Pages

Friday, January 24, 2014

MTAZAMO WA BLOGU ZETU-SUDI MNETE


Kwa kweli nasikitika sana, hizi blogu za nyumbani kwa kiasi kikubwa zinakuwa kama radio nyingi za nyumbani, nikisema nyumbani namaanisha Tanzania kwa mambo kadhaa kwanza kwa kuchukuliana taarifa yaani, ukiona habari moja basi hiyo hiyo, hata kama imekosewa utaiona katika karibu blogu zote, pilia kuna watu wanazungumziwa katika maisha ya kila siku haohao, sijui nani Sepetu mara kafanya hivi mara vile, tatu hata hizo habari wanazoweka na picha za watu hao hazina umhimu wowote kwa jamii. Nyinyi waandishi wa hiyari wenzangu, kabla hujasambaza chochote katika mtandao ebu tumia tu akili ya kawaida kujiuliza je, hiki nnachokisambaza kwa umma kina faida gani!!

Monday, January 20, 2014

KILINGE CHA HiP HoP - TAMADUNI MUZIKI


 Nash Mc mwenye Mic akitoa mitindo huru katika ukumbi wa Msasani Club
 Meja Mbuya Grafit akielezea uhusiano wa maandishi Grafit na Hip Hop
 Kipindi cha Malani kikafikia
Baadhi ya wachora ukutani wakiwa katika picha ya pamoja

Friday, January 10, 2014

SIMBA YATINGA FAINALI MAPINDUZI

 Simba imefanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kuifunga URA ya Uganda  goli 2-a magoli ya Simba yalifungwa Amri Kiemba, na Joseph Owino, Simba itakutana na KCC katika fainali ambayo waliifunga Azam 3-2 na fainali inategemewa kuchezwa Jumatatu katika uwanja wa Aman
 Uhuru Seleman na Haruna Chanongo wakiwa wamepumzika baada ya mechi
 wachezaji wa Simba wakiwa pamoja

MADUKA YA KARIAKOO NA MASHINE ZA TRA

 Hali hii ilitokea jana ambapo maduka mengi ya Kariakoo yalifungwa kuendelea kuishawishi serikali kupunguza mashine za risiti bei



hii ndio hali ilivyokuwa jana maduka ya Kariakoo

Wednesday, January 8, 2014

Eneo la Temeke Kota jijini Dar es Salaam hivi sasa ni kama limepigwa BOMU. Nyumba zote zapigwa chini na waliokuwa wakazi wake wahaha kutafuta sehemu za kujisitiri.

Hili ni eneo la Kota lililoko Temeke Mwisho jijini Dar es Salaam. Limebomolewa lote kupisha mradi wa Serikali ambao mpaka sasa haujaweka wazi kwa Wananchi wa eneo hilo. Hali ndivyo kama inavyoonekana kwenye hiyo picha.

Kwenye picha kulia askari wa manispaa ya Temeke akiwa anaangalia moja ya nyumba ilikuwa inasubiri kubomolewa eneo la Temeke Kota jijini Dar es Salaam.

Eneo la Temeke Kota Dar es Salaam lilivyo hivi sasa baada ya baadhi ya nyumba kubomolewa, hali iliyopelekea wakazi wengi kutafuta sehemu za kujihifadhi.

Moja ya nguzo ya Umeme iliyoangushwa na Greda wakati wa zoezi hilo. Nguzo hiyo iko mtaa wa Mkuranga A.

Unajionea mwenye hali ilivyo Temeke Kota kwa sasa.

Nadhani unaweza jenga kiwanja cha kuchezea soka eneo la Temeke kota kwa sasa.

Baadha ya watu wakichukua baadhi ya kokoto zilizotoka kwenye nyumba zilizobomolewa eneo la Temeke kota jijini Dar es Salaam.

Temeke Kota haitazamiki kwasasa nyumba zote zimepigwa chini.

Mti mrefu unaoonekana kwa mbali unafahamika vizuri kwa wale wakazi wa Temeke Kota Jijini Dar es Salaam.

Nyumba ya Mwalimu Kalinga kwa wanaomfamu ndio iliyobakia.

Nyumba pekee iliyobakia Temeke ndio anayoishi Mwl. Kalinga. Amegoma kuondoka eneo hilo na anasema nyumba hiyo kapewa na Hayati Baba wa Taifa.

MWENYEKITI WA CHADEMA TEMEKE ATEKWA NYARA

Walinitupa na kutimua mbio wakiniacha nikiwa na maumivu makali. Nilitulia kwa muda na kujitahidi kuinuka na kupiga hatua kwenda nyumba zilizokuwa jirani kuomba msaada.” Joseph Yona.PICHA|MAKTABA 

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Wilaya ya Temeke, Joseph Yona (32), ametekwa nyara na kujeruhiwa vibaya kwa kipigo kisha kutupwa katika vichaka eneo la Tegeta Ununio, wilayani Kinondoni a watu wasiojulikana.
Yona ambaye alitekwa juzi akiwa katika eneo la Mtoni kwa Aziz Ali, amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Yona ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema alisema jana kwamba alitekwa yapata saa 5.00 usiku wa kuamkia jana na watu ambao awali, walijitambulisha kuwa ni polisi.
“Tulikuwa tumekaa na vijana wanne wa Tawi la Ukombozi, Chadema la Temeke, ndipo ghafla wakajitokeza watu kama sita hivi wakaja moja kwa moja na kuninyanyua huku wakiniambia twende kituo cha polisi,” alisema.
Alisema baada ya kuingia ndani ya gari ambalo lilikuwa linafanana na yale ya polisi alivuliwa fulana na kufungwa macho na mikono.
Alisema baada ya mwendo uliochukua kitambo kidogo, gari hilo lilisimamishwa na watu hao wakamshusha chini na kumpeleka sehemu iliyokuwa na bonde huku wakiendelea kumpiga kabla ya kumtelekeza na kutoweka.
“Njiani nilijaribu kuwasihi wasiniue kwa kuwa nina watoto wadogo wawili ambao wananihitaji, niliwasisitiza watambue na kwamba nao wana watoto wafikirie, wakaniuliza kwa nini naivuruga Chadema kwa tamko nililolitoa hivi karibuni kutokana na mgogoro unaoendelea,” alisema.
Alisema kuwa alijitetea kwa kuwataka wakasome vizuri tamko lake, lakini waliendelea kumpiga na kumtaka aombe msamaha kwa kuishambulia Kamati Kuu ya chama hicho, jambo ambalo hakuwa tayari kulifanya kwa kuwa hakuona kama kuna kosa alilolifanya.
“Walinitupa na kutimua mbio wakiniacha nikiwa na maumivu makali. Nilitulia kwa muda na kujitahidi kuinuka na kupiga hatua kwenda nyumba zilizokuwa jirani kuomba msaada, hapo sikuwa na simu wala nauli,” alisema.
Alisema kuwa alipata msaada wa fulana na kuwasiliana na ndugu zake na polisi ambao baada ya muda walifika na kumpeleka Muhimbili kwa matibabu.
Hivi karibuni, Yona alitoa tamko la kupinga hatua ya Zitto kuvuliwa nyadhifa zake na Kamati Kuu ya chama hicho.
Kova aunda jopo la uchunguzi
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana kuwa ameunda jopo la wapelelezi wanane watakaoongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jaffari Mohamed kuchunguza tukio hilo.

 Chanzo:Mwananchi

Tuesday, January 7, 2014

HILAL MOHAMED (DADDY BROWN) AZIKWA LEO KIBAHA

Marehemu Daddy Brown enzi za uhai wake

 Baadhi ya rafiki waliojitokeza leo kwenda kuaga mwili wa marehemu hospital ya Muhimbili
 Muddy K mwenye flana nyeusi akiwa na Hassan daruiwesh na Adil katika hospital ya Muhimbili
 Ndugu na jamaa waliojitokeza

 Msemaji mkuu katika msiba huo Ustadh Juni akitoa maelezo na utaratibu utakavyokuwa
 Mwili wa marehemu ukibebwa kwenda kupumzishwa
Jerry Koto akiwa amebeba jeneza la rafiki yake Dady Brown
 Hapa ndio ikawa mwisho wa ndugu yetu rafiki yetu, jirani yetu Daddy Brown.
Mungu amlaze mahali pema peponi amin !

Monday, January 6, 2014

INASISIMUA NA KUTISHA ILA INAFUNDISHA

Katika kijiji cha Matare wilaya ya Mugumu
Serengeti, bwana Wambura alikamatwa kwa kesi
ya kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda jela
miaka mitatu. Huku nyuma akiacha mke na
watoto wanne waliokuwa wanasoma. Hukumu
hiyo ilimtesa sana kichwa chake, alitamani kila
mtu anayemhisi kuwa ana makosa aingie katika
moyo wake na kuupata ukweli. Alilia na
umaskini wake, labda angepata wakili mzuri
angeweza kumtetea, kumkosa wakili
kukahalalisha kifungo hicho!! Alikwenda
gerezani huku akiumia sana rohoni. Aliyaanza
maisha mapya kwa shida sana, akawamnyonge
kila mara na mwili ukapoteza afya kiujumla.
Huko gerezani alifanikiwa kupata rafiki
aliyekuwa na cheo ama jukumu la uzikaji wa
wafungwa hasahasa ambao hawakuwa na ndugu
ama ambao ndugu zao huwa hawajitokezi pale
gerezani. Mzikaji alijaribu sana kumtia moyo
Wambura na kumwaminisha kuwa hiyo ilikuwa
hatua tu ya maisha
anapaswa kuizoea na siku moja ukweli
utajulikana tu! Bwana Wambura maneno ya
mzikaji hayakumuingia kabisa.. alizidi
kunyong’onyea. “Siwezi kuvumilia kukaa
gerezani miaka mitatu…..kama unajali kilio
changu nisaidie nitoroke kwa namna yoyote ile
ndugu yangu!!” Wambura alimsihi mzikaji.
SIKU MOJA mzikaji akamwambia Wambura kuwa
msaada umepatikana. Lakini yataka moyo!!
“Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu nitoke
humu!!” alijibu kwa msisitizo huku akimtegea
sikio mzikaji. “Msaada pekee wa kukutorosha
humu ndani ni kwa njia ya jeneza… yaani
mfungwa akifa mimi nakuunganisha naye
kwenye jenerza…..” akashusha pumzi kisha
akaendelea “Wewe ukisikia kengele ya msiba,
njoo mara moja kwenye chumba cha maiti,
utakuta tayari sanduku liko katikati ya chumba
linakuwa halijafungwa, funua mfuniko ingia
ndani yake ulale pembeni ya maiti kwani
sanduku huwa kubwa la kutosha kila aina ya
maiti na hata miili miwili inaingia.
Kisha nitakuja na kulipigilia misumari. Baada ya
muda tutalipakia kwenye gari na kutoka kwenda
nje ya gereza makaburini nikiongozana na
baadhi ya wafungwa na maaskari magereza.
Tutakuzika huko lakini baada ya dakika 20 hadi
30 nitarudi kukufukua. Hautaweza kushindwa
kupumua kwa dakika hizo, utatoka ukiwa huru.”
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini lilimtisha
sana Wambura. Hata hivyo akaona afadhali
afanye hivyo
kuliko kukaa gerezani miaka mitatu
bila kosa. Siku moja akasikia kengele ya msiba.
Akafanya kama alivyoelekezwa na mzikaji.
Akaenda na kuingia chumba cha maiti. Kweli
akalikuta sanduku, akiwa na hofu
kuu akaingia na kulala pembeni ya maiti
iliyokuwepo. Mara akasikia mtu ameingia na
kulipigilia msumari sanduku. Muda mfupi
baadaye sanduku likainuliwa na kuwekwa
kwenye gari. Gari likatoka nje ya gereza hadi
makaburini. Sanduku likashushwa
na kuwekwa kaburini na kuanza kufukiwa.
Wambura alijitahidi sana kuvumilia japo hofu
ilizidi kutanda. Alimtegemea sana mzikaji na
alianza kumuona mkombozi wa maisha yake.
Kama alivyoambiwa, akasubiri
dakika kumi, ishirini.. zikapita kimya!! Dakika
thelathini kimya. Joto nalo likazidi kuongezeka.
“Nitavumilia hadi afike…” alijisemea kisha
akajiongezea kauli ya ujasiri.
“Kama nilitakiwa kuishi gerezani miaka mitatu
kivipi dakika kadhaa za hapa kaburini
zinishinde” KWA kuwa alishakaa gerezani kwa
muda kiasi akatamani kujua aliyekufa ni nani…
ni kweli aliogopa kuitazama maiti lakini aliona
kama inatisha zaidi ikiwa
imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi. Akaifunua
upande wa usoni… Kwa kuwa kulikuwa na giza
nene alikodoa sana macho kuitazama.
LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA
NA SURA YA MZIKAJI!!!
MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA AMEZIKWA NA
AHADI ZAKE ZA UKOMBOZI!!
________________
FUNZO::
Usimtegemee sana mwanadamu katika maisha
yako, kwanza ni dhambi!! Pili mwanadamu
anakumbana na vikwazo kama unavyokumbana
navyo wewe hadi kumwendea yeye. Hivyo
kumpatia maisha yako ni kuzidi kuyaweka
hatarini zaidi!!
Umeonewa umesingiziwa unanyanyaswa…..
mwachie Mungu afanye maamuzi…
_______________
Haya mzikaji aliyetegemea atamfukua naye ni
maiti…… tazama mateso atakayoyapata hadi
kufa kwake…..Bila shaka atatamani kurudi
gerezani kwa miaka mingine kumi
lakini haitawezekana tena!!!


Crdt: Harakati Zangu

MECHI YA FUNGA MWAKA:WAKONGWE WACHEZEA 6

 Mechi inayochezwa kila mwaka mara moja kati ya  wakongwe na vijana katika uwanja wa squad mwaka huu wakongwe wamechezea goli 6-3 wakongwe walikuwa wakiongozwa na David Beatus, Abdillah Ndonga, chale bonny, Jax Harambe, ngawina ngawina, Hassan Banyai, Peter Kabea,Kijiko, Abeid Mvuma, Photonatus Mang`wela, kablau, |salum Testa, Simon Bute, Kapilima, kessy mapande (geda)
 Vijana: Juma Malenga. Kibazo, Dilunga, Ngalema, West, Kibazo, Jafari Dikongwa, Tola, Samir Luhava, Magay John,
 Jax Harambe akijaribu kumtoka Jafari kaptain
 Photo me mratibu wa mashindano haya kila mwaka
 Hassan Banyai Ginks na Kablau
 Abeid Mvuma akiwa kazini
Hatari katika lango la timu ya Vijana