Pages

Monday, April 20, 2015

SERIKALI - HAKUNA MTANZANIA ALIYEKUFA AFRIKA KUSINI


Serikali imesema hakuna mtanzania aliyeuawa katika matukio ya mauji ya  chuki za kibaguzi (ZENOPHOBIA) yanayofanywa na raia wa Afrika Kusini dhidi ya wageni na tayari imeanza mpango wa kuwarudisha nyumbani watanzania 21 kati ya 23 waliohifadhiwa katika kambi kwenye mjini DURBUN nchni humo kwa ajili ya usalama.

Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe amesema  vifo vya watanzania watatu vilivyotokea nchni humo havina mahusiano na mauaji hayo ZENOPHOBIA na kusisitiza serikali ya afrika kusini imeanza kuchukua hatua na tayari watu wawatu waliohusika na kifo cha rais wa msumbiji wamekamatwa.
Akizungumzia idadi ya watanzania waliohifadhiwa kwenye 
Kambi katika mji wa DURBUN,Mhe Membe amesema takribani watanzania 23 wamehifadhiwa katika kambi ya isipingo iliyo  na zaidi ya raia  wa kigeni elfu tatu ambao wako chini ya ulinzi wa serikali ya afrika kusini na kusisitiza serikali imeanza utaratibu wa kuwarudisha nyumbani watanzania 21 kati yao.
Akielezea msimamo wa tanzania kufuatia mauaji hayo ya ZENOPHOBIA yanayoendelea nchni afrika kusini,Mhe. Membe amesema serikali inaunga na jumuiya ya nchi za SADC kulaani vitendo vya mauaji yanayoendelea nchni humo ambapo watu 8 wamekwisha uawa kikatili na kuita serikali ya afrika kusini kuzuia mauaji hayo haraka iwezekanavyo.
Aidha amesema serikali ya Tanzania haitakuwa na tatizo la watanzania kurudi nchni humo baada ya mauaji kudhibitiwa na kwa upande wa wafanyabishara walisajiliwa kihalali na kupoteza mali zao, serikali itawasiliana na wanasheria wake ili kuona namna ya kutafuta namna ya nchi hiyo kuwafidia hasara waliyoipata.