Monday, February 14, 2011
KINACHOWAVUTA WANAUME KUPENDA
MWANAMUME anapojikuta anampenda mwanamke humpenda kwa dhati na hali hiyo huwafanya wanaume wengi kujikuta wanapenda kupenda.
Mara nyingi wanaume wamekuwa wakitambuliwa kama jamii ya watu wasiokuwa na hisia zaidi ya kujijali wenyewe linapokuja suala la mapenzi.
Ukweli ni kwamba, tumbo la mwanamume hushituka kama mashine pale anapokuwa katika hatua ya kuwa na uhusiano wa kudumu na mwanamke.
Lakini, bado swali linabaki palepale ni kitu gani kinachoweza kumfanya mwanamume ampende mwanamke kwa moyo wake wote na kutulia naye?
Zaidi ya asilimia 60 ya wanaume huchukulia urafiki kama ni kitu muhimu katika uhusiano, lakini je ni aina gani ya mwanamke ambaye humvutia zaidi mwanamume?
Japokuwa hakuna ubishi kwamba suala la mvuto kwa mwanamume halitabiriki, lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo wanaume wengi hupendelea mwanamke anayempenda awe navyo.
Wanaume wengi huvutiwa na mwanamke ambaye ana hisia na kitu kingine zaidi yake, pamoja na kwamba wengi hupenda mwanamke anayewasifia na wenye uangalifu mkubwa, lakini huvutiwa zaidi na wanawake ambao huthamini kazi zao au ndugu zao.
Hali hiyo huwafanya wanaume watambue aina ya mwanamke waliyenaye uzuri wake, malengo yake binafsi, na uhuru wake na kuamua kama huyo ndiye mwanamke wanayetaka kuishi naye maisha yao yote.
Pia wanaume hupenda mwanamke ambaye hatumii muda wake mwingi kumganda, pamoja na kwamba kuna ukweli kuwa wapenzi hupenda kutumia muda wao mwingi pamoja lakini si mara zote hufurahia hali hiyo.
Wanaume hupenda kutumia muda wao wa ziada kwa kukutana na marafiki, kucheza michezo kama vile soka, kamari au kunywa, kutokana na hili kufurahia na kuvutiwa zaidi na mwanamke ambaye anawaelewa na hawabani mara kwa mara.
Wanaume pia huvutiwa na wanawake ambao ni watundu katika nyanja zote, yaani mwanamke ambaye hachoshi, kuanzia tabia yake, ufedhuli au jeuri yake, kujiamini kwake, haiba yake na ucheshi wake ambao unaonesha kuwa anaweza kuwa shujaa kidogo na jasiri wakati huo huo.
Ukweli ni kwamba wanaume wanapenda mwanamke ambaye atawapatia changamoto, ambaye wanaweza kushindana katika mambo mengi ya kimapenzi na kimaendeleo, lakini pia mwanamke ambaye anaweza kuwaongoza wakati mwingine.
Aidha wanaume pia hupenda wanawake ambao watawajali na kuwa nao karibu zaidi kiupendo kuliko hata ule upendo wa mama zao.
Wanawake mkumbuke kuwa, kila uhusiano unaguswa na suala la kupokea na kutoa, na wanaume moja kwa moja watamkimbilia mwanamke ambaye atawaonya pale wanapofanya mambo ya kijinga, atakayewafanya wanaonekane watanashati machoni mwa watu wengine pia atakayewasaidia kutoa maamuzi bila kuwapo kwa tatizo.
Hata hivyo mara nyingi wanaume hupenda kujiona kuwa wanafahamu wanachokifanya na kwamba hawahitaji msaada wowote, lakini wanawake ambao hujitolea kuwalinda na kuwasimamia huwa na nafasi kubwa katika mioyo ya wanaume wengi.
Pamoja na hayo, ikumbukwe kuwa suala la upendo na mapenzi hutegemea zaidi moyo wa mtu, pamoja na sifa hizo bado uchaguzi na uamuzi wa kupenda upo mikononi mwa mhusika.
sheby biboze.wabongousa.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment