Pages

Sunday, July 10, 2011

NI YANGA

 wapenzi wakiwa nje ya uwanja kabla ya kuingia ndani kushuhudia fainal ya Kagame Cup kati Simba SC vs Yanga
 Mashabiki wakiingia uwanjani

 Yanga wakipasha miili yao moto kabla ya pambano

 Simba  wakifanya mazoezi myepesi

Huu ujumbe ulikuwa unasema simba ni Bingwa

Mashabiki wa yanga waliojitokeza

kipa wa Yanga Berko akidaka moja ya hatari katika gori lake

Mashabiki wa simba waliojitokeza

Juma nyoso na  Mwape


Katika utoaji zawadi hali ikawa hivi umeme ukakatika na giza likawatala na mwanga unaoonekana ni mwanga wa  simu

Wachezaji wa Yanga wakifurahia ubingwa wa kombe la Kagame
YANGA ya Dar es Salaam imeandika historia mpya katika michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati 'Kombe la Kagame' baada ya kuifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Bao hilo lililofungwa dakika ya 108 na Keneth Asamoah lilizamisha ndoto ya Simba iliyotwaa ubingwa huo mara sita kuongeza taji lingine, badala yake sasa Yanga imeongeza idadi ya mara ilizochukua kombe hilo kufikia nne.

Asamoah alifunga bao kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi uliochongwa na kiungo wa zamani wapinzani wao hao Rashid Gumbo aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Godfrey Taita aliyeumia.

Kabla kupiga krosi hiyo Gumbo aliambaa na mpira wingi ya kushoto na kuwatoka mlinzi Nassor Said ‘Chollo’ na kumimina krosi ambayo ingeweza kuokolewa na mlinzi Kelvin Yondani lakini katika harakati za kufanya hivyo aliteleza na kuanguka na mpira kumkuta
mfungaji aliyekuwa nyuma yake na kugonga kichwa ambacho kilijaa wavuni na kumwacha kipa Juma Kaseja akiwa hana la kufanya.

No comments:

Post a Comment