Pages

Saturday, August 17, 2013

MIVINJENI HAMENI

Anna Tibaijuka - World Economic Forum on Africa 2010 aaf48
Serikali imewataka wakazi wa Mivinjeni Kurasini jijini Dar es Salaam kuhama ili kupisha ujenzi Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa katika eneo hilo.Mradi huo unateketezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na China katika eneo lenye ukubwa wa hekta 670 na kiasi cha Sh90.4 bilioni zimetengwa kugharimia ujenzi wa kituo hicho.
P.T

Akizungumza na wananchi hao jana, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alisema ni vyema watu wakaondoka katika maeneo hayo badala ya kupoteza muda wao.
Alisema tayari Serikali imewaandalia wananchi hao maeneo ya kuishi huko Kimbiji.
Pia aliwaonya wakazi hao wasikubali kudanganywa na wanasheria wakiamini kuwa watawasaidia katika suala hilo.
"Msidanganywe na wanasheria katika hilo, watakula pesa yenu na kesi hamtashinda na hatimaye mtabaki kulaumiana," alisema Tibaijuka.
Msimamo huo wa Serikali umekuja siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik, kusitisha kwa muda uboamaji wa nyumba katika eneo hilo.
Alisema wananchi, wataendelea kuishi katika nyumba zao hadi hapo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi atakapotoa tamko.
Lakini kwa upande wao, wananchi hao waliazia kwenda mahakamani na kwamba waliofungua kesi ya awali, hawataifuta.
Mjengwa