Pages

Monday, April 29, 2013

MDAU FELIX MWAGARA APATA JIKO

 Mda wa mapozi
 Keki

MBAGALA NA VITONGOJI VYAKE

 Mbagala Charambe
 Charambe msikitini
 Kwa Mbiku
 
Magengeni


Mzunguko wa Mbagala inayogawanya Charambe, Kongowe, na Mjini
Rangi tatu stendi

Hospital ya Zakheim
Mtoni Darajani

Friday, April 26, 2013

WATOTO WA TMK NDANI YA UK


Kushoto: Hamadi Akida, Isla, Agili pamoja na Saidy Akida

Ngoma Africa Band inawatakia kila heri ya miaka 49 ya MUUNGANO wa Tanzania

Bendi ya muziki wa dansi "Ngoma Africa Band" a.k.a FFU yenye maskani nchini
Ujerumani
inawatakia kila la heri na fanaka ya MIAKA 49 YA MUUNGANO wa jamuhuri ya TANZANIA, watanzania wote popote walipo.
Muungano wetu wa bara na visiwani ni muungano wa undugu wa damu.
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ubariki Muungano wetu.

MIAKA 49 YA MUUNGANO WA TANZANIA






JITEGEMEE ALUMNAE REUNION YANOGA

 Baadhi ya wanafunzi mbalimbali ambao walisoma jitegemee leo wamekutana katika Jitegemee alumnae Reunion ambayo lengo ilikuwa ni kukusanya fedha za kuisaidia shule hiyo, na vitu mbalimbali viliuzwa kwa mnada













Thursday, April 25, 2013

HISIA THEATRE WATEMBELEWA NA WAGENI

 Kundi la sanaa ya asili Hisia theatre walipotembelewa na wageni wao leo. hapa baadhi ya viongozi wa Hisia Theatre wakiwa katika picha ya pamoja katika ofisi zao Temeke Sandali
 Wacheza ngoma






Saturday, April 20, 2013

AZAM FC YAPATA SULUHU KWA AS FAR RABBAT









Mechi  ya kombe la shirikisho baina ya Azam fc ya Tanzania dhidi ya timu ya jeshi la Morroco AS FAR Rabat imemalizika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kwa matokeo ya suluhu pacha ya bila kufungana.
Katika mchezo huo timu zote mbili zimekosa nafasi nyingi za kutia mpira nyavuni huku dakika za mwisho waarabu wa Morroco wakijiangusha mara kwa mara kutaka suluhu ugenini.
 Azam FC imeshindwa kutamba katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Emile Fred kutoka Shelsheli na endapo ingeshinda ingejiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele hatua ya makundi.
 Sasa Azam watakuwa na kibarua kizito huko kaskazini mwa Afrika wiki mbili zijazo kwani watahitaji ushindi tu na si vinginevyo.
Kama wawakilishi hao watanzania watahitaji kujaribu bahati yao watahitaji kulazimisha suluhu ugenini ili sheria itumike, lakini kama watahitaji kusonga mbele ndani ya dakika 180 watalazimika kupata matokeo ya ushindi.
Katika dakika ya mwisho ya mchezo huo nyota wa Azam Kipre Herman Tchetche alipiga bunduki moja iliyogonga mtambaa panya na baada ya hapo mwamuzi Fred alipuliza kipenga cha mwisho kuashiria ngoma imemalizika.
Akiongea baada ya mechi hiyo kocha mkuu wa Azam fc, mwingereza Sterwat John Hall alisema ni matokeo mabaya kwao kwani wanahitaji kujipanga vizuri mechi ya marudiano.
“Tumepoteza nafasi nyingi, bahati haikuwa yetu lakini tunaweza kubadili matokeo tukienda kwao kwani katika soka kila kitu kinawezekana”. Alisema Hall.
Kocha huyo aliongeza kuwa timu yake ilicheza vizuri na kwa umakini sana lakini bahati haikuwa yao