopenda wanaume wenzao kwa kuwageuza wake zao, kundi la pili ni la wanaume wanaopenda kugeuzana wanawake kwa kufanya panzi kwa kugeuzana na kundi la tau ni la wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao huku wakifanya mapeni na wanawake kwa njia iliyokubalika.
Mtaalamu huyo alielezea maambukizi ya vvu utokea kutokana na michubuko inayotokea kutokana na njia hiyo inayotumika kutokuwa lengwa kwa kazi hiyo ya kujamiiana na usababisha maambukizi kutokea na kusambaa kwa njia ya mtandao wa ngono zembe.
Na alimaliza kwa kusema hata wanawake wanaosagana pia upata maabukizi kwa urahisi kwani hakuna kinga inayowazuia wasiambukazane vvu wakati wa tendo ilo la ngono kwa njia ya kusagana
by: Denis Chakoma.