Pages

Saturday, May 21, 2011

BUZA NA NAULI ZA DALADALA

Hali ilivyo katika kituo cha Tandika 

BAADHI ya wakazi wa Buza wilayani Temeke, wamelalamikia kutozwa nauli kubwa za usafiri wa daladala kinyume cha  viwango vilivyowekwa kisheria.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti jana, wananchi hao walisema wamekuwa wakitozwa nauli ya kati ya Sh500 na Sh1,000 badala ya Sh300 iliyowekwa kisheria.Mmoja wa wananchi hao, Abdallah Zimbwe, alisema ni miezi miwili sasa tangu waanze kutozwa viwango hivyo vya juu.

"Wanatutoza nauli kubwa na tukigoma kulipa, basi wanakataa kuleta magari yao Buza. Sasa kwanini tulipe kiwango tofauti na kile kilichopendekezwa kisheria ambacho ni Sh300,"alihoji Zimbwe.

Mkazi mwingine aliyejitambulisha kuwa ni Neema Samson, alisema hali inakuwa mbaya zaidi hasa nyakati za jioni wanapolazimika kulipa hata Sh1,000 kwa safari.
Licha ya watu wazima kutozwa viwango hivyo vikubwa, wanafunzi nao wamelalamikia kutozwa hadi Sh 200 badala ya Sh 50 iliyopendekezwa kisheria.
"Na hata hiyo Sh200 unalipa mlangoni kabla hujapanda gari na wakati mwingine tunakataliwa kabisa kupanda magari, utakuta unatoka shule mapema unakaa kituoni zaidi ya saa nne ukisubiri usafiri,"alisema Anjela Joseph, anayesoma katika Shule ya Sekondari Kibasila.
Kwa upande wao, madereva waliozungumza n, walisema wanatoza viwango hivyo kutokana na ubovu wa barabara waliodai kuwa unasababisha magari yao kuharibika.

"Yaani unaweza kwenda safari moja ukarudi unajikuta unapeleka gari gereji , barabara ni mbovu sana inaharibu magari yetu,"alisema Juma Abdallah ambaye ni mmoja wa madereva hao.

No comments:

Post a Comment