Pages

Wednesday, January 8, 2014

Eneo la Temeke Kota jijini Dar es Salaam hivi sasa ni kama limepigwa BOMU. Nyumba zote zapigwa chini na waliokuwa wakazi wake wahaha kutafuta sehemu za kujisitiri.

Hili ni eneo la Kota lililoko Temeke Mwisho jijini Dar es Salaam. Limebomolewa lote kupisha mradi wa Serikali ambao mpaka sasa haujaweka wazi kwa Wananchi wa eneo hilo. Hali ndivyo kama inavyoonekana kwenye hiyo picha.

Kwenye picha kulia askari wa manispaa ya Temeke akiwa anaangalia moja ya nyumba ilikuwa inasubiri kubomolewa eneo la Temeke Kota jijini Dar es Salaam.

Eneo la Temeke Kota Dar es Salaam lilivyo hivi sasa baada ya baadhi ya nyumba kubomolewa, hali iliyopelekea wakazi wengi kutafuta sehemu za kujihifadhi.

Moja ya nguzo ya Umeme iliyoangushwa na Greda wakati wa zoezi hilo. Nguzo hiyo iko mtaa wa Mkuranga A.

Unajionea mwenye hali ilivyo Temeke Kota kwa sasa.

Nadhani unaweza jenga kiwanja cha kuchezea soka eneo la Temeke kota kwa sasa.

Baadha ya watu wakichukua baadhi ya kokoto zilizotoka kwenye nyumba zilizobomolewa eneo la Temeke kota jijini Dar es Salaam.

Temeke Kota haitazamiki kwasasa nyumba zote zimepigwa chini.

Mti mrefu unaoonekana kwa mbali unafahamika vizuri kwa wale wakazi wa Temeke Kota Jijini Dar es Salaam.

Nyumba ya Mwalimu Kalinga kwa wanaomfamu ndio iliyobakia.

Nyumba pekee iliyobakia Temeke ndio anayoishi Mwl. Kalinga. Amegoma kuondoka eneo hilo na anasema nyumba hiyo kapewa na Hayati Baba wa Taifa.