Pages

Thursday, June 28, 2012

BALOTELI AWAMALIZA WAJERUMANI



Mario Balotelli alifunga magoli mawili ya kupendeza mno na kuiwezesha timu yake ya Italia kuishangaza Ujerumani kwa kuifunga magoli 2-1 katika nusu fainali ya Euro 2012, na nafasi ya kucheza mechi ya fainali mjini Kiev dhidi ya Uhispania.
Mabao ya mshambulizi huyo wa klabu ya Manchester City ya England, aliingiza goli la kwanza wavuni kupitia kichwa, na pili kwa mkwaju wa kasi mno katika uwanja wa mjini Warsaw, na Italia kuwathibitishia Wajerumani katika kipindi cha kwanza kwamba ilikuwa na nia kamili ya kufika fainali.
Wajerumani, kufuatia mshituko, walianza kucheza kwa makini zaidi, lakini bao lao la penalti, ambalo lilipatikana katika dakika ya 92, kupitia Mesut Ozil, lilichelewa mno, na halikuweza kuwaokoa.
Italia kamwe hawajawahi kushindwa na Ujerumani katika mashindano makubwa, na wamefanikiwa sasa kucheza mechi nane dhidi ya Ujerumani pasipo kushindwa.
Hii sasa itakuwa mara ya tatu kwa Italia kuingia fainali za michuano hii ya mataifa ya Ulaya, na wataingia fainali kama timu inayodhaniwa kuwa dhaifu ikilinganishwa na mabingwa watetezi Uhispania.
Timu hii ya meneja Cesare Prandelli ilistahili ushindi, kwani sio tu waliweza kupambana na Ujerumani ambayo iliwashinda wapinzani wao kwa urahisi, bali pia walifunga mabao yao mapema katika kipindi cha kwanza.
Timu hiyo ya Azzurri ilikuwa na nafasi ya kujiongezea magoli, lakini ilicheza kwa tahadhari kwa kuhofia kwamba iwapo ingeliongoza mashambulizi zaidi dhidi ya Italia, kulikuwa na uwezekano wa ngome yao kuachwa ikiwa dhaifu, na Wajerumani kuwashambulia.

No comments:

Post a Comment