Pages

Saturday, June 18, 2011

Frederick Chiluba amefariki

Rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba, amefariki, akiwa na umri wa miaka 68.
Bwana Chiluba amekuwa na ugonjwa moyo kwa miaka kadha.
Rais Frederick Chiluba na nmkewe Regina mjini LUsaka

Rais Chiluba aliiongoza Zambia kwa mwongo mzima katika miaka ya '90, na baada ya kustaafu alishtakiwa kwa sababu ya rushwa.
Frederick Chiluba alipata urais wa Zambia mwaka wa 1991, wakati Afrika inaanza kuingiia katika demokrasi ya vyama vingi.
Kabla ya hapo alikuwa kiongozi wa wafanyakazi.
Aliahidi kuleta mabadiliko lakini alipochukua uongozi Zambia ilikuwa imeshafilisika, naye aliacha rushwa kustawi.
Alipojaribu kujiongezea muhula wa tatu wa madaraka, alipingwa.
Piya alilaumiwa kuwa akipenda maisha ya anasa.
Baada ya kuondoka madarakani mwaka wa 2001, mrithi wake, Levy Mwanawasa, alimshtaki kwa shutuma za rushwa.
Baada ya kesi ya miaka 6 kuhusu ubadhirifu wa mali ya taifa, Frederick Chiluba aliambiwa hakuwa na makosa. .
Lakini katika kesi nyengine iliyofanywa katika mahakama makuu ya London, Chiluba alikutikana na hatia ya kuiba mamilioni ya dola ya fedha za serikali ya Zambia, kwa kutumia akaunti kwenye mabenki ya London.

No comments:

Post a Comment