Pages

Tuesday, May 19, 2015

NASH MC NA MIAKA 16 YA JUMA NATURE

Hiki ndio alichokisema msanii wa hiphop nchini Nash Mc katika kuelekea miaka 16 ya Juma Nature
Nawapongeza E.FM 93.7 kwa kuandaa Tamasha la miaka 16 katika game ya Sir Juma Nature, hakuna asietambua mchango wa Juma katika kuifikisha sanaa yetu hapa ilipo ukiacha nyota aliyokua nayo ya kupendwa na watanzania wengi, Ni jambo zuri sana na la kuigwa na Media zingine nchini, maana wengi husubiri wasanii wafe watumie mwanya huo kujipatia kipato kwa kuandaa matamasha ya kumkumbuka Hayati huyo,kama ilivyokua kwa Hayati Albert Mangwear, E.FM wamefanya kitu ambacho Alipaswa kufanyiwa Sir Juma Nature muda tu lakini si haba natumai litakua tamasha zuri na kubwa ntajitahidi niwepo siku hiyo kwa kua itakua nyumbani Temeke basi mzukaaaa.
16 Ya Sir Juma Nature katika Game.

No comments:

Post a Comment