Kenya imetangaza bajeti inayolenga kukabiliana na ongezeko la gharama ya maisha na kudhibiti bei ya bidhaa nchini humo.
Waziri wa fedha Uhuru Kenyatta katika taarifa yake ya makadirio ya matumizi ya mwaka 2011/2012 amesema serikali itaondoa ushuru wa mafutaa ya taa.
Serikali ya pia imetangaza hatua ya kuwaondolea waagizaji mahindi na ngano ushuru . Hii ina lengo la kukabiliana na upungufu unga wa mahindi na ngano nchini Kenya uliosababishwa na mazao duni kutokana na ukame
Hata hivyo bei ya sigara na pombe inatarajiwa kupanda kwani ushuru wake umeongezwa.
Katika kuwasaidia akina mama wajawazito wanaoishi mashambani ili waweze kufika hospitalini kwa wasaa ,ushuru kwa wanaotaka kuagiza magari ya wagonjwa na pikipiki umeondolewa.
Serikali ya Kenya pia imetenga pesa zaidi za kununua dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ili watu wanaoishi na virusi hivyo waweze kunufaika.
Uganda
Pia kueleza pato la serikali, kupitia kodi mbalimbali, litazidi shilingi trilioni 9 au karibu dola za kimarekani bilioni 2.5 (kama asilimia 66 ya bajeti; na wafadhali wanatarajiwa kuchangia zaidi ya asilimia 24 ya bajeti au karibu dola za kimarekani milioni 580 kwa mwaka huu wa fedha.
Lakini wakati huo huo Uganda ina deni linalozidi dola za kimarekani bilioni nne.
Licha ya zao ghafi la ndani (GDP) - yaani thamani ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa nchini zinatarajiwa kukua kidogo hadi asilimia sita kwa mwaka huu wa fedha.
Waziri wa fedha Maria Kiwanuka anakabiliwa na changamoto kali kutokana na hali hasi ya uchumi, shauri ya shilingi dhaifu kulinganisha na sarafu ngumu kama dola ya Marekani na Euro, pato linaloanguka la nchi.
Wakati huo huo mfumko wa bei unaofikia asilimia 16, wa juu kabisa kwa miaka 17 tangu mwaka 1994.
Sasa uchaguzi ukipigwa kisogo, wizara ya fedha huenda ikahisi iko huru kupandisha ushuru na kodi ili kupata pesa za kugharimia matumizi yake.
Watumizi wakubwa ni wizara za miundo mbinu, kama nishati, elimu na ujenzi - kila moja yaahidiwa zaidi ya dola za kimarekani milioni 320m.
Ukilinganisha, wizara ya afya inapangiwa kasoro ya dola za kimarekani milioni 174; ilihali kilimo kwa muda mrefu ambao ni uti wa mgongo wa uchumi wa Uganda, kinapangiwa kama dola za kimarekani milioni 96.
Licha ya maneno mengi ya kisasa, wizara ya ICT - Teknolojia ya Kompyuta na Maelezo - inatarajia kupata ziada kidogo ya dola za kimarekani milioni tatu.
Hata hivyo, matumizi hayo yanaambatana na ahadi za uchaguzi za chama tawala NRM kuielekeza Uganda kuwa nchi ya pato la wastani, kupitia uzalishaji wa viwanda na kilimo cha kisasa, kufika mwaka 2030.
Na waziri mpya wa fedha atatazamia kipato cha mafuta, kwa sasa cha ndo, ndo, ndo, zaidi ya dola za kimarekani milioni 223 kumsaidia mwaka huu wa fedha.
Tanzania yabana fedha za umma
Aidha imetangaza pia kupunguza safari za nje na ndani za viongozi ikiwa ni pamoja na ukubwa wa misafara ya viongozi hao.
Serikali ya nchi hiyo imeapanga kutumia shilingi za nchi hiyo trilioni 13.525 sawa na wastani wa dola za kimarekani bilioni 10.
Pia imetangaza kusitisha kununua samani za ofisi za serikali kutoka nje ambazo zinaweza kutengenezwa nchini humo.
Mambo mengine yaliyojitokeza katika bajeti hiyo ni unafuu kwa wakulima wa nchi hiyo ambao wamefutiwa kodi ya ongezeko la thamani pale watakapokuwa wakinunua zana za kilimo.
Hata hivyo, pamoja na unafuu huo kilimo ipo nafasi ya nne kwa mujibu wa fedha zilizotengwa kisekta katika bajeti hiyo ambapo imetengewa shilingi billioni 926 sawa na wastani wa dola milioni 450.
Mwandishi wetu aliyopo Dodoma, John Solombi amesema sekta nyingine kama ya miundombinu imetengewa shilingi trilioni 2.8 sawa na dola za kimarekani bilioni 1.5.
Wengine wanaoguswa katika bajeti hiyo ni mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo kuanzia sasa wataanza kulipa kodi ya ongezeko la thamani isipokuwa mashirika ya kidini ambayo yataendelea kupata msamaha wa kodi.
Wafanyabiashara ndogo ndogo nao hawajaachwa katika bajeti hiyo kwani nao watatakiwa kulipa ada ya leseni pale watakapokata leseni za biashara zao.
Kwa wale waliopo mjini watalipa ada ya leseni ya shilingi 50,000 sawa na dola 50 kwa mwaka.
Bajeti hii bado haijaonekana kuwa na maeneo mapya ya vyanzo vya mapato kwani bado inaonekana kutegemea vyanzo vile vile vya mapato hasa kwenye ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji na sigara na kodi zilizokuwepo zamani.
Katika kupunguza ongezeko la bei ya mafuta ya petroli serikali ya nchi hiyo imesema itaangalia uwezekano wa kupunguza tozo kwenye bidhaa hiyo ambayo imechangia kuongeza kwa mfumuko wa bei nchini humo. BBC
No comments:
Post a Comment