Matukio Mbalimbali yaliyofanyika Mwezi wa 8 ndani ya Wilaya ya Temeke.
Wadau wa Temeke maeneo ya Wailes wakiwa kwenye Uwanja wa Bandari ulipo Tandika jijini Dar es Salaam wakiangalia moja ya mechi ya mpira wa miguu iliyokuwa ikifanyka kwenye Uwanja huo hivi karibuni.Kutoka kushoto ni David Chonde ni shabiki wa Simba s.c, Abed shabiki wa Ndala ama Yanga na Said Mzirary ni shabiki wa simba s.c.
Rajab Kiazi "Ticha" katikati akiwa na wadau wake wakiangalia mpira wa miguu uwanja wa Bandari Temeke hivi karibuni.
He!!! Hivi haya mambo bado yapo!!! Najua utakuwa unajiuliza ni Uwanja gani haya mambo yanafanyika. Huu ni Uwanja wa Bandari ulipo Temeke jijini Dar es Salaam. Vijana wakuruka ukuta kuingia Uwanjani kwa nia ya kushuhudia moja ya mechi zilizokuwa zikifanyika kwenye Uwanja huo.
Uwanja mkubwa wa Taifa wa mpira wa miguu ambao una uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.Timu ya Yanga iliahidi wanachama wake kujenga Uwanja utakaochukua watu 45,000 mpaka leo kimya kulikoniiiiiiiiiii.
Chuo kikuu cha ualimu Dar es Salaam DUCE, ni moja ya chuo kikuu kulichopo Temeke pembezoni mwa Uwanja wa Taifa.
Hawa ni walinzi waliopo Uwanja wa Taifa wakikagua baadhi ya tiketi kwenye Uwanja huo.
Bajaj ya Temeke pamoja ikiwa kwenye Uwanja Bandari Tandika. Ukitaka usafiri wa Bajaj ndani ya Temeke piga simu zilizopo hapo juu kwenye blog hii. (Picha kwa hisani ya Temekepamoja blog).