Pages

Wednesday, July 22, 2015

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA INTERN.AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN ,JUMAMOSI 25 JULAI 2015


FFU-Ughaibuni Jino kwa Jino na Washabiki wa Tubingen Jumamosi 25,07.2017


Tübingen,Ujerumani

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani,inatarajiwa kutingisha jukwaa la
maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni barani ulaya 6th International African Festival in Tübingen, Ujerumani, bendi hiyo maarufu inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja  itapanda jukwaani siku ya Jumamosi 27 Julai 2015 majira saa 2.00 Usiku katika
uwanja wa Festplatz,Europa str,mjini Tübingen ,uliopo Ujerumani ya Kusini. 
Kikosi kazi hiko cha Ngoma Africa Band ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki au FFU,chenye utajiri wa wanamuziki vijana waliojaa vipaji, bendi inasadikiwa kuwanasa
washabiki kila kona duniani kutokana na mdundo wake"Bongo Dansi" made in Uswahilini. bendi hiyo kwa sasa inatamba na CD mpya ya " La Mgambo" yenye nyimbo mbili za kumuaga rais JK.
Usikose kuwasikiliza at www.reverbnation.com/


No comments:

Post a Comment