Pages

Saturday, October 18, 2014

KASHFA ZAMZIDI MISS TZ

Dar es Salaam. Kashfa imemwandama Miss Tanzania 2014, Sitti Mtevu baada ya vielelezo mbalimbali kuonyesha kuwa ameghushi umri.
Sitti katika fomu zake alijaza ana miaka 18, kitendo ambacho kimewashtua watu wengi na kuanza kufuatilia taarifa zake na kubaini kuwa kumbe ana miaka 25.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, mrembo huyo aliyetokea Kanda ya Temeke hakuwa na sifa za kushiriki mashindano kwa vile tayari alishavuka umri uliowekwa kikanuni na waandaaji wa shindano hilo.
Sifa za mshiriki wa Miss Tanzania, anatakiwa awe na umri wa miaka 18 hadi 23, awe raia wa Tanzania, awe hajaolewa, awe na ufahamu wa kutosha wa kujieleza, awe hajazaa, asiwe mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari.
Pia, asiwe ameshiriki mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi yoyote zaidi ya mara moja kwa mwaka husika, maana yake hairuhusiwi kushiriki mara mbili katika mwaka mmoja. Lugha inayotumika ni Kiswahili na Kingereza.
Lakini, katika hali ya kushangaza, licha ya mrembo huyo kukiuka masharti hayo, alitangazwa kuwa Miss Tanzania mwaka huu, ushindi ambao umezua mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiponda ushindi wake na wengine wakienda mbali na kudai mrembo huyo ana mtoto.
Mastaa mbali mbali wame
toa matamko yao kwenye mitandao ya kijamii wakiponda ushindi huo na kuilaumu Kamati ya Miss Tanzania kuvurunda.
Mwanamitindo Martin Kadinda alisema: “Uncle Lundenga nakuheshimu na ninakuamini, lakini katika hili sikuungi mkono.”
Mtayarishaji wa kipindi cha Diaspora, Jestina George alisema:
“Jamani eee uongo kila mtu anadanganya na makosa wote tunafanya mimi bado nawalaumu viongozi wa Miss Tanzania maana naamini asilimia 100 walilijua hili toka mwanzo. Sitti mama pole.”
Akizungumzia suala hilo, mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga alisema: “Ni changamoto kubwa, lakini naamini ndio kukua kwa mashindano, mwaka jana na juzi walisema shindano limedoda, mwaka huu wanalizungumzia wiki nzima, acha watu waseme ni upepo tu utapita.”
Meneja wa Redd’s, wadhamini wa mashindano hayoilo, Victoria Kimaro alisema: “Kwa kweli maneno yamekuwa mengi, ya kweli na uongo, lakini naamini mengi ni ya uongo, siku yoyote kuanzia sasa Sitti atazungumza.

No comments:

Post a Comment