Patricia Kimelemeta
MBUNGE wa Vunjo, Dk Augustine Mrema amesema kama Manispaa ya Temeke itakuwa imegawa viwanja kwa vigogo peke yao akiwamo yeye bila ya kuwangalia wananchi wa kawaida, itakuwa imefanya kosa kisheria kwa kukiuka haki sawa kwa wote.
Kauli ya Mrema imekuja siku chache baada ya manispaa hiyo kubandika orodha ya majina ya viongozi watakapogawiwa viwanja katika eneo la Gezaulole lililopo nje ya Jiji la Dar es Salaam, jambo ambalo lilisababisha mgongano baina ya wananchi na uongozi wa Manispaa hiyo.
Akizungumza na gazeti juzi, Mrema alisema manispaa hiyo ilipaswa kutenda haki kwa kila mwananchi wakati wa ugawaji wa viwanja hivyo, jambo ambalo lisingeweza kuleta mvutano.
Alisema kitendo walichotumia cha kugawa kwa kuwangalia viongozi peke yake kinaleta taswira mbaya kwa wananchi, jambo ambalo limesababisha kuwapo kwa malalamiko ya hapa na pale.
“Sisi tumeomba viwanja kama wananchi wengine, hivyo walipaswa kugawa haki bila ya kuangalia huyu ni nani? anatoka wapi, jambo ambalo lisingeweza kuleta malalamiko, lakini kitendo cha kugawa kwa viongozi wengi kimesababisha kuwapo kwa malalamiko,”alisema Mrema.
Aliongeza,” niliomba kiwanja kama mwananchi wa kawaida,na kwamba sikutaka kuonyesha dalili yoyote ya kwamba mimi ni kiongozi, lengo ni kuitaka manispaa hiyo kutenda haki wakati wa mgao huo, lakini kilichoonekana ni tofauti ambapo viongozi wamepewa kipaumbele bila ya kushirikisha wananchi, jambo ambalo linaweza kusababisha wananchi kukosa imani na viongozi wao.
Alisema kutokana na hali hiyo Manispaa hiyo inapaswa kujirekebisha ili wasiweze kusababisha migongano isiyokuwa ya msingi na kuweka matabaka ya waliyonacho na wasionacho.
Alisema fomu hizo zilikuwa zinauzwa Sh30,000, kwa kila kiwanja kimoja, na kwamba kila mmoja ana haki ya kutoa na kuingia kwenye mgao huo,hali ambayo isingeweza kuleta mvutano kwa sababu wananchi wangejitokeza kwa wingi zaidi na kuingia kwenye mgao huo.
Naye Mbunge wa Viti maalumu Kigoma, Josephine Genzabuke alisema baada ya manispaa hiyo kutangaza zabuni ya uuzaji wa viwanja, walijitokeza watu wengi kujaza fomu akiwamo yeye bila ya kutumia njia za panya.
Alisema jina lake kuonekana kwenye orodha ya majina ya vigogo ni uteuzi wa manispaa ambao hawezi kujua kilichokuwa kinaendelea.
“Mimi nimejitokeza kama walivyo watu wengine, lengo ni kuomba kiwanja kwa ajili ya familia yangu, kama kumekuwa na uchaguzi wa viongozi peke yake bila ya kushirikisha wananchi siwezi kujua chochote, kwa sababu nami nina haki ya kuomba na kupewa kama walivyo wananchi wengine,”alisema Genzabuke.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emanuel Nchimbi alisema kuwa, hawezi kuzungumzia kitu chochote kuhusu suala
“Naona mnataka habari ili kuweze kuuza gazeti lenu kutoka kwangu, sina cha kusema kuhusu hilo na siwezi kujibu chochote, kwa heri,”alisema Nchimbi.
No comments:
Post a Comment