Pages

Saturday, September 22, 2012

Usijichoshe na kazi, msinyano utakuua!

Wachunguzi wa Uingereza wanasema kuwa kuna uhusiano wa msinyano(Stress) na matatizo ya akili. Watafiti wa Uingereza wamegundua kuwa kufanya kazi nyingi na kuwa na usimamizi mdogo kuzihusu ni hatari mno.
Watafiti hao walitathmini tafiti 13 zilizokuwa zimefanywa ulaya na kuwahusisha karibu watu elfu 200 na kutambua kuwa "kazi zinazochosha" zimehusishwa na ongezeko la asili mia 23 la hatari ya kukumbwa na maradhi ya moyo na vifo vinavyotokana na maradhi ya mishipa ya moyo.
Ripoti ya Jarida la matibabu la Lancet inasema kuwa athari kwa moyo ilikuwa ndogo kushinda kuvuta sigara na kutofanya mazoezi.
Wakfu wa Moyo wa Uingereza umesema kuwa ni muhimu kujua namna watu wanavyochukulia msinyano unaoambatana na kazi.
Kazi za kuchosha ni mojawapo ya msinyano. Kundi hilo la watafiti kutoka Chuo kikuu cha London limesema kuwa kufanya kazi katika taaluma yoyote kunaweza kusababisha uchovu mkubwa na hutokea zaidi kwa wafanyikazi wa taaluma zinazotajwa kuwa za chini.
Madaktari ambao jukumu lao ni kutoa maamuzi mara kwa mara hawamo katika hatari kubwa ya kukumbwa na msinyano kuliko watu wanaofanya katika viwanda vyenye shughuli nyingi za kuzalisha bidhaa uhuru

Msinyano
Kumekuwa na ushahidi wa kutatanisha kuhusu athari za kazi za kuchosha kwa moyo.
Katika makala haya watafititi walitathmini tafiti 13.
Mwanzoni mwa kila utafiti, watu waliulizwa ikiwa walikuwa na kazi nyingi ama muda mchache kufanya kazi zao mbali na maswali yanayohusiana na uhuru waliokuwa nao wa kutoa maamuzi.
Kisha wakagawanywa katika makundi ya watu wanaofanya kazi za kuchosha na kuwafuatilia kwa miaka saba unusu.
Mmoja wa watafiti hao , Profesa Mika Kivimaki, wa chuo kikuu cha London, alisema: "matokeo yetu yanaonyesha kuwa kazi za kuchosha zinahusishwa na hatari japo ndogo ya maradhi ya kwanza ya moyo ambayo hunawiri na kusababisha shinikizo la damu.
Watafiti hao walisema kuwa kuondoa kazi za kuchosha kutapunguza matukio hayo kwa asili mia 3.4% na , 36% ikiwa kila mtu ataaacha kuvuta sigara.
'hamna mabadiliko'
Prof Kivimaki anasema ushahidi wa athari za moja kwa moja ya kazi za kuchosha kwa moyo ulikuwa wa mchanganyiko.
Aliiambia BBC kuwa kazi zinazochosha zinahusishwa na uchaguzi wa mitindo ya maisha ambayo ni mbovu kwa moyo: "Tunajua wavutaji sigara wana kazi nyingi wanaweza kuvuta kiwango kikubwa ilhali watu walio na msisimuko kufanya kazi nyingi wana uwezekano mkubwa wa kufifia na kuna uhusiano na kunenepa kupita kiasi.
"Ikiwa mtu ana msinyano mkubwa kazini anaweza kupunguza uwezekano wa kuathirika kwa kuzingatia mwenendo wa afya bora."
Prof Peter Weissberg, Mkurugenzi wa matibabu katika Wakfu wa Moyo wa Uingereza , anasema: "tunajua kukumbwa na msinyano kazini na kutoweza kubadilisha hali hiyo kunaweza kusababisha maradhi ya moyo.
"Utafiti huu mkubwa unathibitisha kuwa athari mbaya katika mazingira ya kazi nyingi ni ndogo wa mfano kuliko athari inayosababishwa na uvutaji sigara na kutofanya mazoezi.
"Ingawa msinyano kazini ni jambo lisilopingika, namna ya kukabiliana na shinikizo hizo ni muhimu, lakini uvutaji sigara ni hatari sana kwa moyo wako. Kula lishe bora, kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kuacha kuvuta sigara kutaondoa uwezekano wa kupata msinyano kutokana na kazi yako.
Alisema kazi nyingi ni "ni sehemu tu ya kuvuruga saikolojia katika mazingira ya kazi".

No comments:

Post a Comment