ASASI ZA KIJAMII ZA TEMEKE ZAASWA
Waandishi
wa ripoti kutoka asasi zinazofanya kazi ya kupambana na vvu manispaa ya
temeke wakiwa katika mkutano wa robo ya tatu ya mwaka huu
Afisa
maendeleo ya jamii wa manispaa ya temeke ndugu John Bwana amezitaka
asasi zinazojihusisha na mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi katika
jamii ndani ya manispaa ya Temeke kuwasilisha ripoti zao za kila robo
katika mwaka katika vyombo husika serikalini.
Akizungumza na
waandishi wa ripoti wa asasi zaidi ya sitini katika ukumbi wa mikutano
wa shule ya msingi wailesi waiofika katika mkutano huo wa robo ya tatu
katika mwaka huu wa 2013 ndugu Bwana alisema " njia nzuri ya kujenga
mahusiano na mawasiliano mazuri baina ya asasi na serikali ni ni kwa
njia ya asasi kulazimika kuwasilisha ripoti za kazi zao serikalini kwani
ripoti hizo zitaisaidia serikali kujua asasi gani inafanya kazi, kwa
ukubwa upi na ina changamoto zipi
zinazoikabili na isitoshe sisi serikali tunaweza kuandaa mipango yetu ya
kiutekelezaji kulingana na taarifa tunazoletewa na inatusaidia pia
kutambua ukubwa wa tatizo au kupungua kwa tatizo pia itatusaidia
kutambua asasi za kiuzipa kipaumbele kwa kushirikiana nazo".
Wakati
huohuo asasi hizo katika kuchangia majadiliano kwenye mkutano huo
zimeeleza mafanikio katika kupambana na hali ya maambukizi ya vvu, kwani
wameweza kuwafikia watu wengi katika jamii kwa kuwapatia elimu ya
kutokupata maambukizi ya vvu kwa kutoendelea kufanya ngono zembe na kwa
wale wanaofanya biashara ya kuuza miili yao wamepatiwa elimu ya
ujasiliamali na kuanzishiwa huduma ya vikoba ili waweze kujiajili kwa
ajira iliyosalama kwa afya zao.
Katika ripoti zote zilizowasilishwa
na asasi ripoti ya asasi inayojulikana kwa jina la STAY AWARE NETORK
(SANA) yenye makao makuu yake sinza na inajihusisha na uzuiaji wa
maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kundi lililosahaulika la watu
wanaofanya mapenzi wenye jinsi moja inayofanana ndio iliyoleta msisimko
mkubwa kwa wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
Asasi hiyo ilikumbusha
jamii kuwa wwakati jamii inaweka vipaumbele vya mapambano ya vvu
inawasahau kundi ilo ambalo lipo kwenye jamii na limegawanyika katika
sehemu tatu kundi la kwanza ni la wanaume wanaopenda wanaume wenzao kwa
kuwageuza wake zao, kundi la pili ni la wanaume wanaopenda kugeuzana
wanawake kwa kufanya panzi kwa kugeuzana na kundi la tau ni la wanaume
wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao huku wakifanya mapeni na wanawake
kwa njia iliyokubalika.
Mtaalamu huyo alielezea maambukizi ya vvu
utokea kutokana na michubuko inayotokea kutokana na njia hiyo
inayotumika kutokuwa lengwa kwa kazi hiyo ya kujamiiana na usababisha
maambukizi kutokea na kusambaa kwa njia ya mtandao wa ngono zembe.
Na alimaliza kwa kusema hata wanawake wanaosagana pia upata maabukizi
kwa urahisi kwani hakuna kinga inayowazuia wasiambukazane vvu wakati wa
tendo ilo la ngono kwa njia ya kusagana
by: Denis Chakoma.