Pages

Saturday, June 30, 2012

MDAU OMAR KAZEMBE APATA JIKO

 Mdau omari Kazembe akitia saini katika kitabu cha ndoa na mkewe Bi. Asnat
 Hapa akiwa na dada zake
Mashemeji kama kawa

Thursday, June 28, 2012

BALOTELI AWAMALIZA WAJERUMANI



Mario Balotelli alifunga magoli mawili ya kupendeza mno na kuiwezesha timu yake ya Italia kuishangaza Ujerumani kwa kuifunga magoli 2-1 katika nusu fainali ya Euro 2012, na nafasi ya kucheza mechi ya fainali mjini Kiev dhidi ya Uhispania.
Mabao ya mshambulizi huyo wa klabu ya Manchester City ya England, aliingiza goli la kwanza wavuni kupitia kichwa, na pili kwa mkwaju wa kasi mno katika uwanja wa mjini Warsaw, na Italia kuwathibitishia Wajerumani katika kipindi cha kwanza kwamba ilikuwa na nia kamili ya kufika fainali.
Wajerumani, kufuatia mshituko, walianza kucheza kwa makini zaidi, lakini bao lao la penalti, ambalo lilipatikana katika dakika ya 92, kupitia Mesut Ozil, lilichelewa mno, na halikuweza kuwaokoa.
Italia kamwe hawajawahi kushindwa na Ujerumani katika mashindano makubwa, na wamefanikiwa sasa kucheza mechi nane dhidi ya Ujerumani pasipo kushindwa.
Hii sasa itakuwa mara ya tatu kwa Italia kuingia fainali za michuano hii ya mataifa ya Ulaya, na wataingia fainali kama timu inayodhaniwa kuwa dhaifu ikilinganishwa na mabingwa watetezi Uhispania.
Timu hii ya meneja Cesare Prandelli ilistahili ushindi, kwani sio tu waliweza kupambana na Ujerumani ambayo iliwashinda wapinzani wao kwa urahisi, bali pia walifunga mabao yao mapema katika kipindi cha kwanza.
Timu hiyo ya Azzurri ilikuwa na nafasi ya kujiongezea magoli, lakini ilicheza kwa tahadhari kwa kuhofia kwamba iwapo ingeliongoza mashambulizi zaidi dhidi ya Italia, kulikuwa na uwezekano wa ngome yao kuachwa ikiwa dhaifu, na Wajerumani kuwashambulia.

TAMKO LA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 28.06.2012

Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.

Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.

Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.

Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka, Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.

Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.

Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.

Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.

              Imetolewa na Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

KASSIM MANARA ADEKA KWA MAMA

 Kassim Manara akiwa na Mama yake mzazi baada ya kutoonana kwa kipindi cha miaka 25
 Kassim Manara akiwa na Dada zake pamoja na mama yake.
 Familia ya Manara
Kassim akiwa na baadhi ya vijana wake wa Temeke Wailes katika picha ya pamoja

Tuesday, June 26, 2012

SOKO LA MBWA

 Ikiwa hali ya uteteaji wa haki za wanyama zikizidi kushamiri lakini tofauti na nchi ya china ambayo kuna soko maalum la supu ya Mbwa na Paka. Picha ya juu ambayo mbwa wakiingizwa katika soko hilo kwa kwenda kuchinjwa.
 Kitu cha supu kikiwa tayari
 Baadhi ya wateja wakipata supu ya Mbwa katika mgahawa mmoja nchini china
Baadhi ya Mbwa wakiwa wameuliwa tayari kwa maandalizi

MAANDAMANO

Vijana Wa Tandika Kwa Pamoja Tutafanya Maandamano Yatakayoanzia Tandika Mpaka Dodoma (Bungeni) Kwenda Kudai Iwekwe Sheria Na itambulike Kuwa Wizi Ni Taaluma Kama Taaluma Zingine , Tunatumia Akili , Tunaweza Kukuibia Hata Kama umesoma , Tuna Mbinu Za Hali Ya juu , Tuheshimiwe , Tuko Tayari Kulipa Kodi Kuongeza Pato La Serikali ,
C.J.Webber Prezidaa

Sunday, June 24, 2012

HATA KWETU WAPO

Raia wa Japan ambao wapo Mtoni kwa Kindande wakiwa katika mafunzo ya kutaka kujua uhalisi wa maisha halisi ya uswaz dhumuni kubwa la kutembelea mitaa ya uswahilini ni kujua watu wanaishi vipi katika maeneo hayo.

Mwenyeji wa wageni hao akiwa na mgeni wake

Mkuu wa Kitengo cha utamaduni cha Japan akiwa Sudi Saidi ambaye ndie mwenyeji wao

Wednesday, June 20, 2012

MTONI KWA KABUMA

 Huku kwetu sera ya Ujamaa bado inaendelea kusaidiana kwenye shida na raha mchana wa leo
 Soko la Mtoni kwa Kabuma  wauzaji wote wamekimbilia barabara vizimba vitupu
 Vyuku kama kawa kipande buku
 Biashara kubwa Mitaa ya Mtoni Mkaa

 Sokoni
Barabara ya kwa Kabuma

Tuesday, June 19, 2012

MADARAKA DAY IN NUNBERG

 Baadhi ya wadau waliofika katika sherehe hiyo


 Muandaaji wa shughuli nzima  Dj Max akiwa mmoja wa wahudhuriaji katika hafla hiyo

Friday, June 15, 2012

MTOTO RUKIA AFARIKI DUNIA

Ndugu zangu wapendwa najua tulimpenda sana mtoto RUKIA na kuamua kujitolea kwa hali na mali lamini Mungu amempenda zaidi.Kazi yake mola aina makosa.RUKI AMEFARIKI DUNIA JIONI HII,mnamo saa 12:45 jioni hii ameaga dunia.Maralia yalimpata jana jioni,jitihada zilitumika kumuokoa lakini Mungu amemwita ktk makazi ya milele.Nafanya jitihada za kuondoa mwili wa marehemu kesho asubuhi tayari kwa mazishi.Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Ruangwa amenithibitishia kunipa gari la wagonjwa kesho asbuhi.kwenda kuchukua mwili wa marehemu
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi
amin

Wednesday, June 13, 2012

TEMEKE PAMOJA NA JUMP OFF : STRAIGHT FROM THE STREET

 Jabir Saleh akiwa dj Khaleed Uledy aka KU wakijadili jabo kabla ya mahojiano
 Show Love KU na Ramaraldo(TemekePamoja)
 Mahojiano yakiendelea hapa kidogo lazima uwonyeshe upole kilikuwa kipindi cha maswali
 Nikitoa maelekezo kuhusu hali ya maisha kwa ujumla kwani madaq ilikuwa ni kutoka nje ya nchi kunaweza kutatua tija ya maisha yako
Jabir Salehe na KC waliosimama wakiwa na Sandra mtangazaji wa PILLOW TOK
KC ambaye ni mwendeshaji wa tovuti ya dartostockholm ambaye nae alikuwepo katika kuchangia mada

JANDO

Maandalizi ya kwenda jandoni

DIWANI DOTO MSAWA MGENI RASMI MISS KIGAMBONI

 

DIWANI wa Kata ya Kigamboni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dotto Msawa, atakuwa mgeni rasmi katika shindano la urembo la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu ' Redd's Miss Kigamboni 2012' ambalo litafanyika kesho Ijumaa kwenye ukumbi wa Navy Beach jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya K&L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema jana kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na wanamshukuru diwani huyo pamoja na diwani wa Vijibweni (CCM), Suleiman Mathew, kusaidia maandalizi ya shindano hilo.
Alisema kuwa warembo 12 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanatarajia kuchuana kuwania taji hilo na anaamini kwamba kitongoji hicho kimepania kurudisha taji la Miss Tanzania kwenye Kanda ya Temeke.
Aliongeza kuwa ili kuboresha shindano hilo bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma na msanii na mchekeshaji mahiri hapa nchini, Mpoki watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho.
Aliwaomba mashabiki na wadau wa sanaa ya urembo kujitokeza kushuhudia malkia wa Kigamboni anavyopatikana ikiwa ni shindano pekee lililoko ufukweni wa bahari.
Aliwataja warembo watakaochuana kuwa ni pamoja na Susanne Jeremiah, Agness Goodluck, Elizabeth Boniface, Dorothea Kessy, Esther Albert, Edda Silyvester, Sophia Martin, Doreen Kweka, Khadija Kombo, Linnah David, Rosemary Peter na Domotila Shayo.
Aliwashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao ni Redd's, Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global Publishers, Nobro Collections, Times FM na Clouds FM.
Aliongeza kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika shindano hilo wataungana na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe ili kuwania taji la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.

Sunday, June 10, 2012

TAIFA STARS 2- GAMBIA 1






Taifa Stars imeilaza Gambia kwa bao 2-1 katika mechi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil 2014. Mabao ya Stars yamewekwa kimiani na Shomari Kapombe na Erasto Nyoni. Kwa sasa Stars ina pointi 3 na inashika nafasi ya pili katika kundi C linaloongozwa na Ivory Coast wenye pointi 4.

Saturday, June 9, 2012

MAKUNDI YA TMK WANAUME YALIVYOPOA KIMUZIKI

HERIETH MAKWETTA
HISTORIA ya makundi ya muziki wa kizazi kipya ya Wanaume Halisi na Wanaume Family, si rahisi kusahaulika kirahisi akilini mwa wapenzi wa muziki huo Afrika Mashariki.

Ni kwasababu yaliyokana na kundi moja lililokuwa na nguvu kubwa, hata lililipomeguka bado kila upande ulishika chati.
Mgawanyiko wao ulitokea mwaka 2009 baada ya Juma Kassim 'Sir Nature' kujiondoa katika kundi la TMK Wanaume Family na kuunda TMK Wanaume Halisi, alijiengua na wengine kadhaa.

Kundi hilo lilijipatia sifa na umaarufu baada ya kuibuka na albamu yake ya kwanza, inayoitwa �Tatu Bila�. Lakini kabla ya mwaka kuisha kundi la Wanaume Halisi lilivunjika tena baada ya uongozi wake kuwatema wasanii saba na kubaki na watano.

Nature anasema uamuzi huo ulitokana na matakwa ya wadhamini wapya ambapo waliingia nao mkataba, nao ni kampuni ya DLC inayofanya kazi zake katika nchi za Tanzania na China.

Kampuni hiyo ilikuwa ikisimamia kazi zote za kundi hilo, ikiwa ni pamoja na kulitangaza ndani na nje ya nchi na kuliandalia maonyesho.

�Tulipata wakati mgumu sana katika kuchuja vichwa 12 vilivyomo ndani ya kundi ili kubaki na vitano," anasema Sir Nature.
Mbali na yeye wengine wanne waliobaki kundini ni Dolo, Baba Levo, JB wa Mabaga Fresh na KG Son.

Waliochujwa nao wakaamua kuanzisha kundi lao lililofahamika kwa jina la Wanaume.
Wanaume wao walibadili sera. Wakati awali TMK ilikuwa kwa ajili ya wasanii wa Temeke tu, Wanaume wao wakafungua milango kwa yeyote hata awe anatoka Bagamoyo, ili mradi awe mtu wa kazi.

Wanaume wanaundwa na Richard Shauri Rich One, Karim Kazumari Kaka Man, Abdul Ally Mzimu, David Mpangile Daz P, Athuman Yahaya A Man na Juma Mbelwa Juma Jazz.
Wakati hayo yakitokea Inspector Haruni na wenzake wengine walikuwa wameshajiengua awali na kurudia kundi lao la asili, Gangwe Mob.

Hata hivyo kundi la Wanaume Family lililobaki chini ya Fela nalo liliingia doa, Jebi, YP na Y Dash nao wakajiengua na kuunda kundi lao lililoitwa TMK Unity.

Lakini miaka ya hivi karibuni makundi haya mawili maarufu yaani Wanaume Halisi na Wanaume Family yamepunguza kasi na pengine kufunikwa na baadhi ya wasanii wapya waliochipukia

Mwakilishi wa Wanaume Family, Amani Temba 'Mh Temba' anaeleza sababu zilizowafanya kupunguza kasi.

"Ni kweli tumekuwa kimya kwa kiasi fulani, lakini si kimya kirefu kwani hivi karibuni tumetoa kazi. Ni 'Kichwa Kinauma, naamini hii ni kazi iliyokubalika vema tu na mashabiki. Bado tupo," anasema huku akitabasamu.

Anasema mfano upo kwake, kwani ana takribani miaka miwili hajatoa wimbo binafsi, lakini tayari ameshamaliza kazi ya kuandaa wimbo anaotarajia kuuachia hivi punde.
Katika wimbo huo anaoutaja kwa jina la 'Maryoo' anatoboa siri kuwa amemshirikisha Bibi Cheka, kikongwe aliyegukia muziki wa kizazi kipya.

Temba, mkongwe wa Wanaume Family aliyekuwapo tangu awali, anasema kuanzishwa kwa Kituo cha Mkubwa na Wanawe, ndiyo sababu kubwa ya kufifia kwa kundi lao.

"Huu ni mpango maalum, si kwamba Wanaume Family imekufa ila ni mkakati wa kukitangaza kituo cha Mkubwa na Wanawe, kundi letu bado lipo pale pale," anasema.

"Unajua Temba hawezi kutoa wimbo na Aslay akatoa wimbo kwa wakati mmoja, hivyo tumeamua kuwapa sapoti hawa kwanza ili wakue na baadaye tutaendelea."

Katika kupeana nafasi huko, Mh. Temba ameshirikishwa katika wimbo wa Aslay 'Niwe Nawe' na ule wa Bibi Cheka Ni Wewe.
Anasema mfumo wanaoutumia ni kuwafanya vijana wao wajitegemee kwanza ndipo Wanaume Family iweze kurudi upya.

"Kundi bado lina mengi ya kufanya tupo wengi tu na wote tuna nia moja, hivyo tunajitolea kwa hali na mali kuhakikisha tunazalisha vipaji vingi kupitia kundi letu," anasema Temba aliyewahi kutamba na kibao cha Mkono Mmoja alichomshirikisha Chegge.

Monday, June 4, 2012

KARIBU TEMEKE: MATESO YAMEMZIDI

KARIBU TEMEKE: MATESO YAMEMZIDI: UKISTAAJABU YA MUSA....NILIYOYAKUTA KWA SHABANI H.KALEMBO RUKIA ABDALHA ni mtoto wa miaka miwili anayeishi RUANGWA(LUGALO) mkoani LINDI al...

MATESO YAMEMZIDI

UKISTAAJABU YA MUSA....NILIYOYAKUTA KWA SHABANI H.KALEMBO
RUKIA ABDALHA ni mtoto wa miaka miwili anayeishi RUANGWA(LUGALO) mkoani LINDI aliungua maji ya moto,akapelekwa hospitali ya wilaya RUANGWA ambako alipata huduma ya kwanza na kushauriwa aende NDANDA,NYANGAO au MUHIMBILI.Wazazi wa RUKIA hawana uwezo kifedha kumfikisha ktk hospitali hizo,wanazidi kumuuguza mtoto huyo kienyeji nyumbani kwao na sasa mtoto huyo anatoa harufu kali.Mh.MBUNGE KASSIM MAJALIWA saidi mtoto huyu.anaandika victor katika sura kitabu (Facebook)

anaendelea kuandika Victor IMANI YENU KWANGU IMEMFIKISHA MTOTO RUKIA MAHALI HAPA. NYANGAO- ST.WALBURG'S HOSPITAL
Bila kuchelewa alianza kufanyiwa usafi na mwili wake kupoza harufu mbaya ya awali. hapa akiwa amelowekwa ili maganda yatoke

KADILI MUDA ULIVYOZIDI AKAZIDI KUTIA MATUMAINI.
RUKIA anakunywa sana maji,bila kusita uwa anatamka mwenyewe maji.Muhudumu alisitisha zoezi la usafi na kumpatia maji.
 HAKIKA MUNGU NI MKUBWA RUKIA AKAWA HIVI
Baada ya usafi huu RUKIA akaacha kulalamika,naamini uchafu nao ulikuwa si sehemu ya mateso.
                                                        BABA WA RUKIA APATA FARAJA
Baada ya muhudumu kufanya kazi bila kinyaa wala woga na kubadilisha muonekano wa wa mtoto huyu,alipakatwa na baba yake kwa muda iliawekwe ktk nguo safi.

 Maumivu yenye matumaini ndani yake


RUKIA AMELAZWA WODI NO3 CHUMBA NO2 ST.WALBURG'S HOSPITAL NYANGAO-LINDI TZ. DUA,SALA NA IBADA ZAHITAJIKA SANA KWA MTOTO HUYU.MUNGU AMZIDISHIE PUMZI NA UMRI WA KUISHI HAPA DUNIANI
 HUDUMA ILIZIDI KUIMALIKA KWA MTOTO RUKIA
Hakika Mungu amepenyeza mkono wake ktk shida hii.

Unahitajika msaada wako ili Mtoto huyu azidi kupata nafuu zaidi unaweza kutuma kwa akakunti hizo chini
M PESA 0755 754494
TIGO 0715 754494