Pages

Monday, January 2, 2012

Wafa Dar es Salaam wakiogelea

WATU wawili wamekufa maji jijini Dar es Salaam, wakati wakiogelea katika fukwe za Bahari ya Hindi katika Wilaya ya Temeke wakati wakisherehekea sikukuu za Mwaka Mpya na mpaka sasa miili yao bado haijaonekana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime alisema kuwa watu hao wamekufa maji baada ya kupigwa na wimbi zito.


Alimtaja kijana wa kwanza aliyepoteza maisha kuwa ni Emmanuel Mwanyika (23), mkazi wa Kibada ambaye alikufa wakati akiogelea katika fukwe hiyo iliyopo eneo la Sunrise Beach Kigamboni.


Alisema kijana huyo wakati akiogelea na wenzake, ghafla alipigwa na wimbi zito na kuzama na kunywa maji mengi na jitihada za kuutafuta mwili wake zinaendelea.


Mwingine ni Asha Ibrahim (14), mkazi wa Kibugumo ambaye alizama wakati akiogelea na wenzake katika eneo la Zabada Beach Kigamboni.


Misime alisema mwili huo pia haujapatikana na jitihada za kuutafuta zinaendelea. Wakati huo huo, mwendesha pikipiki Musa Ataharama (32), mkazi wa Mwembe Mtemvu amekufa papo

hapo baada pikipiki yake kumshinda na kugonga kingo za daraja.

Kamanda Misime alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 2.00 asubuhi katika barabara ya Kilwa eneo la daraja la Mto Kizinga na kuhusisha pikipiki hiyo yenye namba za usajili T 584

BUA Honda.

Alisema kijana huyo akiwa amempakia abiria wake Ali Musa (16), mkazi wa Mbagala Nzasa wakitokea Mbagala Rangi Tatu kwenda Kongowe walipofika maeneo hayo pikipiki ilimshinda

na kugonga kingo za daraja na kupinduka.

Katika ajali hiyo dereva huyo alikufa papo hapo na abiria wake kujeruhiwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kutibiwa katika hospitali ya Temeke na mwili wa marehemu

umehifadhiwa hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment