Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anasema serikali ya Libya imekubali mpango wa amani wa muungano wa Afrika ili kumaliza mapigano ya miezi miwili.
Bwana Zuma na viongozi wengine watatu wa Afrika walikutana na kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, mjini Tripoli siku ya Jumapili.Sasa wanaelekea katika eneo la Benghazi linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa nchi.Katika eneo la Ajdabiya,vikosi vinavyomuunga mkono Gaddafi vimewazidi nguvu waasi katika mapigano.
Shirika la Nato linasema ndege zake zimeshambulia vifaru 25 vya serikali katika siku ya Jumapili pekee.
Mpango wa muungano wa Afrika unatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja, kufunguliwa njia kwa ajili ya kusafirisha misaada na mazungumzo kufanyika kati ya serikali na waasi.
"muhimu kusitisha mapigano," alisema rais Zuma,baada ya mazungumzo yaliyochukua saa kadhaa.
Mfumo ambao mchakato huo utachukua mtaelezwa baadaye katika taarifa zetu,alisema Bwana Zuma.
Mwakilishi wa upinzani aliye Uingereza, Guma al-Gamaty,akizungumza na BBC amesema kuwa wataangalia kwa makini mpango huo wa muungano wa Afrika,lakini mpango wowote ulio na nia ya kumuacha Gaddafi au wanawe madarakani hautokubalika.
No comments:
Post a Comment