Pages

Friday, July 8, 2011

White House’ ya Sudan-Jumba la Kutisha


Jumba la 'white house' kumbukumbu ya mateso Sudan Kusini

Ngazi zilizo wima zinateremka kuelekea chini na katika giza totoro, hewa ni nzito, ina kama moshi hivi na kuna joto katika eneo hili ambalo punde itakuwa Sudan Kusini iliyoo huru.
Kuna pingu zinaning’inia kwenye mhimili wa chuma kwenye dari nyeusi. Kumbukumbu ya ukatili na mateso yaliyowahi kutokea hapa.
Kwa Sudan Kusini, ambyo tayari inajitahidi kumaliza ghasia, eneo hili linatoa onyo kali kwamba siku za usoni hazitakiwi kuwa kama zilizopita.
"Ni Taifa litakalokuwa jumuishi?" aliuliza Jok Madut Jok, Profesa wa taaluma na historia katika Chuo Kikuu cha Loyola Marymount, California, alipozungumza katika mhadhara wa karibuni.
"Au litakuwa halina msimamo kama nchi nyingine zimetumbukia-kwamba unapata uhuru , halafu unaendelea kufanya yale yale uliyoyapinga?" alisema Bw Jok, ambaye pia ni afisa mwandamizi katika
Wizara ya Utamaduni.
Kwa mujibu wa Mwandishi wa BBC Peter Martell, kuna maeneo machache katika mji mkuu wa Sudani Kusini Juba ambayo yanaibua hofu kama jengo lijulikanalo kama "White House".
Wakati wa vita ya Sudan 1983-2005 lilipata umaarufu kama eneo kuu la Kusini la kutesea na kunyongea la serikali ya Khartoum, kwa wale iliyoamini kuwa ni vikosi vya waasi.
Kuta zenye grisi na masizi pamoja na maganda ya risasi yenye kutu yalitapakaa sakafuni.
Balbu yenye mwanga hafifu ikitoa mwanga mdogo kwenye kona za giza kwenye chumba hicho.
"Nina wasiwasi kama waandishi wengine wamewahi kufika hapa," afisa usalama wa serikali alisema kwa kunong’ona.
"Kama waliwahi, basi hawakutoka wakiwa hai," mwenzake aliitikia.
Inakadiriwa kuwa watu 1.5 milioni walikufa katika vita, mgogoro uliotokana na imani, ukabila, udini, maliasili na mafuta.
Waasi wa Sudan Kusini walipigana dhidi ya kile walichokiita kutengwa na kujilundikia madaraka kwa serikali iliyojaa wasomi ya Kaskazini.

'Kuongezeka kwa ukatili'
Sasa wapiganaji hao wamekuwa jeshi rasmi la Kusini, ambayo itakuwa Taifa lililojitenga Julai 9, likiigawa katika mataifa mawili nchi yenye eneo kubwa kuliko yote Afrika.
Wananchi Sudan Kusini kuelekea uhuru kamili
Lakini jengo kama ‘White House’ halibebi kumbukumbu mbaya za Sudan iliyopita iliyokuwa imejaa damu.
Watu wanasema wanatoa ujumbe wa siku zijazo. Kwamba utawala uliotumia mateso dhidi ya watu wake wenyewe katika Sudan iliyokuwa moja ni lazima iwe historia na kwa namna yoyote isibebwe katika Sudan Kusini mpya iliyojitenga.
"Eneo hilo lilikuwa ni jinamizi kwetu-ukisikia mtu amepelekwa huko, utakuwa tayari umeshaagana nao, hawakuwa wanarudi," alisema mwanafunzi wa chuo Mabil William.
“Ingefaa paitwe 'Red House' kwa sababu ya damu na sio “White House” alisema askari wa SPLA.
Baba yake hakuonekana tena baada ya kukamatwa vitani, inaaminika kuwa alikufa huko ‘White House’
"Tulipopiga kura kwa ajili ya kujitenga, kusema kwa heri kwa Khartoum, maeneo kama hayo tunayapungia mkono wa kwa heri."
Lakini wakati matumaini ya mabadiliko ni makubwa, changamoto ni nyingi.
Chama cha Kusini cha Sudan People's Liberation Army (SPLA) hakijawa na rekodi kamili.
Kuhama kutoka chama cha waasi na kuingia kuwa jeshi la kawaida kumezusha tuhuma za mauaji na ubakaji, kwa mujibu wa makundi ya kutetea haki za binadamu
"Taarifa za uporaji, unyanyasaji kwa raia na hata mauaji vimesababisha kuwa na wasiwasi mkubwa" sehemu ya taarifa ya pamoja ya makundi ya Kimataifa na ya Sudan kuhusu haki za binadamu ilisema.
Taarifa hiyo ilionya juu ya "kuongezeka kwa ukatili wa serikali" Kusini, huku pesa na mamlaka vikilundikwa Juba, na usalama ukichukua sehemu kubwa ya bajeti.
Chama cha SPLA kimekuwa kikipambana na takribani vikundi vya wapiganaji vipatavyo saba kwa mwaka. UN inasema pande zote mbili zilikuwa zikilenga raia.
Zaidi ya watu 1,800 wameuawa mwaka huu Sudan Kusini na wengine 264,000 kwa mujibu wa makisio ya UN.
Serikali ya Kusini imerejea kusisitiza kuwa inafanya kazi kwa manufaa ya siku za usoni, na inasema wakati makosa tayari yameshafanyika, mabadiliko kutoka vita vya msituni hadi serikali si kitu rahisi.
"Sudan Kusini itaheshimu haki za watu wote wanaoishi katika milki yake wawe wa kutoka mchanganyiko wa makabila , utamaduni, lugha dini na asili " ilisema taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa sasa kabla ya kutangazwa uhuru ikiahidi kuzingatia tamko la Haki za msingi za Binadamu.
Uwanja wa Makaburi
Chumba cha mateso

Baada ya sherehe za furaha za uhuru kumalizika, kazi kubwa ya siku za usoni itakuwa ni kuhakikisha ahadi zinalinda haki kwa ujasiri, kuwa na vyombo vya habari na jamii iliyo tayari.
Vikosi vya kaskazini vimeacha chumba hicho cha ‘White House,’ lakini eneo la jirani bado ni kambi hai ya kijeshi kwa sasa ikiendeshwa SPLA.
Jengo halisi lililotoa jina gumu ni mwendo mfupi kutoka kwenye handaki: Wafungwa walikuwa wakiburutwa nje ya eneo hilo wakienda kunyongwa, alisema askari.
Jengo la kawaida, lililopakwa rangi nyeupe sasa linatumika kama duka na bweni
Meja Jenerali Marial Chanoung, kamanda anayesimamia kambi ya jeshi anasema hakuna anayeweza kueleza wasudani maelfu mangapi waliokufa hapa.
"Kulikuwa na mateso. Ni sehemu iliyojulikana kuua watu wengi,” alisema.
Karibu na jengo kuna kifusi cha majani ya kijani, alama ya fuvu jekundu na mifupa miwili ikionyesha kuna bomu ambalo halijalipuka.
Askari wanasema wakati wa kiangazi mifupa ilikuwa ikionekana nje ya kaburi la pamoja.
SUDAN: Ni nchi mbili sasa

No comments:

Post a Comment