Pages

Thursday, September 27, 2012

BINGWA WA BIRIANI

Said Enzi maarufu Kidishi Bingwa huyu jamaa kwa masuala ya msosi maeneo ya Temeke
 Hapa mambo yakiendelea


UJUMBE WA LEO

KUAJIRIWA NI HIARI NA SI LAZIMA
KILA MTU ANAYO HIARI YA KUAJIRIWA AU KUTOKUAJIRIWA KWA AIDHA KUJIAJIRI MWENYEWE AU KUKAA BILA SHUGHULI YA KUFANYA. LAKINI UKIAMUA KUAJIRIWA HUNA HIARI YA KUFANYA AU KUTOKUFANYA KAZI. HIVYO UKIIKUBALI AJIRA NI LAZIMA
1-UWAHI KAZINI
2-UWE NA MPANGO KAMILI WA KAZI
3-UWE SEHEMU YA KAZI AU INAYOHUSIANA NA KAZI MUDA WOTE WA KAZI
4-UIFANYE KAZI YAKO KWA BIDII UAMINIFU UFANISI: NA
5-UMFAHAMISHE MKUU WAKO WA KAZI KAMA ITAKULAZIMU KUTOKUWEPO MAHALI PA KAZI

KAMA SIVYO ITAKUBIDI UANGALIE UPYA HIARI YAKO YA KUTAKA KUENDELEA KUAJIRIWA. LA SIVYO MWAJIRI WAKO ITABIDI AKUSAIDIE KUFANYA MAAMUZI JUU YA HIARI YAKO KWA AIDHA KUKUSIMAMISHA KAMA SI KUKUFUKUZA KABISA- HIVYO

ITUMIE HIARI YAKO IPASAVYO
 
Na.Harakati Zangu

Saturday, September 22, 2012

Usijichoshe na kazi, msinyano utakuua!

Wachunguzi wa Uingereza wanasema kuwa kuna uhusiano wa msinyano(Stress) na matatizo ya akili. Watafiti wa Uingereza wamegundua kuwa kufanya kazi nyingi na kuwa na usimamizi mdogo kuzihusu ni hatari mno.
Watafiti hao walitathmini tafiti 13 zilizokuwa zimefanywa ulaya na kuwahusisha karibu watu elfu 200 na kutambua kuwa "kazi zinazochosha" zimehusishwa na ongezeko la asili mia 23 la hatari ya kukumbwa na maradhi ya moyo na vifo vinavyotokana na maradhi ya mishipa ya moyo.
Ripoti ya Jarida la matibabu la Lancet inasema kuwa athari kwa moyo ilikuwa ndogo kushinda kuvuta sigara na kutofanya mazoezi.
Wakfu wa Moyo wa Uingereza umesema kuwa ni muhimu kujua namna watu wanavyochukulia msinyano unaoambatana na kazi.
Kazi za kuchosha ni mojawapo ya msinyano. Kundi hilo la watafiti kutoka Chuo kikuu cha London limesema kuwa kufanya kazi katika taaluma yoyote kunaweza kusababisha uchovu mkubwa na hutokea zaidi kwa wafanyikazi wa taaluma zinazotajwa kuwa za chini.
Madaktari ambao jukumu lao ni kutoa maamuzi mara kwa mara hawamo katika hatari kubwa ya kukumbwa na msinyano kuliko watu wanaofanya katika viwanda vyenye shughuli nyingi za kuzalisha bidhaa uhuru

Msinyano
Kumekuwa na ushahidi wa kutatanisha kuhusu athari za kazi za kuchosha kwa moyo.
Katika makala haya watafititi walitathmini tafiti 13.
Mwanzoni mwa kila utafiti, watu waliulizwa ikiwa walikuwa na kazi nyingi ama muda mchache kufanya kazi zao mbali na maswali yanayohusiana na uhuru waliokuwa nao wa kutoa maamuzi.
Kisha wakagawanywa katika makundi ya watu wanaofanya kazi za kuchosha na kuwafuatilia kwa miaka saba unusu.
Mmoja wa watafiti hao , Profesa Mika Kivimaki, wa chuo kikuu cha London, alisema: "matokeo yetu yanaonyesha kuwa kazi za kuchosha zinahusishwa na hatari japo ndogo ya maradhi ya kwanza ya moyo ambayo hunawiri na kusababisha shinikizo la damu.
Watafiti hao walisema kuwa kuondoa kazi za kuchosha kutapunguza matukio hayo kwa asili mia 3.4% na , 36% ikiwa kila mtu ataaacha kuvuta sigara.
'hamna mabadiliko'
Prof Kivimaki anasema ushahidi wa athari za moja kwa moja ya kazi za kuchosha kwa moyo ulikuwa wa mchanganyiko.
Aliiambia BBC kuwa kazi zinazochosha zinahusishwa na uchaguzi wa mitindo ya maisha ambayo ni mbovu kwa moyo: "Tunajua wavutaji sigara wana kazi nyingi wanaweza kuvuta kiwango kikubwa ilhali watu walio na msisimuko kufanya kazi nyingi wana uwezekano mkubwa wa kufifia na kuna uhusiano na kunenepa kupita kiasi.
"Ikiwa mtu ana msinyano mkubwa kazini anaweza kupunguza uwezekano wa kuathirika kwa kuzingatia mwenendo wa afya bora."
Prof Peter Weissberg, Mkurugenzi wa matibabu katika Wakfu wa Moyo wa Uingereza , anasema: "tunajua kukumbwa na msinyano kazini na kutoweza kubadilisha hali hiyo kunaweza kusababisha maradhi ya moyo.
"Utafiti huu mkubwa unathibitisha kuwa athari mbaya katika mazingira ya kazi nyingi ni ndogo wa mfano kuliko athari inayosababishwa na uvutaji sigara na kutofanya mazoezi.
"Ingawa msinyano kazini ni jambo lisilopingika, namna ya kukabiliana na shinikizo hizo ni muhimu, lakini uvutaji sigara ni hatari sana kwa moyo wako. Kula lishe bora, kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kuacha kuvuta sigara kutaondoa uwezekano wa kupata msinyano kutokana na kazi yako.
Alisema kazi nyingi ni "ni sehemu tu ya kuvuruga saikolojia katika mazingira ya kazi".

MTUMENTO

Huyu jamaa maarufu sana Mitaa ya Temeke jina lake juu hapo kama unavyoliiona

UJUMBE WA KAWA


Tuesday, September 18, 2012

TANDIKA MAGOLOFANI

 Barabara ya Bandari kuelekea Davis Corner


 Hospital ya Bilal Transfoma
 Maeneo ya shule ya Mabatini (Under Dox)
 Shule ya Msingi Mabatini
 Block B

 Uwanja wa mpira wa Under Dox

 Njia panda ya kwenda Tandika, Bandari na Mwembe Yanga

TUNA SAFARI NDEFU KWENYE MICHEZO-MWENEMTI

 Mshiriki pekee wa Tanzania katika mashindano ya Paralimpiki Zaharan Mwenemti amesema  tuna safari ndefu kwa Tanzania hadi kufikia hatua ya kuchukua medali, mshiriki huyu ambaye amerudi wiki chache zilizopita amesema kuna tofauti kubwa sana kati ya wao na sisi ni kuongeza juhudi zaidi na mazoezi ya mda mrefu kama wenzetu wanavyojiandaa.
Moja ya picha Zaharani akiwa Msumbiji katika mchujo
Zahrani akirusha tufe

Tuesday, September 11, 2012

SIMBA YAIFUNGA AZAM NGAO YA JAMII

 Kikosi cha Azam hii leo
 Kikosi cha Simba
 Washabiki wa Simba waliohudhuria katika mchezo huo wa ngao ya hisani


Magoli yaliyofungwa na Danny Akuffoh, Okwi na Mwinyi Kazimoto yameiwezesha timu ya Simba kuifunga Azam F.c 3-2 magoli ya Azam yalifungwa na John Boko na K. Tchetche. Simba ni mara ya pili mfululizo kuchukua ngao ya hisani

Monday, September 10, 2012

MAZINGAOMBWE

 Amekaa bila kutumia msaada wa chochote kwa chini huku kwetu mazingaombwe kwao nini hapa mwendesha blog ya .darstockholm akipiga picha za kumbukumbu
Picha zaidi:www.darstockholm.blogspot.com

Friday, September 7, 2012

MAISHA YANASONGA


Mechi Ya Ngao Ya Jamii Kuchangia Hospitali Ya Temeke

 
     Release No. 142
                  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
        Septemba 7, 2012

MECHI YA NGAO YA JAMII KUCHANGIA HOSPITALI YA TEMEKE
Asilimia tano ya mapato yatakayopatikana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kati ya Simba na Azam yatakwenda kwenye Hospitali ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Kabla ya kukabidhi, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakutana na uongozi wa Hospitali ya Temeke kupanga maeneo ambayo fedha hizo zitatumika kwenye hospitali hiyo.

Mechi hiyo ya uzinduzi rasmi wa msimu wa 2012/2013 itafanyika Jumanne ya Septemba 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio kwenye mchezo huo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.

WACHEZAJI WAWILI WAOMBEWA ITC URENO
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ureno (FPF) limetuma maombi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupatia Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wawili waliokuwa wakicheza mpira nchini.

Wachezaji wanaoombewa ITC ni Hamis Thabit Mohamed (19) ambaye klabu yake ya mwisho aliyoichezea nchini ilikuwa African Lyon wakati mwingine ni Abuu Ubwa Zuberi (20) ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea timu ya Yanga.

Kwa mujibu wa FPF, wote wawili wanaoombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa (amateur) ili waweze kujiunga na timu ya Atletico Sport Clube ya Ureno ambayo hata hivyo haikuelezwa iko daraja gani nchini humo.

Pia FPF imeombwa kupatiwa hati ya maelezo ya mchezaji (player’s passport) kwa kila mmoja ikiwemo taarifa za ushiriki wao katika mechi rasmi zinazotambuliwa na TFF wakiwa katika klabu zao hizo za zamani.

STARS YAPANGIWA UGANDA CHAN 2014
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepangiwa kucheza na Uganda (The Cranes) katika raundi ya kwanza ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika Afrika Kusini mwaka 2014.

Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa jana (Septemba 7 mwaka huu) makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jijini Cairo, Tanzania imeingia moja kwa moja raundi ya kwanza ambapo itacheza na Uganda.

Mechi ya kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kati ya Juni 21,22 na 23, 2013 wakati ya marudiano itakuwa Uwanja wa Mandela ulioko Namboole jijini Kampala kati ya Julai 5,6 na 7, 2013.

Nchi 38 zinashiriki katika mechi hizo za mchujo ambapo nyingine zitaanzia raundi ya awali itakayochezwa kati ya Novemba 30 na Desemba 1 na 2 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Desemba 14,15 na 16 mwaka huu.

Ratiba imepangwa kwa makundi ya kanda ambapo jumla ya timu 16 ndizo zitakazocheza fainali hizo nchini Afrika Kusini. Kanda hizo ni Kaskazini itakayopeleka timu mbili katika fainali, Magharibi A (timu mbili), Magharibi B (timu tatu), Kati (timu tatu), Kati Mashariki (timu tatu), Kusini (timu tatu akiwemo mwenyeji Afrika Kusini).

Kwa upande wa kanda ya Tanzania (Kati Mashariki), timu zinazoanzia raundi ya awali ni Burundi, Eritrea, Ethiopia na Kenya.

Fainali za Kwanza za CHAN zilifanyika mwaka 2009 nchini Ivory Coast ambapo Tanzania ilishiriki huku Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ikiibuka bingwa. Fainali za Pili zilichezwa mwaka 2011 nchini Sudan ambapo Tunisia ilitwaa ubingwa. Fainali za Kwanza zilishirikisha timu nane kabla ya kuongezwa hadi 16 za sasa.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)