Pages

Sunday, May 26, 2013

JUMP OFF EPIC OPEN MIC YAWASHIKA TEMEKE

 Nash Emcee akiwa na King Zilla kaika tamasha la Jump off epic open mic ambayo dhumuni la tamasha hilo ni kutafuta vipaji vipya waandaji wa tamasha hilo walikuwa ni Times FM, Zantel na mtayarishaji wa \muziki wa Tanzania marco chali
 Umati wa watu waliofurika
 Crew ya Times FM: Bi Natasha, Cliford na Mona
 Walter Chilambo na Zila

 Ilikuwa hatari watu kibaoo
 Nash Emcee akifanya yake

 mmmmmmmmmmh hii kiboko
 

 King Zilla akitupa lakuchumpa
 Waliofanya burudani inoge Kobo na KU
 Mtayarishaji wa Muziki Marco Chali akiwaelezea wananchi kilichowapeka pale
Sie tusiesikia yalitukuta haya
 Fella na babu Talle
 Walter \chilambo alifanya kazi nzuri
 Rais wa Manzese Madee aliinyamazisha Temeke kwa muda
 Madee anamtafuta aliyemwaga pombe yake

 Vinega: Mapacha na Rama dee

 Ney wa Mitego
 hapa unapigwa Muziki gani kati Diamond na Nay wa Mitego utaona video yake baadae hatari
 Mkubwa Fella akijaribu kuongea na mtu aliyetaka kuharibu sherehe
Big Jah ndio alikuwa mambo yote pamoja na Fella na Promota Bonga

NASH EMCEE ALIPOTEMBELEA BUNGE NA KAULI ALIYOTOA



Na hiki ndicho alichosema:

NA HAYA NDIO MAMBO YA DODOMA,BAADA YA KUHUDHURIA KIKAO CHA BUNGE JUMATATU,NA SIKU HIYO PIA NILIFANYA KAZI KATIKA STUDIO ZA AFTER HISTORY NA MTAYARISHAJI WA KUITWA,DOUBLE!! KWA KWELI KWA JINSI NILIVYOISIKILIZA NA KUIELEWA HOJA YA BAJETI... KUTOKA WIZARA YA HABARI,VIJANA,MICHEZO NA UTAMADUNI ILIYOSOMWA NA WAZIRI MWENYE DHAMANA KATIKA WIZARA HIYO,KWA UPEO WANGU MDOGO,NI WAZI SERIKALI HAINA MPANGO WOWOTE WA KUWASAIDIA WASANII WA TASNIA ZOTE KULINGANA NA MAELEZO YA BAJETI YAO,NA HILI LILIWEKWA WAZI NA MBUNGE NYAMBARI NYANGWINE KWA KUSEMA KAULI YA DHARAU KWA WASANII ETI,YEYE ANATAMBUA WASANII AU MSANII NI YULE MUANDISHI WA VITABU TU. KWA KAULI KAMA HIZO WASANII WENZANGU KAENI MKIJUA KUA SERIKALI HAIPO NA SISI,NA HAINA MUDA WA KUPAMBANA NA HUO UNAOITWA UHARAMIA SIJUI UPUUZI GANI, NDIO MAANA TAMADUNIMUZIK TUNASAMBAZA WENYEWE KAZI ZETU NA KUBUNI VITU KAMA KILINGE!NASAHA ZANGU KWAKO MSANII,PIGANA,PAMBANA HAKIKISHA UNASIMAMA MWENYEWE IWE KWA SHIDA AU KWA RAHA!!NAWASHUKURU VINEGA KWA KUNIPA MUALIKO NA HAYA NDIO MAWAZO YANGU.KWA MUNGU KILA JAMBO LINAWEZEKANA! MWENYEZI MUNGU TUBARIKI!!!

DJ MAX ASHEREHEKEA UBINGWA

 Huyu ni DJ MAX mtoto wa Tandika ambaye kwa ss yupo Ujerumani akishangilia ushindi wa Bayern jana na pia ni mwendeshaji wa blog ya djmaxwaziri.blogspot.com


Wednesday, May 22, 2013

AJALI: LORI LA MAFUTA LAPINDUKA MACHINJONI

 Lori la mafuta ya kupikia limepinduka leo asubuhi maeneo ya Chang`ombe Machinjoni, hapa lori likiwa limeiangukia gari
 Kufa kufaana mafuta yaliyomwagika watu wakapata kazi za mda
kazi ya kusomba mafuata inaendelea halafu tunakuja kuuziwa.

 Mafuta yakiendelea kuchotwa
Gari ikiwa imeharibika vibaya

Picha: Mdau
Filemon Rupia

Saturday, May 18, 2013

MUSSA MUDDE HATUA KWA HATUA ALIVYOKOSA PENATI

 Anajiandaa kupiga
 Musa Mude anaanza kuupiga mpira mwangalie bartez keshamuibia
 Bartez anafanikiwa kuruka unapopigwa mpira
 Bartez anadaka mpira ambao ulikuwa mwepesi mno
 unamponyoka bartez
anaufatilia

WATANI WA JADI: YANGA YAITAMBIA SIMBA

 Wapenzi wa mpira waliofurika uwanja wa Taifa kuona mechi ya watani wa jadi
 Napunguza uongo foleni ilianzia Taifa mpaka Uhasibu
 Hii mechi ilikuwa kati ya SIMBA B na YANGA B ambayo simba ilishinda 1

 Hapa ndio picha linaanza wachezaji wa Simba wakiingia uwanjani kwa maandalizi ya mechi




 Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na Kavumbagu




 Goli la pili lilifungwa na HAmisi Kiiza

 Hapa refa sijui nini kilimsibu
 Refa akipata huduma ya kwanza baada ya kuanguka
 Kocha msaidizi wa Yanga Fred Minziro akibebwa juu baada ya ushindi wa 2-0
Jukwaa linaandaliwa