BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limekemea na kulaani tabia ya waumini wa dini hiyo kufanya vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya dini yao kwa kisingizio cha `Kuvunja Jungu’ wakati wa kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Aidha, limesema tabia hiyo ni machukizo mbele za Mwenyeezi Mungu na kwamba Mwezi Mtukufu hukaribishwa kwa yaliyo matukufu.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum ameyasema hayo leo wakati Baraza hilo lilipokuwa likizungumzia kutarajiwa kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kati ya Jumapili au Jumatatu, baada ya kutolewa kwa taarifa ya kuandama kwa mwezi na Ofisi ya Mufti wa Tanzania na Ofisi ya Mufti wa Zanzibar.
“Kuna tabia ya kuvunja jungu kwa njia ya haramu siku za mwisho za mwezi huu, vijana wa kiume na wa kike wanakodi magari wanaenda ‘kujimwaga’ katika fukwe za bahari zilizoko mafichoni na yanayojiri huko hayawi salama,” alisema Sheikh Salum na kuongeza:
“Katika kumbi za starehe huwasikia wasanii wakiwaaalika watu kuvunja jungu, hayo yote ni machukizo mbele za Mwenyeezi Mungu, tuyaache mara moja kwani mwezi Mtukufu hukaribishwa kwa yaliyo matukufu,” alisema.
Alisema kuanza kwa Mwezi Mkutufu, kwa Uislamu ni kutekeleza nguzo ya nne kati ya nguzo tano za Uislamu ambapo Baraza linawataka Waislamu wote kuuheshimu mwezi huo, hata wasiokuwa waislamu waige tabia ya Watanzania kuheshimu matukufu ya watu wa imani nyingine.
Aidha, alisema kuanza kwa mwezi huo, hoteli na migahawa isiyo katika maeneo ya lazima kufunguliwa yasifunguliwe, kumbi za starehe za burudani na hata katika baa zipunguze ghadhabu za Mwenyezi Mungu kwa siku hizo 29 au 30 za Mwezi Mkutufu.
Sheikh Salum pia amewataka wafanyabiashara hasa wa vyakula kuwa na huruma katika mwezi huo kwa kutopandisha bei za vyakula kiasi cha kuwafanya wafungaji kutaabika kupata futari na aina nyingine ya vyakula.
Kuhusu kuwepo kwa migogoro ya Mwezi kwa Waislamu kwamba wapo wanaowahi kufunga na wengine kuchelewa, alisema jambo hilo halitoisha hadi kiama kwani ni asili na jambo la msingi ni kutobugudhiana, kufarakana, kulumbana na kugombana bali waelimishane kila mara.
Kadhalika kuhusu kupungua kwa waislamu katika maeneo ya baa, nyumba za kulala wageni na sehemu za vyakula wakati wa Mwezi Mtukufu, alisema haamini kama waislamu ndio wamekuwa wakishiriki katika maeneo hayo kwa wingi ila ipo tabia ya kuheshimiana baina ya imani nyingine.
Aidha, Sheikh Salum alitumia fursa hiyo kueleza kuwa, Bakwata inawaombea kwa Mwenyezi Mungu Wabunge wa Bunge Jamhuri ya Muungano ili awazidishie hekima, busara na heshima ili yote wayafanyayo yaendane na hadhi ya mahali walipo.
Kauli hiyo, pasi ya shaka inatokana na matukio ya utovu wa nidhamu yanayotajwa au kuonekana kupitia vyombo vya habarihuenda tika siku za hivi karibuni