Mdau Said Akida akijiandaa kuingia old trafford kuangalia mechi kati Man U na Hull City jana
Sunday, November 30, 2014
Saturday, November 29, 2014
RAIS KIKWETE AWASILI DAR
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa abiria wakati ndege aliyopanda ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndegewa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Bw. Rashid Othman baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere aliyefika kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo.
Dua ilisomwa na viongozi mbalimbali wa dini baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza kuongea na wanahabari mara tu alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kadi ya pole toka kwa mjukuu wake Aziza Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa kwa furaha na mwanaye Khalifa Jakaya Kikwete wakati alipowasili Ikulu leo akitokea nchini Marekani kwa matibabu.(Picha na IKULU).
HELKOPTA YA MALIASILI YAANGUKA NA WANNE WAFARIKI
Helkopta hiyo ilivyo haribika vibaya
Miili ya watu waliokuwemo kwenye helkopta hiyo ikiwa imekandamizwa na mabaki ya chopa hiyo.
Helkopta aina ya Chopa iliyoanguka maeneo ya Kipunguni B Ukonga jijini Dar es Salaam, leo asubuhi na kuua watu wanne waliokuwemo akiwa ni rubani pamoja na askari watatu.
Watu wa usalama wakiwa eneo la tukio.
Sehemu ya Wananchi wakiwa eneo la tukio
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Kampanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaa, Kamishna Suleiman Kova wakiwa eneo la ajali. Picha ndogo ni Mrakibu wa Polisi Capt. Kidai Senzala enzi za uhai wake
---
HELKOPTA ya wizaya ya Maliasili na Utalii iliyo tolewa msaada kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet na kupokelewa nchini na Waziri wa Maliasili na Utalii June 14, 2014 jijini Dar es Salaam imepata ajali na kuua watu wanne hii leo.
Thursday, November 27, 2014
Escrow Njiapanda, wabunge wagawanyika
Dodoma. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo jana alipangua hoja zilizotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuacha wananchi njia panda kwa kutokuelewa nani anasema ukweli kati yake na kamati hiyo, inayoongozwa na Zitto Kabwe.
Juzi, kamati hiyo ya Zitto iliwasilisha ripoti yake kuwa imethibitisha kuwa Profesa Muhongo amekuwa mara kwa mara akilipotosha Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha za umma.
Kamati hiyo ilieleza kuwa imebaini kuwa Profesa Muhongo ndiye aliyekuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Singh Sethi na James Rugemalira tena katika ofisi ya umma na pengine hilo ndilo lilikuwa sababu ya upotoshaji.
Akiwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu hoja hiyo, Profesa Muhongo alianza kupangua hoja moja baada ya nyingine ingawa katika mjadala wa baadaye, zilihojiwa na wachangiaji wengine waliohoji uhalali wa vielelezo alivyotoa.
Kutaifisha mitambo
Jana, alieleza kuwa pendekezo la Kamati ya PAC kutaka mitambo ya IPTL itaifishwe si sawa kwa kuwa kulingana na mkataba wa PPA kati ya Tanesco na IPTL, majukumu ya IPTL yalikuwa ni kujenga, kumiliki na kuendesha (Build, Own and Operate – BOO). Hivyo, kutaifisha mtambo huo ni kukiuka makubaliano katika mkataba wa PPA wa Mei 26, 1995.
“Ukiukwaji wa aina hii ukitokea unaweza kuingiza Serikali katika mgogoro mkubwa ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kwenye Mahakama za kibiashara za kimataifa. Aidha, utaifishaji wa miradi ya uwekezaji binafsi itakuwa ni njia ya kufukuza wawekezaji.”
Gharama za uwekezaji
Kuhusu taarifa ya kamati ya PAC kwamba mwaka 2004 Tanesco ilifungua shauri katika Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Kiuwekezaji (ICSID 2) kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya gharama za uwekezaji, Profesa Muhongo alisema suala hilo si kweli.
Alifafanua kuwa Tanesco haijawahi kufungua shauri lolote ICSID ya London au Mahakama yoyote dhidi ya Benki ya Standard Charterd kupinga kiasi kikubwa cha Capacity Charge kama inavyoelezwa na PAC.
“Shauri la ICSID 2 lilifunguliwa Oktoba 31, 2010 na Standard Chatered Bank Hong Kong (SCBHK) kwa ajili ya kudai malipo ya deni ililonunua kutokana na mkopo uliotolewa na mabenki ya ushirika ya Malaysia kwa IPTL. Wahusika katika shauri hilo la ICSID 2 ni SCBHK na Tanesco na wala siyo Tanesco na IPTL.”
Alisema Februari 12, ICSID ilitoa uamuzi kuhusiana na shauri la SCBHK na Tanesco na kuwashauri wakae kukokotoa upya malipo ya Capacity Charge. Hata hivyo, ilikuwa vigumu kwa pande hizo kutekeleza uamuzi huo kutokana na pande hizo kutokuwa na mkataba wa kibiashara baina yao.
“Vilevile, kupitia shauri la madai Na. 60/2014, lililofunguliwa na IPTL katika Mahakama Kuu ya Tanzania Aprili 4, ilizuia utekelezaji wa maelekezo hayo,” alisema.
Uwekezaji wa Sh50,000
Profesa Muhongo alisema kuhusu madai ya PAC kuwa mtaji wa uwekezaji katika mtambo wa IPTL ni Sh50,000 na kwamba huo ndiyo ungetumika kukokotoa gharama za uwekezaji ili kulipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa, maelezo hayo siyo sahihi.
Alisema ukweli ni kwamba kutokana na uamuzi ya ICSID 1 ya Julai 12, 2001, gharama za ujenzi wa mtambo wa Tegeta ni Dola za Marekani 127.2 milioni kama ilivyoelezwa na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Profesa Muhongo alisema katika taarifa hiyo, pia imeelezwa kuwa ilikubalika kuwa uwiano wa deni na mtaji utakuwa 70:30 ikiwa na maana kwamba, deni ni Dola za Marekani 89.04 milioni na mtaji ni Dola za Marekani 38.16 milioni na kwamba uamuzi huo haujabadilishwa na Mahakama yoyote au mtu yeyote.
“Tunakubaliana kwamba fedha iliyopokewa kutoka mabenki ya ushirika ya Malaysia kama mkopo ni Dola za Marekani 85.86 milioni ambazo kati ya Dola za Marekani 105 milioni zilizokuwa zimeidhinishwa,” alisema na kuongeza:
“Swali la kujiuliza je, mtambo huo ulikamilikaje kwa gharama ya Dola za Marekani 85.86 milioni, huku gharama halisi ya ujenzi wa mtambo wa Tegeta ikawa Dola za Marekani 127.2 milioni?
Alisema ni dhahiri kwamba kuna matumizi ya zaidi ya Dola za Marekani 38.16 milioni ambazo pia zimetumika kwenye uwekezaji na kwamba Kamati ya PAC haikuonyesha fedha hizo kuwa sehemu ya uwekezaji.
PAP na umiliki wa hisa saba
Profesa Muhongo alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za Brela za Desemba 31, 2013, uhamishaji wa hisa saba za Mechmar katika IPTL kwenda PAP ulisajiliwa hapa nchini. Kwa maana hiyo, PAP ni mmiliki wa asilimia 70 za IPTL.
Alisema Kamati ya PAC imeeleza kuwa PAP siyo mmiliki halali wa hisa saba za Mechmar katika IPTL lakini kamati imethibitisha kwamba nyaraka za mauziano kati ya Mechmer na Piper Link zilipokewa na Harbinder Singh Sethi ambaye pia ndiye mmiliki wa PAP.
“Kwa uthibitisho huo, kamati inakubali kuwa hisa za Mechmer katika IPTL zinamilikiwa na PAP,” alisema Profesa Muhongo.
Akana kuwa dalali
Profesa Muhongo alisema taarifa ya Kamati ya PAC kwamba yeye ndiye aliyekuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Harbinder Sethi na James Rugemalira siyo sahihi kuwa tangu Novemba 9, 2011, Rita iliitisha mkutano na kuwakutanisha wadau wote wa IPTL wakati yeye alikuwa hajateuliwa kwenye wadhifa huo.
“Mimi kama ni dalali, udalali wangu ni kupeleka umeme vijijini. Mimi kama ni dalali udalali wangu ni kusaidia wachimbaji wadogo wa madini na kupeleka Watanzania kusoma masters (shahada ya pili) duniani kote.”
Serikali kutokuchukua tahadhari
Waziri alisema Kamati ya PAC, imeeleza kuwa Serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha dhidi ya madai mengine yanayoweza kujitokeza kabla ya kutolewa kwa fedha kutoka akaunti ya escrow kitu ambacho alidai si kweli.
Profesa Muhongo alisema kinga iliyochukuliwa inakidhi matakwa ya kisheria na imezingatia athari yoyote ambayo ingeweza kutokea baadaye kutokana na kutolewa kwa fedha katika akaunti ya escrow.
“Kwa hiyo, siyo kweli kwamba Serikali haikuchukua tahadhari kama ilivyodaiwa na PAC.”
Madai ya Sh321 bilioni
Profesa Muhongo alisema hoja ya PAC kwamba imejiridhisha kuwa madai ya Tanesco ya Sh321 bilioni yana uhalali japo usahihi wake utapatikana baada ya kutekelezwa kwa uamuzi wa ICSID 2 na Tanesco na IPTL kukubaliana kiwango sahihi cha Capacity Charge haina nguvu.
“Madai ya kwamba Tanesco inaidai IPTL Sh321 bilioni msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Sh50,000 kwa wakati huo. Dhana hii ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani 38.16 milioni ziliwekezwa kwenye mradi wa Tegeta,” alisema.
Profesa Muhongo alisema Bodi ya Tanesco imekana kuyatambua madai hayo ya Sh321 bilioni... “Kimsingi hata vitabu vya hesabu vya Tanesco ambavyo vimekuwa vikikaguliwa na CAG, havionyeshi kuwapo kwa deni hilo.”
Tuesday, November 25, 2014
MAHAKAMA KUU YAZUIA MJADALA WA ESCROW
Jopo la majaji watatu wa mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam chini ya jaji Radhia Sheikhe limezuia mjadala wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow hadi hapo hoja ya msingi ambayo ipo mahakamani itakapofanyiwa kazi.
Jopo hilo lililokuwa likiongozwa na Mh Radhia Sheikhe wameagiza kutofanyika kwa mjadala wotote kuhusu ripoti ya CAG huko bungeni na kuongeza kuwa majadiliano hayo yanaweza kufanyika baada ya shauri la msingi kupatiwa ufumbuzi.
Awali akizungumza na ITV mwanasheria wa IPTLl wakili Joseph Makandege amesema wamefikisha shauri hilo namba 50 katika mahakama hiyo wakitaka vifanyike vitu viwili kwanza kupata tafsiri sahihi ya kisheria kuwa kama kitendo kilichofanywana ofisi ya CAG kufanya ukaguzi katika akaunt za Escrow kama ni sahihi akaongeza kuwa wao wanachoamini ni kuwa kwa sababu jambo hilo lilikuwa limekwisha amuliwa kisheria mahakama na kwa kutolewa kwa hukumu kulikuwa hakuna haja tena na bunge kuagiza uchunguzi ufantike.
Aidha mwanasheria huyo akaongeza kuwa siyo kwamba hawataki jambo hilo kujadiliwa bali wanataka taratibu zifuatwe ili kuweza kufiki mwafaka wa kina katika jambo hilo mwanaasheria huyo akaongeza kuwa mbali na kupata tafsiri hiyo ya kisheria pia wanaiomba mahakama kulitaka bunge kusitisha mpango wake wakujadili tarifa ya CAG hadi tafsiri ya kina ipatikane.
Mwanasheria huyo pia akasema kuwa wao wanaona kama likijadiliwa haki haitaweza kutendeka kwa sababu wao kama IPTL hawana mwakilishi bungeni na hivyo maamuzi yatafanyika upande mmoja.
Kwa upande wa jopo la wanasheria wa serikali wakiongozwana Obadia Kaimela wameiomba Mahakama kuwapa muda wa kuweza kuwasiliana na baadhi ya watu ama taasisi zinazohusishwa na jambo hilo ili kuweza kupata muda wa kutosha kutoa utetezi wao.
Kutakana na hali hiyo imeamuliwa kuwa bada ya kukamilika kwa taribu zote kesi ya msingi ikiwemo uwasilishwaji wa viapo kesi ya msingi itanza kusikilizwa Desemba 2 mwaka huu.
Monday, November 24, 2014
Temeke: Wapinga Fedha za Miradi ya Maendeleo kuhamishwa kwenye maeneo yao na kupelekwa kwingine
MGOGORO mkubwa wa kubadilishwa kwa miradi ya maendeleo katika baadhi ya Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, umeibuka katika kata hizo baada ya viongozi wa vijiji na Kata kudaiwa kurubuniwa na madiwani wenzao na kupeleka miradi hiyo katika maeneo mengine.
Wameitupia lawama Halmashauri hiyo kwa kujiita Halmashauri mama na kuzuia baadhi ya miradi na fedha zinazopaswa kutumiwa na baadhi ya Kata kwa maendeleo ya jamii.
Baadhi ya miradi inayolalamikiwa ni pamoja na ule wa kutaka wakopeshwe fedha za kuanzisha mradi wa ufugaji kuku utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 21, kwa kila kata – katika kata zote wanaolenga kuwasaidia vijana ambao hawana kazi za kujiajiri wenyewe.
Pia wamelalamikia hatua serikali kushindwa kutenga bajeti ya kutengeneza stendi ya mabasi ya kubeba abiria ya katika Kituo cha (Tandika) zinazotoka katika katika maeneo mbalimbali ya jiji kutokana na kukosekana kwa sehemu maalumu ya kuegesha magari ya abiria.
Taarifa ambazo FikraPevu imezikusanya kutoka vyanzo kadhaa vya habari zimebainisha kuwa, awali suala hilo lililalamikiwa na abiria pamoja na wazawa wa eneo hilo kutokana na adha ya usumbufu wanaoupata nyakati za mvua.
Wanunuzi wanaofika katika soko la Tandika ni miongoni mwa watu wanaokutana na kadhia hiyo na kwamba kuwepo kwa magari hayo husababisha changamoto kwa abiria ambao hawaelewi sehemu maalumu zinapopatikana daladala za kuelekea katika maeneo mengine.
Eneo la soko la Tandika linalolalamikiwa kuwa limetelekezwa na serikali bila kuwa na kituo cha magari ya abiria (daladala) tofauti na kile cha Temeke Mwisho.
Inaelezwa kuwa kupitia viongozi wa Kata na vijiji waliomba fedha katika Halmashauri hiyo za zaidi ya shilingi milioni 150 kwa ajili ya ujenzi huo hadi ukamilike na kwamba cha kushangaza wameambiwa kuwa bajeti ya fesha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya mradi wa kuku pamoja na mradi huo kwa sasa hazipo licha ya kuwa awali ilikubaliwa na baraza la madiwani kuwa zitengwe kwa ajili ya kazi hizo.
“Tumeambiwa fedha zilizokuwa zinatakiwa kutolewa kwa ajili ya miradi yetu pamoja na hizi za stendi zimepelekwa kwenye ukarabati wa nyumba za watumishi wa serikali ikiwemo milioni 40 zitatumika kukarabati nyumba ya Mkurugenzi, fedha inayodaiwa kuwa ni kubwa kuliko gharama ya matengenezo” kilieleza chanzo cha FikraPevu.
Wamesema “Vijana wengi waliopo vijijini hawana ajira katika sekta rasmi na pia hawana mitaji kuendeleza miradi midogo ya kilimo, uvuvi au ufugaji sasa kwa vijana wa mijini, wengi wetu hatuna mitaji kama wale wa vijijini ni vyema wakatupatia fedha ambazo ni wajibu wao kutupatia kama vijana kwamaana tunajua zipo fedha zinazotengwa kwa ajili ya vijana na akina mama katika Halmashauri”.
Sehemu ya Kituo cha mabasi ya abiria, Daladala cha Temeke Mwisho
Wamesema pamoja na mambo mengine wanaishangaa serikali kwa kuanza kuwapatia mbinu za kujiajiri kikamilifu kwa nia mbalimbali ambazo zilitolewa na Maofisa Maendeleo ya Jamii wa Kata wakati fedha hakuna.
Ofisi ya Afisa Habari wa Manispaa ya Temeke, imesema inachunguza madai hayo kujua ni fedha kiasi gani kilitengwa kwa ajili ya miradi hiyo na baadae italitolea ufafanuzi, huku FikraPevu ikiendelea kuwatafuta viongozi wa ngazi nyingine.
Chanzo: Fikrapevu
NI IMANI TU!SUPU YA PWEZA,KARANGAMUHOGO MBICHIHAVIONGEZI URIJALI
ULAJI wa supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na vyakula hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Dk Cuthbert Maendaenda wakati akitoa mada yake katika semina ya wahariri iliyofanyika mkoani Morogoro iliyojadili nafasi ya wanaume katika kuleta mabadiliko katika jamii juu ya afya ya uzazi na ujinsia.
Dk Maendaenda ambaye alikuwa akijibu maswali pia kuhusiana na dhana hiyo iliyozoeleka kuhusu nguvu ya supu ya pweza, alisema ipo haja ya wanaume kuangalia sababu za kudorora kwa uwezo wao na kufanya marekebisho badala ya kudhani kwamba kuna dawa kutoka katika vyakula hivyo.
Miji mingi nchini kwa sasa nyakati za jioni kuna supu ya pweza na mauzo ya karanga mbichi ambao wauzaji wamekuwa wakinadi kama msaada wa kurejesha heshima katika ndoa.
Alisema ufanyaji mapenzi unaathirika na vitu vingi na jamii lazima kuangalia ukweli huo ili kuwa na watu wanaojiamini katika mapenzi na wale ambao wanamatatizio kupata ushaudi wa kidaktari.
Mwezeshaji huyo kutoka Taasisi ya sweden inayohusu haki za afya ya uzazi na ujinsia (RFSU) tawi la Tanzania ambalo linaendesha mradi wa TMEP wenye lengo la kuwaamsha wanaume kuwa chachu ya mabadiliko na hivyo kuwa na uelewa mpana kuhusu haki za ujinsia.
Alisema mwanaume mwenye afya zake hutoa kiasi cha manii cha CC 3-5 kinachotarajiwa kuwa na mbegu milioni 300-500 katika mshindo mmoja.
Alisema alisema vyakula vyote vinavyoliwa havina uhusiano na uimara au ujazo wa manii kwani, wanachokula watu ni vyakula vya kuongeza nguvu (wanga) na wala si protini inayotakiwa kusuka na mbegu.
Alisema kuna sababu nyingi zinazokwamisha furaha katika burudani ya kufanya mapenzi hukua kisema kwamba asilimia 60 za hali inatokana na tatizo la kisaikolojia, hamu iliyopitiliza ya kufanya mapenzi na kuonesha urijali mahusiano ya mwanaume na huyo anayetaka kufanya naye mapenzi na hasa hofu inayotawala kama atamudu kazi hiyo au la.
Aidha alisema sababu zingine ni za kitabibu zaidi, kama mgonjwa ya shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, kisukari, tatizo la homoni, mgongo na pia magonjw aya kuambukiza.
pamoja na kuzungumzia uwezo wa kufanya mapenzi, Daktari huyo pia alisema kwamba ukosefu wa mimba unahitaji kuchunguzwa kwa makini na wala si kumbebeasha lawama mwanamke.
Alisema watu wengi wanaofanyakazi katika maeneo yenye joto linalozidi kama waendesha magari makubwa ya safari, waendeshapikipiki,wapishi hujikuta na tatizo la uzazi kwa kuwa kitabia mfumo wa uzazi wa mwanaume unahitaji joto la chini kuliko la mwili na kupigwa kila mara na jiotoi la juu husababisha athari katika m fumo wa utengenezaji wa mbegu, idadi na uwezo wa kusafiri.
Pia alisema shauri la mtu kuwa na uume mdogo au mkubwa halina uhusiano na uwezo wa kuzaa wala kufurahisha kimapenzi na tatizo hilo linabaki kisaikolojia zaidi.
Wahariri hao wametakiwa kuwa makini katika kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali kwa kuwaambia ukweli na sio kung'ang'ania dhana dhaifu ambazo mwishoni mwa siku zinasababisha mtafaruku katika jamii, kuongeza magonjwa na kujiamini.

Thursday, November 20, 2014
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA ABAKWA DARASANI
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza A katika shule ya sekondari Ntunduru wilayani Sengerema mkoani Mwanza (jina limehifadhiwa, 14), amejeruhiwa vibaya sehemu za siri na shingoni kutokana na kukabwa shingoni wakati akibakwa ndani ya chumba cha darasa la shule hiyo mchana.
Tukio hilo lilitokea Novemba 15, mwaka huu mchana huku baadhi ya walimu wakidaiwa kuwapo shuleni baada ya mwanafunzi huyo kuitwa na mhitimu wa kidato cha nne ambaye anatuhumiwa kutenda kosa hilo.
Mwanafunzi huyo baada ya kuingia katika darasa hilo, alikutana na wanafunzi wawili wa kidato cha nne waliomkaba shingo na kumziba mdomo kisha kumvua nguo na kuanza kumtendea ukatili huo.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Carren Yunus, alisema watuhumiwa hao lazima wapatikane na kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Pamoja kuwasaka watuhumiwa pia lazima ufanyike uchunguzi wa kina juu ya usalama wa wanafunzi wa kike katika shule hii binafsi mchanganyiko ya bweni,” alisema Yunus.
Makamu mkuu wa shule hiyo, Bahati Charles, alithibitisha kutokea kwa tukio na tayari wanafanyia uchunguzi pamoja na vyombo vya dola.
“Ni kweli tukio hilo limetokea, ni tabia tu ya vijana wa leo kukosa maadili,” alisema Charles.
Polisi wilayani Sengerema imethibitisha kuwapo tukio hilo lenye jalada Seng/RB/2949/2014 ya Novemba 15, na kuwataja watuhumiwa ambao hata hivyo majina yao yanahifadhiwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlolowa, alithibitisha kutokea kwa tukio na hilo na kusema msako wa wahusika unaendelea.

SOURCE: NIPASHE
IPTL YAFIKIA PATAMU
Na Ojuku Abraham
MOTO wa ripoti ya upotevu wa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo imekabidhiwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe unatarajiwa kuwaka Novemba 27, mwaka huu, siku ambayo itasomwa na kujadiliwa bungeni baada ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na vigogo wengine kadhaa kuhojiwa.

Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilichotwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 300 katika hali isiyofahamika na wabunge wanataka ripoti hiyo iliyokabidhiwa kwa Kamati na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za…
Na Ojuku Abraham
MOTO wa ripoti ya upotevu wa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo imekabidhiwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe unatarajiwa kuwaka Novemba 27, mwaka huu, siku ambayo itasomwa na kujadiliwa bungeni baada ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na vigogo wengine kadhaa kuhojiwa.
MOTO wa ripoti ya upotevu wa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow, ambayo imekabidhiwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inayoongozwa na Zitto Kabwe unatarajiwa kuwaka Novemba 27, mwaka huu, siku ambayo itasomwa na kujadiliwa bungeni baada ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na vigogo wengine kadhaa kuhojiwa.
Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilichotwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 300 katika hali isiyofahamika na wabunge wanataka ripoti hiyo iliyokabidhiwa kwa Kamati na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, iwahoji wahusika wote kabla ya kuileta bungeni kwa mjadala.
Serikali kupitia kwa mwanasheria mkuu wake, Jaji Fredrick Werema na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, sambamba na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi wamekuwa wakisisitiza kuwa fedha hizo zilitolewa kwa kuzingatia hukumu ya Mahakama Kuu na kwamba haikuwa ya umma isipokuwa ni ya kampuni hiyo ya kufua umeme ya PAP.
“Katika hili, wabunge nao wamegawanyika, wapo wanaotetea madudu haya na wengine hawataki kabisa mchezo. Pale mwanzo ilionekana kama ni ajenda ya wapinzani, lakini kadiri siku zinavyokwenda, hata wabunge ndani ya chama tawala nao wanaonekana hawataki mchezo. Watu wamepania sana na huenda kukawa na mshikemshike mkubwa siku hiyo,” alisema mbunge mmoja wa CCM aliyekataa jina lake kutajwa.
“Inapofikia wakati wa kushughulikia wizi mkubwa kama huu, hatuna budi kuweka masilahi ya taifa mbele, hatuwezi kukubali fedha nyingi kama hizi zinaibwa wakati wananchi wanashindwa kupata mahitaji yao ya msingi kwa sababu ya ukosefu wa fedha, tunataka wote waliohusika katika jambo hili wawajibishwe na hatua zaidi za kisheria zichukuliwe,” alisema.
Kwa mara ya kwanza, skendo hiyo ya fedha iliibuliwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, akisema ana uthibitisho kwamba fedha hizo zilikwapuliwa na wajanja wachache, baada ya kuitafsiri kimakosa hukumu ya Mahakama Kuu chini ya Jaji John Utamwa, kwani hakuna popote ilipotaja Akaunti ya Escrow, akidai ingawa katika kikao kati ya Tanesco, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini walisema fedha zote za akaunti hiyo zipewe Kampuni ya PAP.
Vigogo wa serikali wanaotajwa kuhusika katika kashfa hiyo ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wake Eliakim Maswi, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu, Beno Ndullu, Mwanasheria Mkuu Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felchesmi Mramba.
Tarehe ya kujiandikisha kwa ajili ya chaguzi za Serikali za Mitaa
Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda amesema wananchi wanapaswa kujiandikisha katika daftari maalum la kupigia kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 23/11/2014 hadi tarehe 29/11/2014.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa wananchi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za vijiji, vitongoji na mitaa wanapaswa kuchukua fomu za kugombea kuanzia tarehe 16/11/2014 hadi tarehe 22/11/2014.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Bwana Luanda aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili waweze kupata fursa ya kushiriki katika kupiga kura ili kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa wanaowataka.
Alisema sifa za mtu anayestahili kujiandikisha kushiriki uchaguzi huo ni lazima awe raia wa Tanzania, mwenye umri wa miaka 18 au zaidi, mkazi wa eneo hilo na mwenye akili timamu.
Pia alisisitiza kuwa uandikishaji huo utafanyika katika vituo maalum vilivyoandaliwa ambavyo vipo katika majengo ya umma, isipokuwa sehemu ambazo hazina majengo hayo, uandikishaji utafanyika katika vituo maalum kutokana na makubaliano ya Msaidizi wa Uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa.
Bwana Luanda amesisitiza kuwa vituo hivyo vitafunguliwa saa 1:30 asubuhi na kufungwa saa 10:30 jioni.
Aidha alisema kuwa vyama vya Siasa vitaruhusiwa kuweka mawakala wao wakati wa uandikishaji wa wa wapiga kura lakini gharama za kuwalipa zitakuwa juu ya chama husika.
Kuhusu sifa za mtu anayetaka kugombea nafasi mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mtaa Mkurugenzi huyo alisema kuwa ni lazima awe mtanzania mwenye umri wa miaka 21 au zaidi na awe mkazi wa kudumu wa eneo husika.
Vile vile alisema kuwa wasimamizi wasaidizi wa kila kituo wanapaswa kubandika orodha ya wapiga kura tarehe 30/11/2014, endapo mkazi yeyote au chama cha siasa kitakuwa na pingamizi au maoni juu ya orodha hiyo basi awasiliane na msimamizi msaidizi wa uchaguzi ili kuweza kufanyia marekebisho na orodha ya mwisho itabandikwa siku tatu kabla ya uchaguzi.
Uchaguzi wa serikali za Mitaa Tanzania Bara umepangwa kufanyika disemba 14, 2014, ambapo wananchi watawachagua wenyeviti wa vijiji, vitongoji, Mitaa, Wajumbe wa Halmashauri za vijiji na Wajumbe wa Kamati za Mitaa.
Viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni pamoja na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji wasiopungua 15 na wasiozidi 25, wenyeviti wa Mitaa na wajumbe wa kamati za Mitaa wasioziidi 6 na wenyeviti wa vitongoji wa kila kitongoji.

BINTI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI YOMBO VITUKA
BINTI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI, APORWA FEDHA HUKO YOMBO VITUKA JIJINI DAR
Mwili wa marehemu aliyefahamika kwa jina moja la Betty baada ya kupigwa risasi leo asubuhi huko Yombo Vituka, Temeke jijini Dar es Salaam akiwa kwenye gari aina ya Toyota Pick Up mali ya Tunu Security na watu waliokuwa katika bodaboda.
Mtu asiyefahamika (mwenye simu katikati) akiwasiliana na ndugu wa marehemu Betty baada ya kufika eneo la tukio.
DADA aliyefahamika kwa jina moja la Betty ameuawa kwa kupigwa risasi leo saa mbili asubuhi maeneo ya Yombo-Vituka, Temeke jijini Dar es Salaam akiwa kwenye gari aina ya Toyota Pick Up mali ya Tunu Security.
Marehemu Betty ameuawa na watu waliokuwa kwenye bodaboda wakati akiwa kwenye gari la Tunu Security akitokea kituo cha mafuta kuelekea benki.
Watu hao waliokuwa kwenye bodaboda mmoja alimpiga dereva wa gari risasi ya mkononi alafu akampiga Betty risasi ya kichwani huku mlinzi aliyekuwa katika gari hilo akikimbia ambapo watu hao walichukua mfuko uliokuwa na pesa na kutokomea kusikojulikana.
Baadaye mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi na kupelekwa Hospitali ya Chang'ombe,Dar kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
(PICHA NA GPL)
Thursday, October 23, 2014
MKE AKIRI KUMSALITI MUMEWE MIAKA 7
SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya kulawiti na kutuma picha katika mitandao ya kijamii inayowakabili wakazi wawili wa Mbagala, Dar es Salaam, alidai kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mlalamikaji kwa miaka saba huku akiwa na mume wake ambaye ni mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo.
Sanifa Sadick alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi Saidi Mkasiwa kuwa mshitakiwa Erick Kasira (39) ni mume wake tangu mwaka 2006 na kwamba wana watoto wawili huku mshitakiwa wa pili, Juma Richard ni shemeji yake.
Alidai kwamba Agosti 23 mwaka huu, waliwasiliana na mlalamikaji huyo ili wakutane katika nyumba ya kulala wageni inayojulikana kama Maembe Bar & Guest House iliyopo Yombo Kiwalani kwa ahadi ya kusaidiwa Sh 100,000.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto, shahidi huyo alidai muda wa saa 7 mchana alimuaga mume wake kwamba anaenda kununua bidhaa za saluni.
Alidai kwamba alichukua usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda huku mlalamikaji akimuelekeza kwa njia ya simu.
Sanifa alidai kwamba wakati anaelekea Yombo kulikuwa na mwendesha pikipiki ambaye alikuwa anamfuatilia kwa nyuma hadi eneo hilo.
Alidai kwamba alimkuta mlalamikaji akiwa peke yake na kuagiza kinywaji baadaye walichukua chumba namba sita na kuingia ndani; baada ya muda mlango wa chumba hicho uligonjwa ndipo alimuona mumewe akiingia pamoja na vijana watatu.
‘’Sikuweza kuwatambua wote lakini hawakuwa na silaha zaidi ya simu. Mpenzi wangu aliulizwa na mume wangu kuwa anafanya nini na mimi, naye alimjibu kuwa asiniache kwani atampa gharama yoyote ndipo waliandikishiana kutoa Sh 500,000 ,’’ alidai Sanifa.
Alieleza mlalamikaji kuwa alikuwa na kompyuta na kwamba alimwambia Erick akae nayo hadi atakapompatia fedha hizo walizoahidiana.
Alidai kwamba alikuwa amejificha chooni na kusikia kwamba wanaume hao wanamtaka mlalamikaji afanyiwe kinyume na maumbile na kwamba walimvua nguo zote huku aliyekuwa mwendesha bodaboda akiwa anapiga picha.
Alidai baada ya tukio hilo alikimbilia nyumbani na kukuta simu aina ya Tecno nyumbani kwake na kuiweka laini yake baadaye dada yake alimtumia picha ikimuonesha mlalamikaji akiwa utupu.
Alieleza kwamba mlalamikaji alimpigia simu Erick na kumwambia aende akachukue fedha alizoahidi kutoa wakati akifumaniwa na mke wa mshitakiwa huyo na kwamba mshitakiwa huyo aliondoka pamoja na ndugu yake Richard.
Alidai walipofika Tandika, waliwekwa chini ya ulinzi na Erick alimpigia simu mkewe kumtaarifu kwamba amekamatwa na polisi naye alipofika aliwekwa chini ya ulinzi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 3 mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa.
CHANZO: Habari Leo

Subscribe to:
Posts (Atom)