Pages

Friday, June 27, 2014

KINYESI KERO TAZARA



 Kinyesi kinachotiririka kutoka gorofani kikiwa kimesambaa chini baada ya mifereji yake kuziba n'a kuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo

Thursday, June 26, 2014

KUSAFISHA UWANJA WA KIGODORO

Hali inavyokuwa katika maeneo yetu ya temeke katika kigoma cha kusafisha ua kwa ajili ya kigodoro.




JALALA LAZIDI KUVAMIA UWANJA

 uchafu unavyozidi kuvamia eneo la uwanja
 Kitendo cha Manispaa ya Temeke kuendelea kulifumbia macho suala la dampo la muda lililopo maeneo temeke mwisho limezidi kuwa kero ambapo kwa sasa limeanza kuingia katika uwanja wa michezo wa eneo hilo.

Monday, June 9, 2014

VICHOCHORO SASA MALI TEMEKE

 Katika hali isiyotarajiwa sasa baadhi ya vichochoro  vimetoka katika hali ya uchafu na kusafishwa kwa kukodishwa hali hiyo amikutana nayo mpiga picha wetu alipokuwa maeneo ya Tandika na Wailes



 baadhi ya vichochoro vinavyotumika kuuzia vyuma maeneo ya wailes

KINAOMBEKA


watoto waliokutwa maeneo ya tandika wakigawana askirimu

KERO YA MALORI BARABARA YA KILWA


Sasa imekuwa kama barabara ya malori usiwe na haraka ukapita kilwa road na foleni huanzia Sabasaba mpaka Jeshi la Uwokuvu, wahusika lifanyieni kazi hili suala.

KAKOSA NINI MSICHANA HUYU

Hii picha ikionyesha msichana wa miaka 13 akiwa amebeba ndoo tatu za maji je hili suala linaangaliwa vipi?

LORI LAVAMIA NYUMBA MTONI

 Gari iliyoacha njia na kwenda kuvamia makazi ya watu katika mzunguko wa Mtoni kwa Azizi Ally


Katika ajari hiyo haikuweza kuleta madhara kwa wananchi wa eneo hilo

Wednesday, June 4, 2014

MAJANGA DEREVA NA UTINGO WAJIIBIA MALI WALIZOKUWA WAKISAFIRISHA

                                                                                           

Kamanda  wa polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi kushoto akisalimiana na mwakilishi wa kampuni ya Dandu ambao lori lao limeteketezwa kwa moto.

(Francisblog)(FS)

Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa akionyesha mitumba  iliyohifadhiwa katika nyumba  moja Nyololo baada ya kufaulishwa na dereva na utingo wake kisha lori kuchoma moto.(Francisblog)(FS)

Mitumba  hiyo ikionekana kwa nje baada ya kujaa ndani ya nyumba hiyo kupita kiasi 

Safari ya kwenda  kubaini mali ya wizi iliyofanywa na kamanda wa polisi Iringa
 
RPC Iringa Ramadhan Mungi akiangalia  mitumba  iliyohifadhiwa porini baada ya  kuporwa 



Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akitoka  kushuhudia mabelo ya mitumba yaliyofichwa  porini kijiji cha Maguhani Mufindi 

kamanda wa  polisi Iringa Ramadhan Mungi akimwonyesha mmiliki wa nyumba iliyohifadhi  mali  hizo za wizi kulia na dereva wa gari hilo mbele lenye namba  T 185 CJM ambalo  ndilo lilikuwa likisomba mali  hizo za wizi kutoka katika  lori lililochomwa moto
 
Watuhumiwa wa  wizi wa mali  zilizokuwa  zikisafirishwa na lori la kampuni ya Dandu
 
Hili ndilo lori  lililokuwa na mali  hizo  chini kukiwa na ubichi wa mafuta  ya taa yaliyomwagwa ili  kulilipua lori hilo bila mafanikio

mwonekano wa lori hilo kwa ndani baada ya mali zote  kuhamishwa kwa  lengo la kuziiba 

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akionyesha  lori hilo mali ya kampuni ya Dandu ambalo limechomwa moto na dereva na utingo wake baada ya  kufaulisha mali zote kwa lengo la kuiba
 
Picha: Fransic blog 
 

WASHIRIKI MISS MBAGALA 2014

 Washiriki wa Miss Mbagala wakiwa katika ofisi za Global Publisher Bamaga Mwenge

Washiriki wa Miss Mbagala wakiwa katika picha ya pamoja kujiandaa na kinyanganyiro hicho kitakachokuwa june 7 ukumbi wa Dar Live

Picha: Global Publisher

WAUE-YA MH. TEMBA NA CHEGE YAKAMILIKA

 Baadhi ya vipande vya videovitakavyokuwepo katika nyimbo hiyo



Wanamuziki wa kizazi kipya wanaotoka kundi la TMK Wanaume Family, Chegge na Mhe Temba wanatarajia kuachia hewani wimbo wao mpya uitwao 'Waue' waliowashirikisha 'membaz' wa Mkubwa wa Wanawe.
Wasanii walioshirikishwa  ni Maromboso na YP ambao nao wanatokea 'ukoo' wa TMK Wanaume Family na Mkubwa na Wanae.
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe na Meneja wa wasanii hao, Said Fella 'Mkubwa' alisema  kuwa, wimbo huo utaachiwa 'audio' na video  muda wowote kuanzia sasa kwa kuwa kila kitu kipo tayari.
Mkubwa, alisema wimbo huo umerekodiwa katika studio zao za Mkubwa na Wanae chini na mtayarishaji, Shirko na video imefanywa na Adam Juma kupitia kampuni yake ya Visual Lab.
"Wasanii Temba na Chegge wamekamilisha kurekodi 'audio' na video ya wimbo wao uitwao 'Waue' walioimba na Maromboso na YP, na tunapanga kuachia kazi hiyo mda wowote," alisema.
Chegge na Mhe Temba wamekuwa wakitoa kazi za pamoja mbali na zile za binafsi za kila mmoja nje ya nyimbo za kundi lao la TMK Wanaume Family.

WAIZUNGUKA DUNIA KWA GARI WALIOTENGENEZA

 Raia wa Argentina wakiwa na gari lao walilotengeneza wenyewe kwa dhumuni ya kutembelea mabara tofauti duniani


Hapa gari likiwa lipo katika viwanja vya ndege vya JK kuanza safari ya kuizunguka Tanzania