Pages

Thursday, July 23, 2015

HII IMEKUAJEEEE! !!


HII INAKUWAJE..................

Hiki ninaweza kuita ni kioja katika moja ya vioja vingi vilivyotokea katika mwaka huu.. hakika inasikitisha sana katika zoezi linaloendelea la uandikishaji la wapiga kura kwa mfumo wa Kielektroniki (Biometric Voters Registration) kuna vitu vya aibu vinafanyika vinavyodhalilisha nchi kuonekana kama kwamba ina uhaba mkubwa wa watu wenye maarifa ya kuweza kutenda kazi.

 kwa mfano; uchukuaji na uwekaji wa picha (pass port) tazama picha iliyowekwa katika hicho kitambulisho hauhitaji kuwa na elimu yoyote kujua hiyo picha haiko sawa na ukichukulia kwamba vitu vya msingi katika kitambulisho ni maelezo (Particulars), saini na picha (Passport size) sasa hiyo picha hapo ni passport, post card au ni kitu gani? Na hiki kitambulisho kinawakilisha vitambulisho vingi (si vyote) vilivyotolewa  katika hili zoezi kwa mtindo huo.Ukiachilia huo utendaji na hata muonekano wa nyuma ya picha (background) ni mbovu haupendezi hata kidogo

Mfano wa umuhimu wa picha angalia pale unapohitaji Hati ya kusafiria (Passport)  unapopewa vigezo ya picha wanayohitaji au hivi ni vigezo tumepewa na wazungu kwa kuwa matumizi ya Pass port ni ulimwenguni kote (worl wide)  na tusipofuata Raia wetu hawataweza kusafiri popote na hiki kitambulisho cha kura kina matumizi ya nyumbani tu basi bora liende..........

 Napenda kuwapongeza wale waandikishaji wa vitambulisho vilivyopita vya Analojia walikuwa na uweledi mkubwa waliweza kuandika (handwriting) na kutoa picha kwa ukubwa unaostahili kuliko hawa wa kidigitali wanaofanya kazi katika kipindi hiki ambao wengine walikuwa hawajahi kukutana na Kompyuta lakini kwa maelekezo na mafunzo ya saa moja tu wanaingia kwenye zoezi kubwa kama hili.

Hivi tatizo ni nini? .................. Au ni wivu unanisumbua!!... naomba niishie hapo niachie wadau kuchangia kwa mustakabali mzuri wa nchi yetu.



No comments:

Post a Comment