Pages

Saturday, May 14, 2011

Man United mabingwa wa Ligi ya England

Bao la mkwaju wa penalti lililoonekana la utata lililofungwa na Wayne Rooney lilitosha kuipatia Manchester United ubingwa na kuvunja rekodi ya kunyakua ubingwa wa Ligi ya Soka ya England kwa mara ya 19 katika uwanja wa Ewood Park.

Sir Alex Ferguson
Sir Alex Ferguson


Pointi moja ilitosha kwa meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya 12 tangu aanze kuifundisha timu hiyo katika pambano dhidi ya Blackburn.
Manchester United ilionekana ingepoteza mchezo huo hadi mlinda mlango wa Rovers Paul Robinson alipofanya makosa ya kumuangusha chini Javier Herndandez na wageni wakapatiwa nafasi ya kupiga mkwaju wa penalti.
Rooney alifunga mkwaju huo wa penalti na kuisawazishia timu yake na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kuhanikiza kwa shangwe za ubingwa.
Blackburn walikuwa wa kwanza kupata bao lililopachikwa na Brett Emerton baada ya ngome ya United kujichanganya akiwemo mlinda mlango wake Thomas Kuszczak.
Lakini bao la mkwaju wa penalti katika dakika ya 73 lilitosha kuibua shangwe za ubingwa kwa mashabiki ambapo sasa Manchester United imepata pointi 77 ambazo timu inayofuatia Chelsea hata ikishinda mechi zake zote mbili zilizosalia haitaweza kufikisha pointi hizo.

No comments:

Post a Comment