Pages

Friday, April 11, 2014

VUNJA VUNJA INAYOENDELEA TEMEKE



Picha na 1-3 eneo la Kwa masangati ambalo kwa sasa limevunjwa na kuachwa kuwa wazi


 Picha na. 3-6 eneo la Bar Maarufu Matako Pub nalo limepitiwa katika bomoa bomoa hiyo
 Gulf maeneo ya wailes


Hivi ni baadhi tu ya maeneo yaliyovunjwa na manispaa ya Temeke kuacha maeneo yake wazi

MAANDALIZI YA MUUNGANO



Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wilaya ya Temeke wakiwa katika maandalizi ya sikukuu ya Muungano

Tuesday, April 1, 2014

LIDAKE TENA CHOZI LANGU

sehemu 1.
"mimi bolizozo pendazozo sioviozo nimekubari kumuoa jesca simon majuto hawee" "stop! Ilikuwa ni sauti toka kwa bi harusi ikafatiwa na kilio. Machozi nayo yakichukua nafasi yake kuonyesha gani uchungu umemshika. "Mchungaji naomba waambie baba na mama angu huyu sio chaguo langu simtaki chaguo langu ni" hakuweza kufanikiwa kumaliza kauli yake, ni kitendo cha bila kutalajiwa mle kanisani, akadondoka chini huku mpambe wake akishindwa kumzuia asianguke. Mwili wake ukajikuta ukipokelewa kwa sakafu nzuri ya kanisa. Kishindo kikubwa kikifata nyuma yake akabaki kalala huku fahamu zikiachana na mwili wake, akashindwa kutambua ni jambo gani linaendelea kanisani.
"jesca kwanini ujanikataa toka mwanzo mpaka leo kuniabisha ndani ya kanisa, jua hii sio yangu tu umeaibisha mpaka familia yangu". Kilio cha bwana harusi bolizozo ndio kikawakurupusha­­mpa­ka wale ambao walikuwa nje ya kanisa wakipiga soga. Ndani ya kanisa likazidi kupokea watu zaidi, sasa ikawa sio kuwa mashaidi wa ndoa bali mashaidi wa kilichoipata familia ya mzee pendazozo. Furaha yote ikawa imemezwa na kilio cha ndugu, wapambe, wapo waliolia kwa ajili ya bi harusi na wapo waliolia kwa ajili ya bwana harusi. Wapambe wakishirikiana na baadhi ya ndugu wa bi harusi wakageuka wahudumu katika kutoa huduma ya kwanza kwa bi harusi. Wakambeba kumpeleka kwenye gari ambalo liliandaliwa maalumu kuwabeba pindi wakipewa uhalali wa mume na mke mbele ya mtumishi wa mungu. Sasa likageuka gari la kubebea wagonjwa, mgonjwa mwenyewe hakiwa bi harusi. Mzee pendazozo mda wote alikuwa yupo kimya akizunguka huku na huku. Mara hatoe simu yake arudishe mfukoni ili mradi akili yake ikae bize. Hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua hanawaza jambo gani kichwani mwake. Moyoni mwake kulijengeka chuki, chuki iliyozaliwa baada ya mwanae pekee kuaibishwa. Chuki ikaanza kusambaa kwa kasi ndani ya nafsi yake mpaka ikaweza kumzaa mtoto ikampa jina kifo. Kifo kikawa kimeibeba akili yake yote sasa nani wa kukipokea kama si familia ya mzee simon majuto. Akajiapiza akili mwake lazima nilipize kisasi siwezi kuvumilia udhalilishaji kama huu.
Watu wakaanza kuondoka kwa vikundivikundi huku wajadiliana tukio lililotokea mda mfupi kanisani. Kanisa likabakiwa pekee na mchungaji tu wengine wakitawanyika.
***************
ndani ya shule ya sekondari ya kutwa ngerengere. Kijana dickson dionis ndio alikuwa hameamishiwa hapo kuja kusoma. Hiyo yote kutokana wazazi wake na ndugu zake kuaga dunia baada ya kupata ajari mbaya ya gari moshi mkoani dodoma. Maisha mapya ya shuleni mda mwingi yalimfanya hawe mnyonge. Mtu wa kupenda kushinda darasani. Juudi zake zote akizipeleka kwenye masomo. Kwani ndio mzazi pekee aliyebaki nahe duniani. Kauli kubwa ambao ilibaki kichwani mwake ambao ndio urithi toka kwa wazazi wake ni URITHI WA KWELI DUNIANI NI ELIMU. Ikawa ndio changamoto yake kuu katika masomo ya darasani pasipo kuchagua somo. "Samahan kaka naitwa jesca simon, je naweza kukaa hukanisaidia haya maswali" hakainua uso akamtazama, akajibu kwa kutikisa kichwa kutoka juu kwenda chini. Jesca hakutaka kupoteza mda akasogeza kiti wakaanza na maswali. Ni kengere ya mapumziko ndio iliwatenganishakuend­elea kufanya maswali. Wakaachana jesca akienda kupata chai anywe huku dickson akitafuta japo maji ya hamsini apate japo kulistua tumbo lake. Tumbo ambalo lilikuwa limeshinda kwa chakula cha jana mchana huku usiku akinywa maji akiweza kulala.
itaendelea

Mtunzi: Dee Dion