Pages

Wednesday, July 31, 2013

TSHIRT ZA MIA SABA SABINI SOKONI-WANAUME HALISI


Inakuaje watu wangu wa nguvu,mzigo wa tshirt ndio huo umeanza kutema na kwakuanza tu tumeanza na MIA SABA SABINI kma unavyoziona hpo na ni kwa bei ya sh 15 tu sio kma mjanja wa wanaume halisi si mbaya ukachangia chama kwa kuvaa tshrt zetu kwa anae hitaji number za simu ni 0718313258 na 0716138467 au unaweza kufika katika duka letu ambalo lipo mbagala mtaa wa mji mpya na utapewa cd moja bure yenye nyimbo za wanaume halisi

Saturday, July 20, 2013

UBIZE WETU UNAWALA WANETU

Na: Albert Sanga, Iringa.
Leo ngoja niweke kando kidogo masuala ya biashara na uajsiriamali; nigeukie moja ya jambo ambalo limekuwa likinigusa na kuniumiza sana kichwa-malezi ya watoto wetu kuanzia wakiwa wadogo mpaka wanapofikisha umri wa kujitegemea. Gazeti la The African linalotolewa na New Habari (2006) Limited; la jumatano ya tarehe 5, Agosti, 2009 limewahi kuripoti habari ya watoto wawili wa kiume;( mmoja miaka 7 mwingine miaka 9 ) walioshirikiana kumlawiti mtoto mwenzao wa kiume (wa umri wao) na kusababisha majeraha na maumivu sehemu zake za siri. Tukio hilo lilitokea Mbezi Temboni Kwa Msuguli jijini Dar es Salaam. Wazazi wa watoto waliotuhumiwa walipohojiwa walikiri kuwa hawakuwa na habari ikiwa watoto wao wanaweza kuwa na tabia za kifirauni namna hiyo! Habari hiyo imenipa tafakari ya kina nikiiunganisha na tukio la hivi karibuni nililolishuhudia; ambapo mama mmoja alikuwa akimuadhibu vikali mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka saba. Sababu ya adhabu hiyo ni baada ya mama huyo kumsikia binti yake huyo mdogo akiigiza sauti za watu wanaofanya mapenzi. Mtoto huyu mdogo alieleza kuwa sauti hizo ameziiga kutoka kwenye mkanda wa ngono wa video, ambao huwa wanaangalia wakiwa na dada yake (house girl) mama na baba wakiwa
kazini!
Kadiri dunia inavyozidi kubadilika katika mifumo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa npyo ambavyo watu wanazidi kusongwa na mambo mengi mno ili kukabiliana na mabadiliko hayo. Na kwa kadiri "ubize" unavyozidi kupanda npyo na athari mbalimbali zikiwemo za kijamii zinavyozidi kuongezeka. Moja wapo ya eneo hili la kijamii ni malezi ya watoto wetu wadogo.
Kuna maeneo matatu ambayo kutokana na yalivyo yanaua kabisa baadae njema za kizazi cha watoto wetu (future). Eneo la kwanza ni malezi ya watoto mikononi mwa wafanyakazi wa ndani, "house girls"; la pili ni shule za bweni ambazo zinachukua watoto wadogo na la tatu ni vituo vya watoto yatima. Katika makala haya nitaeleza maeneo mawili ya kwanza nikiliacha hili la tatu la vituo vya watoto yatima, ambalo linahitaji mjadala wa makala inayojitegemea.
Umekuwa ni mtindo maarufu sana nyakati za sasa kwa wazazi wengi miezi michache baada ya kujifungua kuwaacha watoto wao mikononi mwa "ma-house girls" ili wawalee. Na tena ni kawaida sana kuona mtoto hadi anafikisha miaka mitano akawa amelelewa na wafanyakazi wa ndani hata watano, ambao wote wameshafukuzwa kutokana na tabia mbalimbali. Hebu tutazame mfano huu.
Unaweza kuona mama mwenye nyumba anamfukuza binti wa kazi kutokana na tabia yake ya uvivu na kisha anamtafuta mwingine bila kujua kuwa ana tabia ya uzinzi. Wengi wa akina mama huwa wanakuja kushtukia kuwa wakati mwingine mabinti hawa hutembea hata na waume zao! Huyu akifukuzwa anampata mwingine ambaye nae unaweza kuona ana tabia ya uchafu, umbea, uvivu na mengine mabaya.
Saikolojia ya malezi ya watoto inabainisha kuwa ubongo wa mtoto mdogo huwa mwepesi sana kunakiri vitu na tabia mbalimbali kwa haraka sana. Anayemlea akiwa na hulka za uzinzi, udokozi, uvivu ama matusi mtoto ataiga na kuwa hivyo. Watoto wengi siki hizi wanakua wakiwa tayari ni makahaba, wezi, wakatili, wasio na nidhamu na wenye kila tabia zinazokatisha tamaa.
Mtaalamu na mwandishi wa mausuala ya saikolojia na ukuaji wa kiroho, M. Scott ameandika katika kitabu chake cha "The Road less traveled" kuwa wazazi wanafanya kosa kubwa sana la kutotumia muda wa kutosha kimalezi kwa watoto wao wakiwa wadogo. Kosa hili analiita "sins of the father".
Mtaalamu huyu anasema dhambi hii ya baba husababisha mtoto awapo mkubwa kuandamwa na upweke, kutojikubali, kukosa ulinzi wa kiroho (insecurity) hali ambayo hupelekea watu kuhamishia hali hiyo katika utafutaji usio halali wa mali, ukatili, kuheshimiwa na kulazimisha mapenzi. Inadaiwa watoto waliokosa malezi mazuri kutoka kwa baba zao huwa wakatili sana kwa wake zao pindi wakioa na kama wakishika nafasi za kisiasa mara nyingi huwa madikteta.
Makala haya hayakatai uwepo wa wafanyakazi wa ndani ambao wananidhamu na maadili mema kufanikisha makuzi mazuri kwa wanetu. Lakini yanajaribu kuangalia kundi la wale ambao wana tabia za kufisha na kuwa hatarisho kwa ustawi wa watoto wetu wadogo.
Kama walivyo wafanyakazi wengine, wafanyakazi wa ndani wametofautiana kwa hulka na misukumo ya wao kufanya kazi hizo. Tunao ambao wanafanya kazi hizo kwa sababu ya kukosa nafasi ya kuendelea na masomo, kufeli masomo, tamaa ya kutajirika wakiwa mijini na ugumu wa maisha.
Katikati yao hawa wapo ambao wamekata tamaa kabisa kiroho na kimwili. Ndio hawa ambao walalapo vyumbani na watoto wetu wa kiume huwafundisha ngono, wawapo na mabinti wetu wadogo huwafundisha usagaji! Ni hawa ambao kwa sehemu kubwa huwa ni wakatili sana, wakiwanyima chakula watoto, wakiwapiga na kuwatesa pamoja na kuwatukana na kuwanenea laana pindi wazazi wakiwa hawapo.
Nae mtaalamu wa masuala ya saikolojia, Freud Sigmund anaeleza katika tafiti zake kuwa mtoto anapozaliwa huwa na viambata vingi vizuri ambavyo husubiri muongozo sahihi ili kufikia katika utendaji wake mzuri. Viambata hivyo vinajumuisha matarajio ya kuishi na kufa, ujenzi wa kufikia kipaji kamili pamoja na furaha. Inasemwa kwamba wazazi ndio wanaobeba miongozo ya kijenetiki "genetics stimulations behaviours" kufanikisha muonekano bora wa viambata kwa mtoto.
Ni vigumu kupata kizazi bora kwa kutumia rasilimali duni. Hatuwezi kuwa na watoto waliojengeka vema kimaono, kifikra na kinidhamu kwa kuwatumia, "ma-housegirls" waliokata tamaa, wadokozi, wambea na wenye kila namna ya kutojitambua. Lakini pia tusitegemee "ma-house girls" wawatendee mema watoto wetu pindi tuwapo "bize" wakati sisi waajiri tunawadharau, tunawatesa, tunawadhulumu kwa mishahara midogo na kwa kuwarundikia kazi nyingi bila mapumziko. Tataendelea kuvuna tunachokipanda!
Eneo la pili ni mtindo unaozidi kushika umaarufu siku hizi wa kuwapeleka watoto wadogo katika shule za bweni. Mtoto hadi wa miaka mitatu anapokelewa bwenini bila wasiwasi. Hapa kuna kitu cha kujiuliza, Je, watoto hawa wadogo tunaowapeleka shule za bweni wanakuwepo katika mikono na malezi ya watu sahihi? Je, malezi yanayotolewa ndiyo ambayo mzazi angependa mtoto wake ayapate?
Mwanamuziki nguli wa rege hayati Lucky Dube amewahi kuimba wimbo wa, "Born To Suffer" akielezea athari za watoto wadogo kukua bila uangalizi wa wazazi. Katika wimbo huo Dube anasema maneno haya, "The parents are the people we are depending on, for the growth of the children. If they treat them right we are going to have brighten future.If they grow up without their parents who is going to tell them this is wrong/right"
Watoto wakiwa katika shule za bweni wanakuwa mbali na wazazi wao. Huko kwa bahati mbaya ama nzuri wanakutana na watoto wenzao ambao nao wamekusanyika na tabia mbalimbali nyingi zikiwa kutoka kwa "ma-house girls" ambao wamewalea wazazi wao wakiwa bize kazini. Kinachofuatia hapa ni kuigana.
Kama mitaani tunashuhudia watoto wakifanyiana ulawiti, wakifanya ngono na usagaji nini kituzuie kuamini kuwa huenda tabia hizi zikasambaa hata kwa hawa watoto wetu tunaowapeleka shule za bweni wakingali bado wachanga? Bila kujua ama kukusudia watoto wanaanza kuwa mashoga, wasagaji, makahaba na majambazi wakingali wadogo wa miaka saba!
Wazazi hawawezi kulazimika kukaa na watoto wao muda wote, kutokana na mishughuliko na mihangaiko ya kimaisha. Lakini ninachokiamini ni kuwa hakuna mzazi hata mmoja ambaye yupo tayari kushuhudia mtoto wake akiharibikiwa. Kutoka hapa tunapata changamoto ya kutafakari namna ya kuwaandaa watu tunaowakabidhi jukumu la kuwalea watoto wetu.
Ndio, "ma-house girls", "matrons" na "patrons" katika nyumba zetu na katika shule tunakowapeleka wanetu wanatakiwa kuwa na elimu sahihi kuhusu malezi ya watoto, (professional in children care). Wazazi waepuke kukusanya, "bora mfanyakazi wa kazi" na shule ziepuke kuteua bora mtu kuwa, "patron" ama "matron"; vinginevyo tutakuwa tunawaweka rehani watoto wetu kwa ustawi wao wa baadae.
Kuna ushindi katika malezi bora ya watoto!

MIILI YA WANAJESHI WA TANZANIA YAWASILI





Picha: wavuti.com

Thursday, July 18, 2013

BARABARA ZAZIDI UCHAFU TEMEKE









Baadhi ya barabara zilivyokuwa katika mazingira machafu maeneo ya Temeke

Wednesday, July 17, 2013

Mbunge wa Temeke Mh. Zubery Mtemvu atoa 200,000/= kwa timu mbili zilizoingia Fainali ya Kombe la Diwani kata ya Azimio. Bingwa alichukua zawadi ya mbuzi.

Fainali ilikuwa kati ya timu ya CCM Mji Mpya na Azimio Kaskazini. Bingwa ilikuwa timu ya CCM Mji Mpya kwa ushindi wa penati 7-6 ambapo Diwani wa Kata ya Azimio temeke aliikabidhi timu ya Mji Mpya Mbuzi mnono.

Mgeni rasmi katika Pambano hilo alikuwa mbunge wa Temeke Mhe. Zubery Mtemvu ambapo kwa utashi wake alitoa laki mbili yaani kila timu ilipata laki 1.

MechI zote zilifanyika Uwanja wa Mashine Ya Maji eneo linaloitwa AZIMIO.



Timu ya Mji Mpya CCM ambo ndio walikuwa mabingwa wa Kombe la Diwani kwa kuibuka na kitita cha Laki moja na Mbuzi mnono.


Nyomi ya maana kwenye Uwanja Mashine ya Maji Azimio. Hii ilikuwa mechi ya fainali kati ya Mji Mpya na Azimio Kaskazini.


Mbunge wa Temeke Zubery Mtemvu akiikagua timu ya CCM Mji Mpya huku akiongozwa na mratibu wa mashindano hayo Bw. Albino Lwila.



Mtemvu akifurahi pamoja na viongozi wa CCM waalikwa kwenye pambano la fainali kati ya Mji Mpya CCM na Azimio kaskazini kwenye Uwanja wa Mashine ya maji Azimio Temeke.


Timu ya Al Qyadiria ya Mtaa wa Changani Temeke yaikung'uta kwa taaaaaabu 4-0 timu ya Taifa Academy. Pambano lilifanyika kwenye Uwanja wa Skwadi Temeke.


Mchezaji wa timu ya Al Qyadiria ambaye ni mfungaji wa Goli la tatu katika mechi yao na Taifa Academy.


Kocha wa timu ya Al Qyadiria Rajabu Kiazi almaarufu "Ticha" mwenye fulana nyeupe akiwa anaongea kwa kujiamini na baadhi ya Mashabiki wapenda soka. Kutoka kushoto Fadhil Aziz Zinzoo " Mbuyu Twite" ambaye ni meneja wa PUB ya CCM kata ya 15 iliyopo Temeke maeneo ya makutano ya mtaa wa Himo na Kitomondo na mwenye flana ya kibluu ni Godwin Nasser " Mzee wa Utelezi au Gololi" akipeana mikono na Kocha Ticha wa Al Qyadiria ya Temeke. Wengine kwenye picha hiyo ni Mashabiki waliohudhuria mchezo huo Uwanja wa Skwadi.


Wachezaji wa timu za Al Qyadiria na Taifa Academy wakiwa Uwanjani kwenye mechi baina yao ambao Taifa ilikung'utwa goli nne kwa nunge na timu ya Qyadiria.


Beki wa timu ya Taifa Academy akipiga mpira kuondoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake.


Wachezaji wa Qyadiria na Taifa Academy wakipambana vilivyo kwenye mechi baina ya timu zao.


Ama kweli mpambano ulikuwa mkali sana hali iliyopelekea timu ya Al qyadiria kuibuka kidedea kwa taabu sana baina yake na timu ya Taifa Academy leo kwenye Uwanja wa Skwadi Temeke.

Tuesday, July 16, 2013

Jinamizi la Bongo Dansi bado linatisha na kuwanasa wengi ughaibuni !

 
Ngoma Africa Band aka FFU na Mzimu wao muziki !
Bado unasumbua ughaibuni
 
Hakuna mashaka yeyote unapoutaja muziki wa Tanzania katika Nyanja za kimataifa
Jina la Ngoma Africa band maarufu pia kama  “FFU Ughabuni” inayoongozwa na
Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja wa FFU mwenye kukaanga mbuyu na wa
Kuwachia wenye meno kutafuna.
Kamanda Ras Makunja na kikosi chake hicho Ngoma Africa band yenye maskani yake
Nchini  Ujerumani,Ughaibuni ndio wanazidi kuwatia wazimu washabiki wa muziki
Barani ulaya kwa kuitangaza miziki ya Tanzania na kiafrika kwa kasi kubwa barani ulaya.
 
Bendi  hiyo maarufu  iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake Ebrahim Makunja
Almaarufu Kamanda Ras Makunja,imeweza kufanikiwa kuwapo katika medani ya muziki
Na kuweza kukonga nyoyo za washabiki tangu ilivyoanzishwa,pamoja na mafanikio hayo
Ambayo sio kitu rahisi kuyafikia kwa bendi za kiafrika barani ulaya,lakini kamanda
Ras Makunja na mzimu wake huo Ngoma Africa band inaonekana kuwa ni hekalu
La ajabu!
Watafiti na tahasisi mbali mbali za kimataifa za mambo ya itifaki katika medani ya muziki
Zimeelezea bendi hiyo kuwa na washabiki au wapenzi wapatao milioni hamsini
(Milioni 50) kila kona duniani kote, na kuifananisha bendi hiyo kuwa sawa na
Na muzimu mkubwa wenye mvuto na mtandao   wa mamilioni ya watu!
Watafiti wanashangazwa sana sana kuona kuwa bendi hiyo maarufu ya kiafrika barani ulaya
Imekuwa na mvuto mkubwa kwa washabiki,hadi sasa watafiti hawajagundua siri inayoifanya
Bendi hiyo kuwavuta washabiki kwa wingi!
Tunapozungumzia  umaarufu na ustadi wa Ngoma Africa Band ni sawa na kuzungumzia Moto
Mkali wa  nyikani Usiozimika ! na washabiki wake wapo tayari katika kila hali kuutetea mzimu wao
„Ngoma Africa Band“ ukipenda FFU.
 
Ngoma Africa band na Ushindi wa International Diaspora Award 2012
 
Juhudi za harakati za bendi ya Ngoma Africa zimevuna matunda makubwa licha ya kuwanasa mamilioni
Ya washabiki wa kimataifa bendi hiyo imeweza kuchagulia kuwa bendi bendi bora katika maonyesho mengi ya kimataifa yakiwemo maonyesho ya “Expo 2000 Hannover” Germany na “Pacific World Music Festival 2000,Honolulu,Hawai.
 
Mwaka huu 2012 Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja alitunikiwa tuzo ya kimataifa ya (IDA) International Diaspora Award,kwa niaba ya bendi yake mjini Tubingen,Germany.
Ngoma Africa band inatajwa kuwa ndio bendi ya kwanza ya kigeni barani ulaya kupewa tuzo hiyo ya kimataifa ,kutokana juhudi za bendi hiyo za kuutangaza muziki na utamaduni kiafrika.
Kutokana na taarifa za tahasisi ya Africa-activ Organizatation yenye makao yake Reutlingen, Ujerumani zinailezea bendi hiyo kuwa ni urimbo mkali unaowanasa mamilioni ya washabiki mara moja na mamilioni ya  washabiki wapo taabani kwa mapenzi na mzimu huo wa muziki Ngoma Africa band. Siri iliyiomo ndani ya bendi hakuna anayejua !! Labda mwenyewe Ras Makunja.
 
Wataalamu  mbali mbali wa sosholojia na  sekolojia ya maswala ya kijamii wanaizungumzia bendi ya Ngoma Africa kuwa ni jinamizi lenye nguvu kubwa za ajabu,jinamizi ambalo limetumia muziki wake kuwateka washabiki barani
Ulaya ! haijulikani nini siri ya mvuto huo ! Jinamizi hili la “Bongo Dansi” ! pia limewapa wakati mgumu bendi nyingi sana zinazo shea majukwaa katika maonyesho ya kimataifa.
 
Ngoma Africa band ukipenda waiite FFU ni bendi inayomilikiwa na washabiki na wapenzi wa bendi hiyo ambao wapo kila kona duniani,na mafanikio haya ni mafanikio ya kujivunia watanzania.
 
Ngoma Africa Band imeweza kuutawanya muziki wake katika vituo mbali mbali vya redio vya kitaifa na kimataifa,
Zikiwemo redio za afrika mashariki na ughaibuni,pia nyimbo hizo zinasikika katika mtandao au tuvoti ya bendi hiyo

Monday, July 15, 2013

Kombe la Diwani kata ya Miburani bado linaendelea. Ngeta na Mwarobaini zatoka sare ya 3-3.

Mwita, Humud Mwarabu na baadhi ya mashabiki wa timu ya Mwarobaini wakifuatilia mchezo kwa undani kabisa kwenye uwanja wa Temeke Squad Temeke leo jijini Dar es Salaam.

Mwamuzi wa mchezo wa leo kati ya Ngeta na Mwarobaini aakimuelekeza mchezaji wa Ngeta Mabruki sehemu sahihi ya kuweka mpira kabla ya kuupiga. Mechi iliisha kwa sare ya 3-3.

Mchezaji wa Ngeta Mabruki akipiga mpira wa adhabu kuelekea kwenye lango la Mwarobaini leo.

Kocha wa Mwarobaini Habib Sultan a.k.a Pep Guardiola  na Mkurugenzi wa timu ya Mwarobaini 
 Bw. Maliki wakitoa mawaidha kwa wachezaji wao wakati wa mapumziko leo jioni mechi iliisha kwa sare.

Mwenyekiti wa Tawil la CCM kata ya 15 Wailes Temeke jijini Dar es Salaam Bw. Asad Mfaume mwenye suti nyeusi akifuatilia kwa makini mawaidha yanayotolewa na kocha wa Mwarbaini.

Wachezaji wa Ngeta na Mwarobaini wakiwa mchezoni Uwanja wa TMK Squad leo Temeke.

Mechi ikiendelea.

Kutoka kushoto ni Malik Mkurugenzi wa timu ya Mwarubaini na pia  kocha mkuu wa timu ya Mwarubaini Habib Sultan a.k.a Pep Guardiola wakitabasamu wakati timu yao ikiwa inacheza mechi dhidi ya Vijana wa Mtaa wa Ngeta Temeke jijini dar es salaam.

Habib Sultan a.k.a Pep Guardiola kocha wa Mwarubaini leo hii akiangalia viajana wake wakiwa mchezoni.

Kombe la Diwani linalofanyika Uwanja wa Temeke Squad likiwa linachanja Mbuga.


Leo ilikuwa mechi kati ya Mwarubaini na timu ya Mtaa wa Ngeta. Matokeo yalikuwa 3-3 (sare).

Wednesday, July 10, 2013

MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA CCM KATA YA MIKENGENI TEMEKE









HEPI BETHDEI ANKO ISLAM

 Mjomba wangu Islam akisherehekea kutimiza miaka mitano nyumbani kwao Temeke Wailes
 Mambo ya keki hayo
 Mama Mkuu akilishwa keki
 Mama Mkuu mwingine
 Mama Mzazi wa Islam akilishwa keki
Familia

Sunday, July 7, 2013

HISIA ZA MTOTO WA TEMEKE NATAMASHA LA MATUMAINI

Shigongo pamoja na timu nzima mlioandaa huu mpango mnazingua mazima kwa kuzidi kujitajilisha kupitia tamasha mliloandaa wenyewe huku Shigongo ukitumia kauli mbiu yako "kufeli shule sio kufeli maisha" kakudanganya nani katika dunia ya leo inayotaka elimu na pesa kama huna elimu kuwa na pesa. Pesa ndio inaleta elimu bora kwa sasa. Ikiwa kweli umeamua kusaidia elimu ya Tanzania... haikuwa na haja ya kutoa asilimia 10 ya mapato yatakayopatikana apo mlangoni siku ya tamasha, kwani watanzania watakaoingia apo ni zaidi ya asilimia kumi unayotoa wewe kupeleka kwenye elimu sasa hzo asilimia nyingine 90 zinaenda wapi na kufanya nini au ndio zinaenda kutafuta matukio ya kudhalilisha watanzania kupitia magazeti yako yanayoandika habari za uzushi, uongo, kuwagombanisha watu na familia zao kuwafanya waonekane wajinga katika jamii ya watanzania wanaosoma magazeti yako uliyoyabatiza jina jipa "magazeti pendwa" huku ukijua kinachoandikwa ni udaku pakiwa na neno "habari na mwandishi wetu" hv huyo mwandish wenu hana jina au ndio jina lililopa ajira ni "mwandishi wetu" habari ikiwa za kweli lazima jina la mwandish aliyekuwepo eneo la tukio liwepo. Kwa upande wangu mimi naona haikuwa na haja ya kudanganya watanzania kupitia matatizo ya elimu yetu kuwa unawasaidia kwa asilimia 10 ikiwa asilimia 90 ujasema zinapoenda, ni hv ungetumia tu pesa ya magazeti yako uliyoyaita pendwa kuchangia asilimia kumi uliyochagua wewe na wasomaji wengi wa magazeti yako ni wanafunzi na wao ndio wahusika wakuu wa kuchangiwa huo mchango tamasha lako ungeliandaa kwa mengine kabisa unayoyajua wewe na mafisadi wenzako mliojificha kwenye ulokole.

Pia wabunge nyie ndio wanafiki wakubwa katika elimu yetu mliwah kukataa hoja ya mh flani mkisema elimu haina tatizo mpaka matokeo mabovu yakawaumbua. Nyie mngetumia posho ya kikao kimoja kuchangia katika elimu ingetosha sana kuliko kuja kusapoti wizi wa akili kama huu uliopewa jina tamasha la matumaini. Tambueni kwenye njaa na dhiki apaponywi kwa mkate mkavu. Elimu yetu inaitaji mchango mkubwa sana sio huo wenu mnaofanya sasa wa kimagumashi kuboresha miladi yenu.


Mwana Hisia Tmk
Dee Dion

TAMASHA LA MATUMAINI LINAVYOENDELEA

 Maandalizi ya ndondi yanakaribia

 hali ya mchana ilivyokuwa kabla ya watu kuanza kujaa
Baadhi ya wabunge wa Yanga wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga wabunge wa samba kwa penati 4-2
 Mdau Abeid Mvuma akiwa na shemeji Hilda
Bongo flava wakishangilia ushindi baada ya kushinda kwa penati 1-0