Pages

Monday, March 9, 2015

Kijiji cha Mtimbwilimbi

Baadhi ya wanafunzi Wa while ya msingi Mtimbwilimbi wakiwa njiani wakirejea majumbani

Wakati wengine milioni 10 ya mboga huku watu wanaendelea kula mizizi ambacho ndio chakula maarufu kusini wengi wanakiita Ming'oko

Imetosha

Watu saba wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukata kiganja cha Albino

 Jeshi la polisi mkoani rukwa linawashikilia watu saba hadi sasa, kwa tuhuma za kuhusika na kitendo cha kikatili cha kukata kiganja cha mkono wa kulia, cha mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Baraka Cosmas Lusambo mwenye umri wa miaka sita, katika kitongoji cha kikonde kata ya kipeta wilaya ya sumbawanga vijijini, ambapo pia katika tukio hilo wamemjeruhi mtoto huyo mkono wa kushoto.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa rukwa kamishna msaidizi wa polisi Leons Rwegasira, amesema wamefanikiwa kuwakamata watu hao kufuatia msako mkali, mara tu baada ya kutokea tukio hilo kwenye kitongoji hicho cha kikonde, ambacho kinakuwa na wakazi wakati wa msimu wa kilimo na kiangazi watu wanahama tena, katika familia yenye watoto wengine watatu wenye ulemavu wa ngozi. 
 
ACP.Rwegasira pia amesema kwenye msako huo mkali, wamefanikiwa kuwakamata watu wanane wanaojihusisha na uganga wa jadi na upigaji wa ramli chonganishi, ambacho ni chanzo kikubwa cha kusababisha vifo na kujeruhiwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikina. 
 
Mtoto baraka na mama yake mzazi wamelazwa kwenye hospitali ya rufaa ya jijini mbeya, wakitibiwa majeraha waliyoyapata wakati wa purukushani za kumshambuliwa mtoto huyo.

Monday, March 2, 2015

TANZANIA INAPOTEZA MABILIONI KWA RUSHWA

Tanzania inapoteza mabilioni ya fedha kwa rushwa na udanganyifu unaofanywa na watumishi wa TRA
Serikali imekiri kuwa Tanzania inaendelea kupoteza mabilioni ya fedha za umma kutokana na rushwa na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa mamlaka ya mapato (TRA) kwa kuvusha mizigo mikubwa bila kulipa kodi kwa kudanganya kuwa  ni mali ghafi huku mingine ikidaiwa kupelekwa nje ya nchi na kuuzwa njiani hali inayo wafanya wananchi kukosa imani na taasisi za serikali.
Waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora GEORGE MKUCHIKA ametoa kauli hiyo jiji Arusha alipokuwa anazungumza na watendaji wa mamlaka ya mapato takukuru na viongozi wa dini katika kikao cha mpango mkakati wa TRA kupambana na rushwa kwa kuwashirikisha wadau na kuongeza kuwa watanzania wamechoka kusikia upotevu wa mabilioni ya fedha za umma kwa ajili ya kunyakuliwa na  watu wachache.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya amani ya viongozi wa dini SHEKH ALHAD MUSA amesema  TRA imekuwa ikilalamikiwa sana na wananchi kuhusu kushamiri kwa rushwa  hivyo kuna muhimu wa viongozi wa dini kutoa semina za neno la mungu kwa watumisi huku msaidizi wa askofu wa kanisa la KKKT Diosisi ya mashariki na pwani GEORGE FUPE akidai kabla kutengeneza mipango mkakati inapaswa  kila mmoja ajitathimini kama inatosha kuwepo katika nafasi yake.
Chanzo.itv
Kamishina mkuu wa mamlaka ya mapato nchini TRA, RISHED BADE amesema TRA ni taasisi iliyopo katika mazingira hatarishi kwa vishawishi vya rushwa lakini bado mikakati inafanyika kuondoa hali hiyo na sasa wameanza kushirikisha wadau katika kuianda mikakati mikakati hiyo.

AZAM YAMTIMUA OMOG


Uongozi wa Azam FC unatangaza kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omog baada ya kuwa naye kwa miezi 14.
Omog aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondoka pamoja na msaidiI wake Ibrahim Shikanda.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya George Best Nsimbe

Aliyechomwa afauru

Msichana huyu Aisha Nabukeera alichomwa na mama yake wa kambo mnamo mwaka 2006.

Habari hii iligonga sana vichwa vya habari vya Afrika Mashariki.

Mfanyabiashara mwenye mafaniko Frank Gashumba alimchukua na Kumfanya Mtoto wake na kumsomesha.

Sasa hivi amefaulu mtihani wake wa kidato cha sita na anategemea kujiunga na Elimu ya Chuo kikuu na ndoto zake ni kusomea sheria.
Chanzo:JF

VIONGOZI WANANCHI WALIVYOMUAGA CAPT.KOMBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete, akiongoza maelfu ya Watanzania kuuaga mwili wa Kapteni John Komba, katika viwanja vya Karimjee  jijini Dar es Salaam.…
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa viwanja vya Karimajee.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete, akiongoza maelfu ya Watanzania kuuaga mwili wa Kapteni John Komba, katika viwanja vya Karimjee  jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassani Mwinyi akipita kando ya jeneza lenye mwili wa John Komba.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho.
Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akiaga.
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Eduard Lowassa, akipita kando ya jeneza.
Huyu ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Abdulahman Kinana.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM. Yusuf Makamba akilia kwa uchungu wakati anakaribia jeneza.
Huyu ni mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale-Mwiru.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dk. Rejinard Mengi akiaga.
Waziri wa Utalii Razaro Nyalandu akiaga mwili wa marehemu John Komba.
Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Selemani Kova, akipiga saluti wakati wa kuaga.