Wednesday, November 30, 2011
WATOTO WA USWAZI
Ni Jabir Saleh mwenye kofia nyeusi akiwa na Dj KU ni waendeshaji wa kipindi cha Jump Off kinachorushwa hewani kuanzia Jumatatu-hadi Ijumaa saa 1-4 na sasa wamekuja na mtazamo mpya katika suala zima la burudani usikose hii
KICHWA KINAUMA-JUMAPILI MAISHA CLUB
Kundi la Muziki kutoka Temeke Wanaume familiy baada ya kukaa kimya kwa kipindi cha miaka minne wataitambulisha video yao mpya ya kichwa kinauma katika ukumbi wa maisha club.
Monday, November 28, 2011
KWETU KAWAIDA
Mitaa ya kwetu ni jambo la kawaida kukuta mwanaume anaosha vyombo barazani kama hivi. Je? kwenu mnaweza
Friday, November 25, 2011
Thursday, November 24, 2011
UGALI NAO BEI JUU
Huku kwetu ndio kilikuwa chakula cha bei rahisi lakini kadri siku zinavyozidi kwenda na bei inazidi kuwa kubwa
Wednesday, November 23, 2011
Gumbo Mapumzikoni
Mchezaji wa Yanga Rashid Gumbo akiwa na familia yake katika kipindi hiki cha mapumziko ya Ligi kuu Tanzania Bara ambayo kwa sasa imesimama kupisha mashindano ya Cecafa
KITAANI
Mitaa ya Temeke Kata 14, maeneo ya klabu ya Good Hope
Mtaa Uzuri na Mwaka hali ilivyo kwa sasa
Uwanja wa Mabati uliopo kati ya Mtaa Uzuri,Pazi na Mwaka
Huu Ukumbi wa Luxury Pub mpaka sasa bado haujafunguliwa ambao ulileta matatizo na baadhi ya watoto kufa katika ukumbi huo
Urafiki Bar, ndio Bar ilikuwa maarufu maeneo ya Temeke imebaki kama Gofu
Urafiki Bar Ilivyo kwa sasa

MCHAKAMCHAKA
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi Temeke wakikimbia Mchakamchaka katika maandalizi ya maazimisho ya miaka 50 ya uhuru
Wednesday, November 16, 2011
UKARABATI
Mitaa ya Wailes, Miburani barabara zake zimeanza kukwangulia nini kinachofuata rami au vumbi tunasubiri
UMRI NA MAJUKUMU
hali ya watoto wanaozagaa mitaani kipindi cha masomo inazidi kuongezeka hawa ni baadhi ya watoto ambao ulikuwa mda wa masomo wao walikuwa wapo mitaani wakiokota vyuma ili kwenda kuuza na kupata fedha
Tuesday, November 15, 2011
Tandika wachanga fedha kuchimba mifereji
WANANCHI wa kaya zipatazo 23 katika Kata ya Tandika eneo la Devis Kona wamechanga Sh150,000 kwa ajili ya kuchimba mitaro ya kupitisha maji yanayokwama na kusababisha mafuriko katika nyumba zao kufuatia mvua zilizonyesha mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Davis Corner, Mfaume Mbonde alisema kwamba aliwahamasisha wakazi hao ili kila kaya kutoa Sh5,000 kwa ajili ya kuchimba mitaro iliyoziba na kusababisha mafuriko ndani ya nyumba za wakazi wa mtaa wake.
Mbonde alisema kwamba walikuwa wakipeleka malalamiko mara kwa mara katika ofisi ya kata, lakini hatua za haraka hazikuchuliwa hali iliyosababisha yeye kuchangisha fedha katika mtaa huo.
“Tulipeleka malalamiko yetu katika ofisi yetu ya kata mara nyingi tu, lakini hatuoni hatua zikichukuliwa na hivyo nimechangisha hizo fedha” alisema Mbonde na kuongeza
“Mimi nimeongezea Sh20,000 ili kutatua tatizo la maji ya mvua kukwama katika maeneo haya”, alisema.
Akizungumzia adha wanayoipata kutokana na mafuriko hayo, mkazi wa eneo hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Albert Mwakatumbula alisema kuwa maji yanaingia hadi ndani na kusababisha vitu kuloa ikiwa ni pamoja na magodoro, makochi na vyombo vingine.
Alisema hali hiyo ilijianza baada ujenzi wa barabara iliyokuwa ikitoka Davis corner kwenda Yombo Dovya kuziba miundo mbinu iliyokuwa ikipitisha maji katika mtaa huo.Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata ya Tandika, Joseph Kambanga alionyesha wasiwasi kwa wananchi hao kuchangishana fedha hizo.
Alisema kuwa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Mwenyekiti ya Serikali ya Mtaa wa Devis Kona, alikwenda eneo hilo pamoja na mhandisi wa Manispaa ya Temeke kisha wakatoa ombi kwa kampuni husika kuchukua hatua za dharura ili kudhibiti hali hiyo.
Afisa Mtendaji huyo wa kata ya Tandika aliongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo itokayo Devis Kona kuelekea Yombo Dovya ulianza Septemba mwaka jana lakini hajui ujenzi huo utaisha lini kwani mkataba wa mkandarasi huyo upo Manispaa ya Temeke.

MTAMBO WA TANESCO WAUNGUA
MOTO mkubwa umezuka jana kwenye Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kuunguza kifaa kiitwacho ‘reactor’ kinachotumika kudhibiti mfumo wa usambazaji umeme katika jiji la Dar es Salaam hali iliyosababisha jiji hilo kukosa umeme.Tukio hilo lililotokea saa 10:45 jioni, lilisababisha kukatika kwa umeme katika jiji hilo na viunga vyake huku uongozi wa ukisema haijajulikana tatizo hilo lingechukua muda gani kutatuliwa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Sophia Mgonja aliwaambia waandishi wa habari kwamba: “Hadi sasa hatujui chanzo na wala athari zake. Umememe umekatika jiji zima na hatuwezi kurudisha hadi tutakapofanya uchunguzi kuona kiwango cha uharibifu.”
Alisema kifaa hicho kilichoungua kinachokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani 500,000 (takriban Sh 900milioni) hakitengenezeki na badala yake kinatakiwa kuagizwa kingine.
Mgonja alisema mbali ya kifaa hicho vingine kama ‘Control Cable’ pamoja na vikombe vya kwenye nguzo ambavyo vilikuwa havionekani kutokana na kufunikwa kwa moshi huenda navyo vimeteketea.“Kuanzia sasa mafundi wanaanza kazi ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo lakini pia kuona namna tunavyoweza kurudisha umeme kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam”.
Mkuu wa zamu wa Kikosi wa Kikosi cha Zimamoto wa Jiji la Dar es Salaam, Seleman Said alisema kikosi hicho kiliwasili katika eneo hilo saa 11:03 baada ya kupata taarifa saa 10:45 jioni.
Alisema baada ya kuwasili, walielezwa kuwa kifaa hicho kina mafuta hivyo kulazimika kuchanganya maji na dawa ili kuwezesha kazi hiyo kufanywa kwa ufanisi.“Kazi tuliifanya kwa muda wa dakika saba na katika muda wa dakika 20 tulikuwa tunamalizia kuhakikisha moto huo haulipuki tena,” alisema Said.
Mwananchi

Saturday, November 12, 2011
Friday, November 11, 2011
HALI ILIVYOKUWA MBEYA MCHANA WA LEO
Manati na Risasi
maeneo ya soweto jijini mbeya
Wamachinga wakichochea moto wa matairi katikati ya barabara ya mbeya na tunduma
majeruhi wa risasi za polisi katika vurugu za Mwanjelwa leo hii akiwa kapigwa kichwani. Hadi sasa kuna majeruhi wanne wa risasi, wawili kichwani, mmoja kwenye paja na mwingine mkononi
Mmoja wa majeruhi wa risasi za polisi katika vurugu za Mwanjelwa leo, Abel Mwalukali akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kupigwa risasi kwenye mkono.
Msaada:mbeyayetu.blogspot
Thursday, November 10, 2011
USWAZI TAFARANI, WABUNGE WAONGEZWE POSHO
SUALA la nyongeza ya maslahi kwa wabunge limeibuka tena safari hii, wabunge wote wakiwamo wa Chadema, wakitaka nyongeza za mshahara na posho.
Wakizungumza wakati wa mkutano wa kuelezwa kazi zitakazofanyika katika Mkutano wa Tano wa Bunge ulioanza juzi, wabunge hao walisema mshahara na posho wanazopata ni ndogo na haziwatoshi.
Habari kutoka katika mkutano huo ulioanza baada ya kipindi cha maswali na majibu, zilisema aliyeanzisha hoja hiyo alikuwa Mbunge wa CUF.
“Mara baada ya kuzungumzia hilo la posho na tabu wanazopata wabunge wanapotaka kutoa magari bandarini, hoja yake ya nyongeza ya maslahi iliungwa mkono na wabunge wote wakiwamo wa Chadema,” alisema mmoja wa wabunge aliyehudhuria mkutano huo.
Miongoni mwa wabunge wa Chadema waliopingana na kauli ya chama chao ya kupinga nyongeza hiyo katika mikutano ya Bunge iliyopita, ni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, aliyesema maslahi hayo ni madogo kulinganisha na shughuli za wabunge.
Selasini anakaririwa akimwambia Spika, “Mheshimiwa Spika nilivyokuwa nje ya Bunge, nilikuwa nikifikiria tofauti na nilivyokuwa Mbunge, leo naomba Mungu anisamehe, kumbe malipo ya wabunge hayatoshi.”
Katika hoja yake, Selasini alieleza kuwa kauli iliyotolewa na Chadema haikuwa msimamo wa chama, bali ni ya mtu binafsi na kubainisha kuwa wanaopinga nyongeza hiyo, wana vyanzo vingine vya mapato tofauti na wenzao akiwamo yeye.
Mbunge mwingine wa Chadema, Mustapha Akunaay (Mbulu), alizungumzia nyongeza hiyo ingawa alionesha wasiwasi wa kutokuwapo usiri kwenye suala hilo na yote yanayozungumzwa kutolewa nje ya kikao hicho.
Hata hivyo, Spika Anne Makinda aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, alitaka wabunge wasihofu kuzungumzia maslahi yao na kuwaeleza kuwa suala hilo limeshafikishwa kwenye vyombo husika na linashughulikiwa.
Mshahara wa wabunge ni Sh milioni 2.3 kwa mwezi na pamoja na posho kiwango cha juu anachopokea mbunge kwa mwezi kinafikia Sh milioni saba.
Katika mikutano iliyopita ya Bunge hilo, suala la posho liliibuka huku baadhi ya wabunge wa Chadema wakipinga kupokea posho za vikao vya Bunge wakisema zinastahili kupelekwa kwenye miradi ya wananchi.
Hata hivyo, Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, alitofautiana na wabunge wenzake akisema wabunge wanastahili kulipwa posho hizo kwani wanazolipwa sasa Sh 70,000 bado haziwatoshi na badala yake ziongezwe hadi Sh 500,000.
Kauli hiyo ilizusha mtafaruku mkubwa ndani ya chama hicho hata kutishia mustakabali wake pale alipolazimika kujadiliwa na Kamati Kuu ya chama hicho kwa ilichokiita utovu wa nidhamu kutofautiana na sera ya chama chake.
Shibuda alijiunga Chadema siku chache kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana akitoka CCM ambako alienguliwa katika kura za maoni za ubunge.

Tuesday, November 8, 2011
MAHAFALI CHUO CHA DUCE
Baadhi ya picha za katika mahafali yaliyofanyika chuo cha Mazoezi Chang`ombe (DUCE) hivi karibuni
Picha na X-Pasua
Monday, November 7, 2011
MAZINGIRA HATARISHI
Baadhi ya uchochoro maeneo ya Temeke Kitomondo yakiwa katika hali ya hatari baadhi ya nyumba kutoboa nyuma ya nyumba na kuruhusu maji kusambaa
Hawa watoto walikutwa wikicheza kando ya Maji hayo ambayo yanatoka chooni
Hawa watoto walikutwa wikicheza kando ya Maji hayo ambayo yanatoka chooni
Thursday, November 3, 2011
SERIKALI YAKATAA USHOGA
Raymond Kaminyoge TANZANIA imesema ipo tayari kukosa misaada yote kutoka Serikali ya Uingereza na kamwe haiwezi kuruhusu sheria inayotambua mashoga na kuhalalisha ndoa za jinsia moja.Msimamo huo mzito wa serikali umekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, kutamka kwamba nchi yake ina mpango wa kusitisha misaada yake kwa nchi ambazo sheria na katiba zao, hazitambui mashoga na ndoa za jinsia moja. Cameron alikaririwa akithibitisha kuwa tayari amewajulisha juu ya suala hilo Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola waliokuwa wakihudhuria mkutano wa Jumuiya hiyo uliomalizika siku nne zilizopita, mjini Perth , Austaralia ambao pia ulihudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete. Waziri Mkuu huyo kutoka chama cha Conservative ambacho kilishinda uchaguzi Mei mwaka jana, alisema suala hilo la mashoga na ndoa za jinsi moja ni moja ya mambo yanayoongoza sera ya serikali yake kuhusu misaada kwa mataifa mbalimbali na kwamba tayari imeanza kutekelezwa katika maeneo kadhaa duniani. Kauli ya Cameron imechukuliwa kama kielelezo cha ukoloni mamboleo ambao Uingereza inajaribu kuupandisha daraja kwa mataifa yanayoendelea kwa kigezo cha misaada Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema pamoja na umasikini wake, Tanzania kamwe haitaruhusu upuuzi huo kwa kigezo cha misaada. “ Tanzania ni nchi maskini lakini hatutakubali kuruhusu upuuzi huo eti kwa sababu ya misaada yake na fedha zao, lakini ushoga si utamaduni wetu, hata sheria zetu zinakataa,” alisema Membe. Alifafanua kuwa katika kuonesha msimamo wa kutokukubaliana na masharti hayo, Tanzania imeshikilia msimamo thabiti kupinga upuuzi huo ambapo Januari mwaka huu, ilimkataa balozi shoga ambaye aliteuliwa na nchi yake kuja kuiwakilisha hapa nchini. Hata hivyo Waziri Membe hakutaja jina la balozi huyo wala nchi anayotoka. “Niwape siri moja ambayo tuliificha lakini leo ngoja niwaambie, mwanzoni mwa mwaka jana nililetewa barua kunijulisha ujio wa balozi mmoja anayekuja kuiwakilisha nchi yake, mwanamume mwenye ndoa ya jinsia moja. Nilikwenda kumweleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu wasifu wa balozi huyo mtarajiwa naye akajibu kwa maneno matatu, yarabi toba! Mkatae!” Waziri Membe alifafanua kuwa serikali ilimkataa balozi huyo kwa kuwa ni kinyume cha utamaduni wetu na sheria za nchi kuwa na watu wenye tabia hizo. Alisema alimjulisha waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kwamba balozi huyo haruhusiwi kuja kufanya kazi nchini kwa kuwa ni kinyume na utamaduni wetu. “ Waliendelea kuniomba kwamba balozi huyo akija hatatoka kwenye makazi yake akiwa na mwenza wake hivyo watu hawatamuona lakini tulimkataa kabisa, wakatuelewa,” alisema Membe. Alieleza kuwa tamko hilo la Waziri Mkuu Cameron linaweza kusababisha hatari ya kuvunjika kwa uhusiano miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola na koloni mama Uingereza na waziri huyo atabeba lawama hizo Akisisitiza msimamo huo wa serikali, Membe, alisema Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha tisa, kinatambua ndoa ya jinsia mbili tofauti, yaani mume na mke. “ Sheria hizi tunazozitumia hivi sasa tumezirithi kutoka Uingereza ambako leo wanatukuza ndoa za jinsia moja na ushoga,” alisema Membe. Suala la kile kinachoitwa haki za binadamu kuhusu ushoga ilikuwa moja ya ajenda ambazo viongozi kadhaa walishindwa kuafikiana katika mkutano Perth . Hoja ya kukomesha vizuizi dhidi ya ushoga na ndoa za jinsi moja lilikuwa moja ya mapendekezo yaliyokuwamo katika ripoti ya ndani kuhusu matarajio ya baadaye ya Jumuiya hiyo ya Madola. Itakumbukwa kwamba, Malawi tayari imeathirika na mpango huo wa Uingereza kwa sehemu ya misaada yake kusitishwa kutokana na msimamo wa nchi hiyo kuhusu kile Uingereza na nchi za Magharibi zinazokiita haki za mashoga. Ikumbukwe pia kuwa, mjadala mzito ulioibuka katika Bunge la Uganda mwaka 2009 kuhusu ndoa za jinsi moja ilikuwa sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo ya Uingereza na washirika wake. Ajenda zingine Mkutano wa Perth Waziri Membe alisema viongozi wa Jumuiya ya Madola walikubaliana suala la mabadiliko ya tabia nchi kuwa ajenda kuu katika nchi hizo. Alisema ajenda hiyo sasa inakuwa muhimu kutokana na nchi nyingi wanachama wa jumuiya hiyo kuwa katika tishio kubwa la uharibifu wa mazingira. Aidha, Membe alisema nchi hizo zimekubaliana kuandaa kanuni na mwongozo ambao utatakiwa kufuatwa na nchi za jumuiya hiyo. “ Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Jumuiya ya Madola tutakutana Aprili mwakani kuandaa miongozo na kanuni hizo,” alisema Membe. mwisho Mwananchi | Waziri Membe asema kama ni misaada yao basi
WEZI WABOMOA MADUKA USIKU-TEMEKE SUDAN
Baadhi ya wananchi wakiangali baadhi ya maduka yaliyovunjwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya Temeke Sudan, idadi ya maduka yaliyovunjwa yalikuwa kumi na moja
Mkurugenzi Mkuu wa Timbwa Co.Ltd Yusuf Shaban mwenye shati jeupe akijadiliana na baadhi ya wafanyakazi wake
Eneo la tukio
Baadhi ya vifaa walivyotumia kubomoa na kukatia
Moja ya duka lililovamiwa na baadhi ya vitu kuibiwa
Hawa wezi walikuwa kama panya buku jinsi walivyokuwa wanatoboa baadhi ya matobo waliyoyatumia katika kufanya shughuli zao
walikuwa wanatoboa chumba baada ya chumba
Baadhi ya matundu waliyotumia kuibia

Tuesday, November 1, 2011
7 UP TMK BASKETBALL LEAGUE 2011
Mashindano ya 7up tmk BasketBall league 2011yanazoshirikisha timu za Temeke yamefikia katika hatua ya nusu fainal ambayo inategemea kuanza jumamosi katika Uwanja wa ndani wa Taifa(Indoor).
Timu ambazo zimepata nafasi ya kuingia katika hatua ya Nusu Fainali ni, Chang`ombe, Jkt, Abc, na Pctw katika nusu fainali ya kwanza itaanza saa 8.00 mchana na ya pili itakuwa saa 10.00 jioni
Subscribe to:
Posts (Atom)