Pages

Wednesday, May 11, 2011

Wageni wana haki ya kuamini Kilimanjaro haipo Tanzania



DHANA ya kwamba Tanzania tumekuwa hatufaidi maliasili zetu kama vile utalii, madini , pamoja na mlima Kilimanjaro, na badala yake fursa hii inatumiwa na nchi za wenzetu, dhana hii inazidi kupata mashiko kutokana na kile nitachokiita kushindwa kujitambua.

Nasema hivyo nikimaanisha kwamba bado watalii wengi wanazidi kuaminishwa kwamba, nirahisi kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kenya kuliko Tanzania.

Lakini bado serikali kwa kupitia mamlaka za mawasiliano na utalii hawajaona umuhimu wa kudhibiti habari au taarifa potofu zinazoingia mara tu unapoingia Wilaya jirani na Mlima Kilimanjaro.

Mfano mzuri ukiingia Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro utakaribishwa na ujumbe mfupi (sms) toka Kenya katika baadhi ya mitandao ukiambiwa "umeingia Kenya" au "karibu Kenya” na kupata maelekezo ya huduma kwa nchi hiyo.

Zaidi ya hapo utalakiwa na vyombo vya habari vyenye matangazo makini na yakudhihirisha utaifa wao kutoka Kenya, Vyombo hivyo ni kama vile KBC idhaa ya taifa, Mwanedu FM, Citized radio, Milele FM na nyinginezo lukuki.

Wakati huo kwa Tanzania ni redio mbili tu zinazosikika vizuri, ambazo ni Killi FM na Sauti ya Injili ambazo zote ni za palepale mkoani Kilimanjaro.Hivyo basi kwanini watalii wasione mlima upo Kenya, au ni vema kupitia Kenya kuliko Tanzania?.

Wakati umefika Serikali kuangalia maeneo yenye faida kubwa inayopotea pasipo sababu na isiwe Kilimanjaro tu, ila maeneo yote yenye thamani kubwa katika uchumi wa Taifa.

No comments:

Post a Comment