Pages

Monday, January 30, 2012

FOLENI ZA MWISHO WA MWEZI

 Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB tawi la Temeke Sudani wakiwa katika foleni kusubiri kuingia ndani ya Benk hiyo kuhudumiwa
Kila kona watu kibao

MTO RUFIJI

 Kivuko cha Mto Rufiji
 Duh! huu mtumbwi akipita kiboko tu karibu ya huu hatari
Mtumbwi ni moja ya kivuko kikubwa wanachotumia wakazi wa maeneo ya Rufiji na pembezoni mwake

Saturday, January 28, 2012

WASHEREHEKEA MIAKA 50 YA NDOA YAO (GOLDEN JUBILEE)

Wapendanao Bw & Bi.Mohamed Mturo wakiwa na wajukuu zao katika sherehe yao ya kuazimisha miaka 50 ya ndoa (GOLDEN JUBILEE) walifanya kisomo cha kumshukuru Mungu nyumbani kwao Temeke Mtaa wa Mji mwema


Wanazuoni wakisoma dua ya kuzidi kuwatakia heri wanandoa hao

Mzee Mbonde kushoto akiwa na rafiki Mzee Mturo

Baadhi ya wanafamilia waliouhudhuria katika sherehe hiyo
Keki ya ukumbusho

unaweza kuitafsiri hii picha inasemaje


Na hii
Mjukuu akimlisha keki babu
Hivi unakumbuka tulikutana wapi!mmmmmmmmmh

Wednesday, January 25, 2012

STICKO-MUSALA UNONO

Msanii wa Kundi la Wanaume family family ametambulisha video yake mpya inayoitwa Musala Mnono akimshirikisha msanii wa zamani wa kundi la B Love M Masiga

Monday, January 23, 2012

TEMEKE SQUAD YAIFUNGA BANDARI

 Wachezaji wa Timu ya Temeke Squad wakikaguliwa kabla ya mchezo kuanza

 Wachezaji wa Timu ya Bandari
 Captain wa Temeke Squad Ibrahim mwenye jezi nyekundu pamoja na Captain wa BAndari Kijiko wakiwa picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo huo.

 Moja ya matukio katika mchezo huo

Moja ya hatari zilizotokea katika lango la Bandari, mpaka mechi inaisha Temeke squad ilishinda 1-0

Timu ya soka ya Temeke Squad imeweza kuifunga Bandari maarufu Cargo nayo ya Temeke katika mashindano yanayoendelea katika viwanja vya Bandari Tandika vya kumtafuta Bingwa wa Wilaya ya Temeke, mpaka sasa Temeke Squad imecheza mechi mbili na kujikusanyia point 4 na Bandari imecheza mechi mbili ikiwa na pointi tatu baada ya kupoteza mchezo huo. Kocha wa Timu ya Bandari Ngawina Ramadhani amesema timu yake inabidi ijilaumu kwani hawakucheza vizuri kama inavyokuwa na wapinzani walipata nafasi na kutumia na inabidi tujipange na mechi zijazo

Thursday, January 19, 2012

WASAIDIWE WATOTO HAWA

KATIKA gazeti la Uwazi, toleo la wiki iliyopita tulitoa habari za mtoto Mustafa Ally, 12, (pichani), mkazi wa Mtoni Mtongani, Wilaya ya Temeke  jijini Dar es Salaam anayewauguza wadogo zake  mapacha wenye umri wa miezi nane.
Mtoto Mustafa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Twiga, Temeke amelazimika kuwauguza wadogo zake hao, Swaumu na Ramadhani kwa kuwa  baba yao alishafariki na mama yao yupo mahututi.
Watoto hao mapacha wanaumwa na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mama yao aliyekuwa akiwauguza aliugua ghafla na kupewa matibabu na kwa sasa yupo hoi nyumbani kwake, hivyo Mustafa kuchukua mzigo huo wa kuwauguza.
Matatizo yanayoikabili familia hiyo ni pamoja na ukosefu wa chakula, nguo za kawaida na za shule, fedha za matumizi, maziwa ya unga ya watoto na kodi ya nyumba.
Gazeti hili kwa niaba ya familia hiyo linatoa shukrani kwa watu mbalimbali waliompatia msaada wa maziwa, sabuni, sukari, nguo na fedha, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 300,000.
Bado msaada unakaribishwa kwa watoto hawa. Aliyeguswa na kilio cha mtoto Mustafa afanye mawasiliano na Afisa Ustawi wa Jamii Muhimbili,  Erika Ishengoma kwa simu 0714 220 038 au mwandishi wetu kwa namba 0713 454 656 au afike Muhimbili wodi ya watoto, Makuti B atakutana nao ana kwa ana.


GARI LAKUTWA KWENYE VYUMA CHAKAVU

 Gari ambalo lilisombwa na mafuriko siku za nyuma Dsm limekutwa kwenye sehemu ya vyuma chakavu likitaka kuanza kukatwa lakini walikuwa hawajawahi kulikata.

 Gari lilivyokuwa ndani baada ya kuanza kuondolewa viti


Gari ambalo limenusurika kukatwa na wauza vyuma chakavu -Temeke

TFF INATAKA TUSHUKE DARAJA-AFRICAN LYON

Kwa masikitiko makubwa sana, uongozi wa timu ya African Lyon Fc ambayo maskani yake Temeke Sigara inapenda kuwaeleza watanzania hususani wapenzi wa mpira wa miguu kuwa, katika jitihada zote za timu yetu ya kukuza na kuedeleza soka hapa nchini, Tumekuwa na mahusiano MABAYA SANA na chama cha mpira wa miguu yaani TFF.
Napenda kuweka wazi bila kificho chochote kuwa TFF imekua ikitukandamiza na kutuchafua mbele ya jamii kwa makusudi. Tena ni kana kwamba si mtu mmoja ndani ya TFF bali ni kuwa agenda ya TFF nzima.
Kuanzia kwa Rais wa shirikisho kamati ya mtendaji, kamati ndogondogo na pia sekretarieti cha kusikitisha kama si kufurahisha mpaka kwa walinzi wa milangoni siku za mechi.
Napenda nitoe baadhi ya mifano michache ambayo tunakutana nayo katika jitihada zao za kutuyumbisha pamoja na vilio vyetu vya kila siku.
  1. RATIBA YA LIGI KUU.
Timu zote ambazo zimekua zikienda kucheza mechi kanda ya ziwa zimekuwa zikicheza mechi zote mbili(yaani kucheza na Toto Fc na Kagera sugar). Kitu ambacho African Lyon Fc chini ya uongozi wetu hatujawahi kukutana nacho.
Nakama hiyo haitoshi mechi yetu ya mwisho wanatupeleka Manungu Turiani kucheza dhidi ya JKT Ruvu na hali sisi na JKT uwanja wetu ni Chamazi alafu wenyeji wa Turiani (mwenye Uwanja wao) Mtibwa wanapelekwa Morogoro kucheza dhidi ya Moro United.
Ni vigezo vipi vilivyowekwa kutupeleka sisi na si Simba wala Yanga. Je hii TFF ni ya Simba na Yanga tu.
  1. MBWANA SAMATA
Ndugu watanzania, Tumeandika barua zaidi ya 15 kwa sekretarieti,kamati ya haki ya wachezaji, Raisi Tenga. Lakini hakuna yeyote aliyezungumzia jinsi ambavyo Simba imegushi uhamisho wa Mbwana Samatta kutoka African Lyon Fc. Cha kushangaza ndugu Alex Mgongolwa ambaye pamoja na kupelekewa barua yetu TFF ofisini kwake,kaibuka na timu ya Kimbangulila Fc na African Lyon tumeachwa bila hata kusikilizwa.
Napenda kumlaumu kwa nguvu zote ndugu Alex Mgongolwa kwa makusudi yake kabisa tena kwa kukusudia ya kugoma kukaa na sisi na kutisikiliza. Na kwa dharau yake ya kushindwa hata kutujibu japo moja ya barua zetu.
Na kwa kuonyesha chuki za wazi kwetu ni pale ambapo aligoma kukutana na WAFADHILI wetu aliokuja kutoka Marekani na Uarabuni kutaka kujua maswala haya hususani ya MBWANA SAMATTA. Hawa ni watu waliotumia fedha na mda wao kuja nchini kwetu alafu mtu anagoma.
Na si yeye tu aliyegoma hata uongozi wa juu wa TFF uligoma kukutana nao ili hali hawa wote walipata taarifa wiki moja kabla juu ya ujio wa wageni hawa.
  1. YUSUFU SOKA
TFF kupitia kwa kaimu Katibu mkuu wake bwana Sunday Kayuni na wakala waliamua kumpeleka Sweden mtaja hapo juu na tunasikia kuwa hivi sasa yupo Jela. Tunalaani na tunaomba vyombo vya dola viingilie kati na sheria ichukue mkondo wake vielelezo vya mchezaji alivyoondoka na wahusika wa safari yake tunavyo.
  1. TIKETI ZA MILIONI 35
Mwaka 2009 TFF walituomba tuwaletee tiketi toka Marekani zenye thamani ya shilingi milioni 40 na wakaturudishia tiketi za shilingi milioni 5 zilizobakia baada ya kutumia katika mechi kadhaa hivyo kwa sasa tunawadi milioni 35. Tiketi zenyewe zilitumiwa kwa mechi mbalimbali zikiwemo za Kilimanjaro Taifa Cup na Kagame cup. TFF wamekuwa mara kwa mara wanatoa ahadi hewa juu ya malipo yetu. Hii inatufanya tuzidi kuamini kuwa TFF haina nia nzuri na timu yetu African Lyon Fc. Tunaomba tulipwe.
  1. SWALA LA KASSIM DEWJI
TFF nathubutu kusema kuwa haiko makini kwa jambo lolote lile hapa nchini, baada ya sisi kununua timu 2009/2010. Timu yetu ilipata zawadi ya sh.milioni 5 kama timu yenye nidhamu bora cha kushangaza kaimu Katibu mkuu ndugu Sunday Kayuni alimuandikia hundi kwa jina la Kassim Dewji,huku akijuafika kuwa sisi ndio tunaomiliki timu, na hata kama angekuwa yeye ni mmiliki bado jina lingekuwa ni la timu na sio la mtu binafsi.
Kuna uwezekano mkubwa sana hela hizo viongozi wa juu kabisa wamegawana na ndio maana wanalikingia kifua. Tunataka hela zetu, hii ni haki ya wachezaji.Ni nidhamu gani aliyoonyesha uwanjani Kassim Dewji mpaka apewe yeye?
  1. FEDHA ZA VODACOM 2010 – 2011
Jamani hadi leo hii tumepokea shilingi 3.5 milioni tu. Je wenzetu wote wamepewa hivyo? Vodacom wanajua? Halafu wanataka bado tuvae jezi za Vodacom ambao udhamini wao ni wa hela ya mboga. TFF wanajipaka matope na aibu iwakute kwa wizi wa mchana kweupe.
TAMKO LA AFRICAN LYON
African Lyon Fc kwa nguvu zetu zote na tunapenda tuelewe kuwa TFF ina mpango madhubuti wa kuishusha timu yetu daraja kama si kuiondoa kwenye ramani ya soka.
Hivyo basi tunatoa siku 30 kwa TFF kukutana nasi na kuzungumzia matatizo yetu na kama ikishindikana basi sisi tunajitoa kwenye ligi pasipo kujali chochote.

TAMASHA LA WAZI LA JINSIA

 Kikundi cha sanaa cha Maonyesho cha Sageta wakierimisha jamii kwa njia ya nyimbo katika viwanja vya Temeke Buriaga



 Baadhi ya wasanii wa kikundi cha Sageta wakitoa burudani katika tamasha la wazi la jinsia la wanaume tuwajibike na vunja ukimya ambayo ndi kauli mbiu ya Tamasha hilo

Sunday, January 15, 2012

AROBAINI YA RICHARD MAYABU: RICH TALL

 Masheikh wakisoma dua ya kumuombea marehemu Rich aliyofanyika nyumbani kwao Temeke Mikoroshini

 British mwenye nguo nyeupe pamoja na Salum Nyumba

 Hapa watu waliofika wakipata riziki kabla ya kutawanyika

 Kwenye Sekta hii huku kwetu hamna masihara kabisa Chanya, Haji Sophy na Mudy tall wakipata riziki


 Sayana Mwalongo akiwa na Juma Bakari Kidishi

 Baadhi ya rafiki wa karibu wa familia wakijaribu kuweka mambo sawa

Usher first Lady Tayana mmoja waliohudhuria katika arobaini hiyo

Saturday, January 14, 2012

Gogo Mzome; nimeona mengi chumba cha maiti kwa miaka 20

 Gogo Mzome akiwa kazini
Na Florence Majani
WASWAHILI husema kazi ni kazi, bora mkono uende kinywani. Lakini, zipo kazi ambazo wengi katika jamii huzikimbia na wakati mwingine kuzipa majina mengi.hili si jina geni kwa wakazi wa Temeke,maeneo ya chan`gombe Usalama, evereth, Mwembeyanga, Mtaa Yombo nk
Lakini, kuna dhana imejengeka katika jamii kuwa kufanya kazi katika chumba cha kuhifadhia maiti, lazima uwe kichaa au pengine mtu ambaye umejitoa mhanga kweli.
Ni nini ukweli kuhusu maisha katika chumba cha maiti na nini majukumu ya mhudumu wa chumba kile?
Safari ya Mwananchi katika chumba hicho katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  jijini Dar es Salaam inaanza!
Jokofu  la kwanza linapofunguliwa inaonekana miili mitatu. Ule  wa kwanza ni wa mfungwa, alitambulika kutokana na sare zake. Huyu  alikuwa na jeraha kubwa usoni …  huku ngozi yake ya  kichwa ikining’inia.
Mwingine wa pili ulikuwa umefunikwa kwa shuka gubigubi, lakini shuka hilo lilikuwa limejaa damu usoni na wa tatu ulikuwa kawaida.
Kulia kwangu kilikuwapo chumba kingine kikubwa. Hicho kilikuwa na wanaume wanne walioonekana kutingwa na kazi zao za kila siku. Kila mmoja alikuwa  mbele ya meza ya chuma akiushughulikia mwili wa marehemu.  Miili  yote ilikuwa  ni  ya wanaume. Walikuwa wakisafishwa tayari kwa maziko.
Mtu anayenitembeza katika milki hii ya kutisha si mwingine bali amejitambulisha kuwa  Gogo Mzome Abdallah. Yeye ni mhudumu mkuu katika chumba cha kuhifadhi maiti (mortuary) cha MNH.
Kama wewe ni mfiwa na umekwenda kuchukua mwili wa nduguyo na kuwakuta wahudumu hawa wakipiga soga- huku wakicheka - wakiwa ndani ya sare zao za suti zenye rangi ya bluu bahari, utadhani hawana huruma, wala hawayajui machungu ya kufiwa. Lakini, yakupasa ukumbuke kuwa … wapo kazini!
Novemba 1991 ndicho kipindi ambacho Mzome aliajiriwa katika kitengo hiki cha uhifadhi miili ya marehemu hapo MNH.
Wakati huo, Mzome anasema alikuwa na  umri wa miaka 34. Anasema, hakulazimishwa, wala hakwenda kwa kubahatisha bali alifika mwenyewe mahali pale (Muhimbili) na kuomba kazi.
Hawezi kusahau siku yake ya kwanza kazini:  “Nilipoanza kuonyeshwa maeneo yangu ya kufanya kazi, ikiwamo kazi nitakazokuwa nafanya, nilinyong’onyea. Miguu yangu iliishiwa nguvu,” anaanza Mzome katika simulizi yake.
Anasema alijisikia  hali ya ukiwa kwa saa tano baada ya kuanza kazi, lakini baada ya hapo aliyaelewa majukumu yaliyompeleka mahali pale na alianza kuchapa kazi.
Kazi  kubwa  ya wahudumu wa maiti ni nini?
Mzome anajibu  kuwa, kazi kubwa ni kuipokea miili ya marehemu na kisha kuihifadhi. Miili hiyo inapohifadhiwa katika majokofu huwekwa jina na namba kwa ajili ya kuitambua.
Huduma nyingine tunazozifanya ni pamoja na kuosha miili  hiyo endapo wafiwa watataka huduma hiyo, ambayo hulipiwa Sh25, 000, kuwachoma dawa ili wasiharibike na kuwasitiri
Huduma nyingine ni kuweka rekodi ya kila mwili wa marehemu unaofika hapo.
Anaongeza  kuwa, wafanyakazi wote wa kitengo hicho hupewa mafunzo na madakatari wa pathologia ambapo  pamoja na mambo mengine huelekezwa jinsi ya kumdunga marehemu dawa maalum(formaline) ya kuzuia mwili usiharibike.
Wakati mwingine tunapasua maiti ili kuweka dawa kwenye miili inayosafirishwa nje ya nchi ili isiharibike.
Hali kadhalika sisi husaidiana na madaktari kufanyia uchunguzi mwili wa marehemu (post mortem), anasema.
Mauza uza ndani ya chumba cha maiti
Wengi wetu tumekuwa tukisikia dhana au hadithi mbalimbali kuwa, yapo matukio ya ajabu  katika vyumba vya kuhifadhi maiti.   Kwa mfano, maiti kufufuka, kusikia maiti zikisemezana katika majokofu na mengine mengi.
Mzome anakanusha uvumi huo na kusema: Katika miaka 20 niliyofanya kazi  humu sijawahi kuona  vitu kama hivyo. Huo ni uvumi na woga tu, hata ukiwa nyumbani ukiwa mwoga utahisi mauzauza,
Anakanusha dhana nyingine kuwa,  wahudumu wa chumba cha maiti hawawezi kufanya kazi mpaka walewe pombe au wavute sigara au bangi , na kusema kuwa, yeye hafanyi kazi akiwa amelewa hata siku moja
Hata hivyo, Mzome anakiri kuwa, wakati mwingine hukumbwa na hofu  na simanzi kwani baadhi ya miili huletwa ikiwa  imeharibika vibaya au imeoza.
Hii kazi wakati mwingine haina raha bwana! Hakuna picha ya kutisha kama maiti iliyooza, au iliyoungua. Lakini, kwa sababu tupo kazini, sisi huzihudumia maiti hizo vile inavyotakiwa, anasisitiza Mzome.

Changamoto kuu
Gogo Mzome anasema kuwa, changamoto kubwa ambayo amekutana nayo katika miaka yake 20 ya kufanya kazi katika chumba cha kuhifadhi maiti ni kuwahudumia wafiwa.
Mara nyingi wafiwa huwa katika hali ya  kuchanganyikiwa. Hawa wanataka uhuzunike nao, lakini utalia mara ngapi kwa siku?  Yakupasa kuwahudumia kwa  hekima ili wasijisikie vibaya, anasema.
Mzome anaikumbuka siku alipokuja mwanamume mmoja kutafuta mwili wa marehemu, lakini hakuwa akitoa taarifa kamili.
Alipoambiwa akahakikishe majina ya marehemu  ndipo arudi kuutafuta mwili wa nduguye, alilipuka kwa hasira na kumwambia Mzome Ndiyo maana kazi yenu ni  kucheza na maiti tu.Mzome anaizungumzia kazi yake na kusema, hakuna kazi inayohitaji umakini kama ya kuhudumia maiti.
Ukifanya kazi hii unatakiwa uwe makini mno! Maiti hasemi, kama ndugu wasipotoa taarifa kamili za marehemu wao au wakawa waoga kumtambua, unaweza ukafanyika uzembe wa hali ya juu, anasema.
Analikumbuka tukio moja ambapo wafiwa walikuwa waoga kuutambua vyema mwili wa ndugu yao na mhudumu hakuwa makini,  hivyo wakachukua mwili  wa marehemu mwingine.
Lakini tuliwawahi kabla hawajaaga. Tulipowaeleza ilibidi waahirishe kila kitu na kuanza upya kumhudumia marehemu wao halisi, anasema.

Mzome: Ninawapenda maiti
Katika kazi yake Mzome anasema amejifunza kitu kimoja. Nacho ni upendo. Anasema, binadamu wote ni marehemu watarajiwa hivyo yatupasa tuishi kwa upendo.
Mimi ninajifunza mengi hapa, leo unazungumza na mtu, anacheka, pengine ana mipango  ya kufunga ndoa, lakini kesho analetwa hapa tayari ni marehemu.
Kwa hiyo, nawapenda  na kuwahudumia maiti  kwa upendo, kwani hata mimi kesho nitakuwa marehemu na sijui atakayenihudumia,aAnasema Mzome akionyesha kuwa na hisia kali.
Anasema, kwa kuwa maiti hazungumzi basi isiwe kigezo cha kumhudumia vibaya.
Siku asiyoweza kusahau
Mzome ambaye ni baba wa watoto wanne na mke anasema, hataweza kuyasahau matukio mawili katika kipindi chake chote cha ajira hapo Muhimbili.  La kwanza ni siku kilipoletwa kichwa cha mtoto Salome.
Sitalisahau tukio la kijana Ramadhan ambaye alikutwa maeneo ya Muhimbili akitafuna kichwa cha mtoto Salome.
Basi, tuliletewa hapa kichwa, na baadaye kiwiliwili. Kichwa cha mtoto yule kilikuwa kimesukwa vizuri maskini! Liliniuma mno tukio hilo, anaeleza.
Anaongeza na kusema, tukio la pili ni la ajali ya  basi huko Yombo Dovya. Marehemu walikuwa wanakuja vipandevipande, wengine ubongo katika mfuko wa rambo, yaani vilikuja viungo na si miili.
 Hali kadhalika anakumbuka siku ya kwanza kuingia zamu usiku ambapo alihisi analala na maiti na hakufumba jicho, mpaka kulipopambazuka.

Alificha siri kwa mwaka mzima.
Alipoajriwa katika kitengo hiki cha kuhudumia maiti, hakutaka watu wafahamu wapi anapofanyia kazi. Awali, aliona ni kazi ya aibu. Hakuwaficha marafiki tu, bali  hata mkewe.
Kila mara mke wangu aliponiuliza  nafanya kazi wapi nilimwambia kwa kifupi: Muhimbili. Lakini, baada ya kupita mwaka mmoja nikasema potelea mbali, na nikampasulia jipu, Anasema huku akiangua kicheko kikubwa.
Gogo Mzome  ni baba mtu mzima mwenye umri wa miaka 55 sasa, ana uzoefu wa hali ya juu katika kitengo cha kuhifadhi miili ya marehemu. Anatoa wito kwa Watanzania kuachana na dhana kuwa kazi hii ni ya fedheha.
Hii ni kazi kama kazi nyingine. Nisipofanya mimi atafanya nani?” anauliza Mzome.
Naye  Mkuu wa Kitengo cha Kuhifadhi Maiti MNH, Dk Innocent Mosha anasema pamoja na  moyo wa ujasiri, kazi hiyo inahitaji uzoefu na umakini wa hali ya juu.
Ukifanya uzembe kidogo tu unajitia matatani. Kwa mfano, maiti za watoto wachanga mara nyingi huchanganya watu, utakuta wote wawili wana majina kwa mfano, Mwajuma Saleh, halafu wanafanana, basi hapo utata mzito hutokea, anasema Dk Mosha.
Dk Mosha anaongeza na kusema, wahudumu wa chumba cha maiti hutumika pia kufanya uchunguzi katika miili ya marehemu wakishirikiana na madaktari.
Hali kadhalika anatoa wito kwa Watanzania kujenga tabia ya kuifanyia miili ya marehemu uchunguzi (postmortem)kabla ya kuzika.  Nia ni kujifunza na kupata ukweli wa chanzo cha kifo badala ya kuhisi.

SHUKURANI NA TAARIFA YA AROBAINI

Maskani ya Good Hope ya Temeke Dar es Salaam inatoa shukrani za dhati kwa ndugu, rafiki na jamaa wote walioshiriki katika kipindi kigumu na majonzi makubwa baada ya kupata taarifa ya msiba ya ndugu ya Richard Mayabu kulichotokea tarehe 3/12/2011 na kuzikwa tarehe 4/12/2011

Familia inashukuru sana! na tumepata faraja kubwa sana toka mwanzo wa msiba mpaka maziko. Tunamuomba MwenyeziMungu awajaalie kila la kheri kwa yote Inshallah

Familia inapenda kuwafahamisha kwenye kisomo cha Arobaini Marehemu ya Marehemu Richard Mayabu itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 15/01/2012 nyumbani kwao Temeke Mikoroshi maeneo ya Sandari saa 5.00 asubuhi


Mdau
Sayana Mwalongo
Maskani ya Good Hope, Temeke

Friday, January 13, 2012

CCM Keko Machungwa waomba mgogoro wao kutatuliwa

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), tawi la Keko Machungwa B wilayani Temeke, kimeuomba uongozi wa chama hicho mkoa kuingilia kati mgogoro uliopo baina ya uongozi wa tawi hilo na wilaya unaoweza kuwapoteza zaidi ya wanachama 444 waliopo katika tawi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa tawi hilo, Andrew Kisalu alisema kwa muda mrefu uongozi wa pande hizo mbili umekuwa na mgogoro wa chini chini aliodai ni hatari na unaweza kuwasarambatisha wanachama wakati wowote.


Alisema mgogoro huo kimsingi hauna maslahi kwa chama hicho na sasa umefikia hatua ya kukwamisha ununuzi wa jengo linalotumiwa kama ofisi ambalo mmiliki wake alishatangaza kuliuza tangu mwishoni mwa mwaka jana huku akitoa kipaumbele kwa chama hicho.


Kisalu alisema baada ya uongozi wa chama hicho tawi kuwasiliana na mwenye jengo hilo, walikubaliana kumpatia fedha anazohitaji kiasi cha Sh milioni 15 ambazo waliziomba kutoka makao makuu ya chama kupitia ngazi ya Kata na Wilaya.


“Matokeo yake hadi hivi sasa bado hakuna dalili zozote za kupata fedha hizo na kila tulipojaribu kufuatilia tulibaini kuwapo kwa ukwamishaji katika ngazi ya chama wilaya, suala linaloweza kusababisha tulikose jengo hili tunalolihitaji kwa nguvu zote,” alisema Kisalu.


Alisema kwa taarifa zilizopo jengo hilo pia linatakiwa na chama kimoja cha siasa kwa gharama ya Sh milioni 18 ili walitumie kama ofisi, jambo alilodai kuwa bado halijakubaliwa na mmiliki wake kwa vile pia ni mkereketwa wa CCM hivyo kipaumbele chake anatoa kwa chama chake.


Aidha alisema tangu waanze kulitumia jengo hilo kama ofisi mwaka 2008, mbali na kupata mafanikio ya kuongeza idadi ya wanachama.


Aliwaomba viongozi wa juu wa chama hicho kulitafutia ufumbuzi suala hilo haraka ili kukinusuru chama hicho na wanachama wake kwani tayari kimeweza kujijenga vizuri huku kukiwa na maombi mengi kutoka kwa wanachama wengine wanaotaka kujiunga.

Monday, January 9, 2012

Nigeria yazizima kwa mgomo wa mafuta

Mgomo wa nchi nzima umeitishwa nchini Nigeria kupinga kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta ambayo imesababisha shughuli za nchi hiyo kusimama.
Maduka mengi, ofisi, shule na vituo vya mafuta nchini humo vimefungwa katika siku ya kwanza na mgomo ulioitishwa na vyama vya wafanyakazi.
Maelfu ya watu wamekusanyika mjini Lagos na miji mingine kupinga kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta ambayo imesababisha kupanda mara dufu kwa bei ya mafuta na gharama za usafiri.
Rais Goodluck Jonathan alisema ruzuku hiyo ina athari za kiuchumi.

Risasi

Mitaa ya Lagos ambayo kawaida huwa imejaa watu imekuwa kimya, isipokuwa kwa doria za polisi na watu wanaoelekea kwenye mikutano ya hadhara.
Maelfu kadhaa ya watu wamekusanyika katika eneo la wazi la Gani Fewehinmi mjini humo na wengine wengi wanaendelea kuwasili, anasema mwandishi wa BBC Mark Lobel aliyepo nchini Nigeria.
Nigeria
Wananchi wa Nigeria wamekasirishwa na kuondolewa kwa ruzuku
Kumekuwa na taarifa kuwa mwandamanaji mmoja amepigwa risasi na kufa mjini Lagos.
Katika mji wa Kano kaskazini mwa nchi hiyo, polisi wamefyatua mabomu ya kutoa machozi na kupiga risasi hewani kutawanya maelfu ya waandamanaji waliokuwa wakikusanyika katika ofisi ya gavana. Watu 12 walijeruhiwa, alisema mwandishi wa BBC Idhaa ya Kihausa Yusuf Ibrahim mjini humo.
Mjini Abuja, vizuizi vimewekwa na kusababisha uwanja wa ndege kufungwa, na hivyo kuzuia ndege kupaa na kutua, anasema Ibrahim Shehu Adamu wa BBC akiwa katika mji huo mkuu.
"Lazima tutazame manufaa ya taifa, hata iwe ngumu kiasi gani, kwani maumivu ya sasa hayawezi kufananishwa na manufaa ya kesho"
Rais Goodluck Jonathan
Pia mjini Abuja, kuna taarifa kuwa vijana waliokuwa wamepiga kambi katika eneo la wazi la Eagle waliondolewa usiku na polisi kwa kutumia mabomu ya machozi.
Katika mji wa kaskazini wa Kaduna, kuna polisi wengi na mitaa iko kimya, huku maduka yote yakiwa yamefungwa, amesema mwandishi wa BBC Abdullahi Kaura Abubakar.
Shughuli pia zimesimama katika mji mkubwa wa Ilorin uliopo kusini magharibi mwa Nigeria, mtu mmoja anayefanya biashara sokoni ameiambia BBC. Alisema aliwataka wafanyakazi wake kusalia nyumbani baada ya kuona magari mawili yakifanyiwa uhalifu.

Ongezeko

Kumekuwa na maandamano yenye hamaki tangu kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta tarehe mosi ya Januari na gharama za mafuta, usafiri na nyinginezo kupanda pia.
Kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta kumewakasirisha wananchi wengi wa Nigeria, ambao waliona ndio faida pekee wanayopata kutokana na utajiri mkubwa wa mafuta wa nchi hiyo.
Maandamano
Mitaa haina watu
Wananchi wengi wa Nigeria ambayo idadi yao ni milioni 160 wanaishi chini ya dola mbili kwa siku, kwa hivyo ongezeko la bei limewaathiri sana.
"Kwa ongezeko hili, gharama za usafiri zimepanda na hii imeathiri gharama za chakula na mahitaji muhimu, kama vile kodi ya nyumba, ada za shule na gharama za hospitali," alisema Chris Uyot, msemaji wa chama cha Labour, moja ya waandaaji wa maandamano hayo.
Maandamano kama hayo mwaka 2003 nusura yasimamishe kabisa shughuli nchini Nigeria. Hali hiyo ilipungua baada ya serikali kukubali kupunguza kiasi cha ruzuku, badala ya kuondoa kabisa.
Wakati mgomo huo ukitarajiwa kuathiri wafanyakazi wa mafuta pia, vyanzo kutoka idara ya viwanda vinasema mgomo huo hautarajiwi kuathiri mauzo ya mafuta yasiyosafishwa nje ya nchi, limeripoti shirika la habari la Reuters.
Mafuta
Ukosefu wa miundombinu ya usafishaji unasababisha gharama kupanda
Licha yakuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta, Nigeria haijawekeza katika kusafisha mafuta, kwa hiyo ni lazima iagize mafuta ya petroli kutoka nje.
Kwa ruzuku kutolewa, mafuta huuzwa kwa bei rahisi nchini Nigeria kuliko nchi majirani, kwa hiyo mafuta mengi yalikuwa yakiuza nje ya nchi kwa njia za ulanguzi.
Wabunge wamemtaka Rais Goodluck Jonathan kufikiria upya jambo hilo, lakini alisema ruzuku hiyo ina athari za kisiasa.
Rais alitoa hotuba kupitia televisheni siku ya Jumamosi kutetea kuondolewa kwa ruzuku na hatua nyingine za serikali za kubana matumizi.
"Lazima tutazame manufaa ya taifa, hata iwe ngumu kiasi gani, kwani maumivu ya sasa hayawezi kufananishwa na manufaa ya kesho."
Jonathan
Rais Jonathan ametetea kuondoa ruzuku
Mabadiliko katika sekta ya petroli, alisisitiza, ndio njia nzuri ya kupambana na ufisadi na kuhakikisha uchumi unakua.
"Ukweli ni kwamba, sote tunakabiliwa na mambo mawili... ama tuendelee na hili na uchumi wetu uendelee au tuendelee kutoa ruzuku ambayo itateteresha uchumi wetu na tukabiliane na matatizo makubwa."
Alisema maafisa wa ngazi za juu, kuanzia mwaka huu, watakatwa mishahara yao kwa asilimia 25, na safari za nje ya nchi pia zitapunguzwa.
Serikali imesema itatumia dola bilioni 8 ambazo zitatokana na kubana matumizi, katika kuweka hali bora katika sekta ya afya, elimu na tatizo sugu la umeme nchini humo.
Hata hivyo, wananchi wengi wa Nigeria wanahofu kuwa huenda fedha hizo zikaishia katika mifuko ya mafisadi.
Mwezi uliopita, mkuu wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde alisifu jitihada za Rais Jonathan za kufanyia mabadiliko uchumi, lakini alionya kuwa nchi hiyo haina budi kutotegemea mapato ya mauzo ya mafuta nje.
 BBC

Sunday, January 8, 2012

JKT YAIPIGA ABC RBA

 wachezaji wa Timu za JKT na ABC wakifanya mazoezi madogo kabla ya mpambano kuanza


 Wachezaji wa Timu ya ABC

 Juma kisoky akipeana mkono na mgeni rasmi

 Mchezaji wa JKT akisaliamiana na mgeni rasmi

 Mchezaji wa ABC Steve Macho

Mashindano ya mpira wa kikapu kwa Mkoa wa Dar es Salaam yameanza jana huku wapinzani wa jadi kwa Temeke ABC na JKT wakifungua rasmi pambano hilo nakumalizika JKT ikiibuka kwa ushindi wa vikapu 60 kwa 54 vya ABC mashindano hayo yatakuwa yanachezwa katika uwanja wa ndani wa Taifa