Pages

Monday, November 24, 2014

Temeke: Wapinga Fedha za Miradi ya Maendeleo kuhamishwa kwenye maeneo yao na kupelekwa kwingine


MGOGORO mkubwa wa kubadilishwa kwa miradi ya maendeleo katika baadhi ya Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, umeibuka katika kata hizo baada ya viongozi wa vijiji na Kata kudaiwa kurubuniwa na madiwani wenzao na kupeleka miradi hiyo katika maeneo mengine.
Wameitupia lawama Halmashauri hiyo kwa kujiita Halmashauri mama na kuzuia baadhi ya miradi na fedha zinazopaswa kutumiwa na baadhi ya Kata kwa maendeleo ya jamii.
Baadhi ya miradi inayolalamikiwa ni pamoja na ule wa kutaka wakopeshwe fedha za kuanzisha mradi wa ufugaji kuku utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 21, kwa kila kata – katika kata zote wanaolenga kuwasaidia vijana ambao hawana kazi za kujiajiri wenyewe.
Pia wamelalamikia hatua serikali kushindwa kutenga bajeti ya kutengeneza stendi ya mabasi ya kubeba abiria ya katika Kituo cha (Tandika) zinazotoka katika katika maeneo mbalimbali ya jiji kutokana na kukosekana kwa sehemu maalumu ya kuegesha magari ya abiria.
Taarifa ambazo FikraPevu imezikusanya kutoka vyanzo kadhaa vya habari zimebainisha kuwa, awali suala hilo lililalamikiwa na abiria pamoja na wazawa wa eneo hilo kutokana na adha ya usumbufu wanaoupata nyakati za mvua.
Wanunuzi wanaofika katika soko la Tandika ni miongoni mwa watu wanaokutana na kadhia hiyo na kwamba kuwepo kwa magari hayo husababisha changamoto kwa abiria ambao hawaelewi sehemu maalumu zinapopatikana daladala za kuelekea katika maeneo mengine.
Daladala-Tandika-Stand
Eneo la soko la Tandika linalolalamikiwa kuwa limetelekezwa na serikali bila kuwa na kituo cha magari ya abiria (daladala) tofauti na kile cha Temeke Mwisho.
Inaelezwa kuwa kupitia viongozi wa Kata na vijiji waliomba fedha katika Halmashauri hiyo za zaidi ya shilingi milioni 150 kwa ajili ya ujenzi huo hadi ukamilike na kwamba cha kushangaza wameambiwa kuwa bajeti ya fesha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya mradi wa kuku pamoja na mradi huo kwa sasa hazipo licha ya kuwa awali ilikubaliwa na baraza la madiwani kuwa zitengwe kwa ajili ya kazi hizo.
“Tumeambiwa fedha zilizokuwa zinatakiwa kutolewa kwa ajili ya miradi yetu pamoja na hizi za stendi zimepelekwa kwenye ukarabati wa nyumba za watumishi wa serikali ikiwemo milioni 40 zitatumika kukarabati nyumba ya Mkurugenzi, fedha inayodaiwa kuwa ni kubwa kuliko gharama ya matengenezo” kilieleza chanzo cha FikraPevu.
Wamesema “Vijana wengi waliopo vijijini hawana ajira katika sekta rasmi na pia hawana mitaji kuendeleza miradi midogo ya kilimo, uvuvi au ufugaji sasa kwa vijana wa mijini, wengi wetu hatuna mitaji kama wale wa vijijini ni vyema wakatupatia fedha ambazo ni wajibu wao kutupatia kama vijana kwamaana tunajua zipo fedha zinazotengwa kwa ajili ya vijana na akina mama katika Halmashauri”.
Temeke-Bus-Stand
Sehemu ya Kituo cha mabasi ya abiria, Daladala cha Temeke Mwisho
Wamesema pamoja na mambo mengine wanaishangaa serikali kwa kuanza kuwapatia mbinu za kujiajiri kikamilifu kwa nia mbalimbali ambazo zilitolewa na Maofisa Maendeleo ya Jamii wa Kata wakati fedha hakuna.
Ofisi ya Afisa Habari wa Manispaa ya Temeke, imesema inachunguza madai hayo kujua ni fedha kiasi gani kilitengwa kwa ajili ya miradi hiyo na baadae italitolea ufafanuzi, huku FikraPevu ikiendelea kuwatafuta viongozi wa ngazi nyingine.
Chanzo: Fikrapevu

No comments:

Post a Comment